Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,050
- 79,392
Hamjambo!
1. Kuna mambo yanafurahisha Sana nchi hii.
2. Wapo watu waliokuwa wafuasi wa Mwandambo Mzee wa nachoka kabisa.
3. Kuna watu ni wafanya vichekesho, vituko, content creator. Sasa ni kosa kubwa kushindwa kuwatofautisha na wapigania Haki.
4. Kwani utajikuta unadandia mitumbwi ya vibwengo na Kila mara utakuwa disappointed.
5. Mwandambo huhitaji elimu kubwa kujua yeye sio mwanamageuzi, sio mwanaharakati, sio mpigania Haki. Ni kosa kubwa Sana utalifanya kumuamini MTU katika nafasi isiyo yake.
6. Mwandambo kwenye maelezo yake baada ya kutoka anajieleza kinyume na kilichomfanya akamatwe.
7. Mwandambo hakuwahi kuwa na tatizo na Samia, na hakukamatwa kwa kuwa na tatizo na Samia.
8. Mtu kuwa mkosoaji wa serikali au kumkosoa Rais Samia hiyo haimaanishi unatatizo na Samia.
9. Kitendo cha kuchukulia Jambo personal au kumshambulia mtu personal kinamuondoa MTU kwenye upiganiaji haki, uanaharakarati na kuwa na agenda zingine za kibinafsi.
10. Ni sawa na kiongozi wa serikali achukulie mambo personal anaposhughulikia mambo ya kitaifa. Lazima avunje Sheria na uzalendo ukae pembeni.
11. Mwandambo amekamatwa, amewekwa ndani, madai yake anasema aliwekwa kwenye chumba chenye wadudu. Anamaanisha wadudu wasiorafiki.
12. Muda huohuo anasema alimchagua Samia, sijui Hana tatizo na Samia. Kwani nani alimwambia anatatizo na Rais?
13. Credibility ya Mwandambo ingebaki palepale kama angeeleza na kubaki na msimamo wake kuwa yeye ataendelea kuikosoa serikali kwa Nia njema kama mpenda nchi. Haijalishi viongozi WA serikali watatafsiri vipi. Kwa sababu lengo na Nia yake ni kurekebisha basi yeye angebakia hapo.
14. Ushasema huna ugomvi na Rais Samia. Mpe makavu sasa kwamba Rais mimi sina ugomvi na wewe lakini nilipokamatwa Sheria na haki haikufanyika. Eleza kwa namna ipi haki na Sheria hazikufuatwa.
15. Mfano uliotoa kwamba ulilazwa chumba chenye wadudu ni kielelezo cha kumwambia Rais wako ambaye huna matatizo naye. Mueleze watu wanaokamatwa ukiwemo wewe mnapelekwa kwenye maeneo yanayohatarisha afya na utu wenu. Simple.
16. Eleza unapinga na kukemea mambo hayo kwani hayaendani na utu na haki za binadamu. Na yanachafua sifa ya serikali. Eleza.
17. Sio unacheka cheka. Mara akae mjomba wako sijui Babu yako kwenye kiti cha urais. Hiyo ni dalili ya kukata tamaa. Kujivua nguo, kujidharau. Kuonyesha akili imekuwa contained.
Unajivua nguo hadharani kweli.
18. Haya serikali itakudharau, wananchi watakudharau, wewe utajidharau.
19. Huyo Rais mwenyewe atakuona mavimavi.
20. Tundu Lisu anaweza kuwa na madhaifu mengi lakini tabia yake ya msimamo, ukweli na kupigania anachokiamini ndicho kinamfanya aheshimike sio tuu na wafuasi wake Bali hata serikali na watesi wake.
Sio ajabu Rais Samia kule Zanzibar kumuita Yule Simba Tundu Lisu.
21. Mzee Warioba msimamo wake na tahadhari katika hotuba zake bila kuathiri msimamo wake wa nyuma ndio unamfanya azidi kuheshimika na serikali na watu.
22. Kuna mambo ukiyafanya hayahitaji bendera fuata upepo. Kutokuwa na Msimamo.
Mojawapo ni kupigania HAKI au kusema UKWELI.
23. Hakuna kitu watawala wanakipenda kama kukudhalilisha yaani kukuyumbisha msimamo wako ili uonekane kigeugeu.
Kwa sababu ukishakuwa kigeugeu unapoteza nguvu na ushawishi. Hakuna atakayekuamini hata wewe utakuwa hujiamini. Utadharauliwa na kujidharau.
24. Ni pigo takatifu. MTU anaweza kukutesa, kukuumiza na kuutoa utu wako kwa kukuvunjia haki zako lakini heshima yako Ikabaki palepale. Kwa anayekutesa na watu waliosikia habari zako.
25. Yaani mtu anakutesa lakini moyoni anasema hiki chuma. Respect. Kwa sababi ya msimamo.
26. Mtesaji hafurahii anapokutesa. Hiyo no saikolojia.
Mtesaji anafurahi unapojizalilisha mwenyewe. Unapojivua nguo. Anafurahi kwa sababu heshima yako umeivua mwenyewe.
27. Zingatia hakuna mtu anayeweza kuivua heshima yako zaidi yako mwenyewe.
28. Ndio maana adui zako hawatafurahi wakikudhalilisha kwani hudhaliliki kwa kudhalilishwa. Unadhalilika kwa kujidhalilisha.
Ni hayo tuu Kwa Leo.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam