Mwanaume mzima unashika shika........!

Mwanaume mzima unashika shika........!

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,444
.......mwanaume zima unashika shika mikoba ya wanawake!! we vipi??? Yalikuwa ni maneno yaliyonichoma barabara moyo wangu tena kutoka kwa mwanamke ninayempenda kuliko wote, yaani mke wangu!!!

Ilikuwa hivi, ametoka kazini akanipitia mimi kazini kwangu tukawa tunajirudisha home taratiibu na stori mwanana za kutaniana hivi na vile bora tumekutana tunaopendana!!!

Ugomvi ulianzia nilipopokea simu ya mfanyakazi mwenzangu akinitaarifu kuwa report niliyotuma, attachment haikwenda ambayo ndiyo report yenyewe!!! So nitume tena na kwa haraka sana coz makao makuu wanaisubiri jioni hiyo hiyo!!! Niliwasha laptop yangu nikakuta ina umeme kidogo sana nilichofanya ni kuibeba kwenye flash na nikalazimika kumuomba mke wangu laptop yake ili niitumie kwa muda huo!!!

Ye wife anatumia mini laptop ambayo inaingia kwenye mkoba wake anaoweka na vitu vingine vya kike, kiukweli sikusubiri jibu lolote toka kwake nikafungua mkoba wake na kutoa min laptop yake nikaiwasha na kuanza kutumia, kumbe mwenzangu muda wote huo hakuniona ila alinielewa kuwa nahitaji laptop yake!!!

Aliposimamisha gari na kunigeukia akakuta natumia tayari, daah!!! Yalimtoka maneno ambayo sijawahi kuyasikia kinywani mwake tangu namfahamu (moja wapo ni hayo niliyotumia kama title aya ya kwanza)!! Alikasirika mwanamke mpaka nikashangaa, sikumjibu kitu kwani nilituma niliyoyatuma nikazima laptop yake nikamrudishia!!!

Katika kudadisi kwangu niligundua yafuatayo;
1. Alikasirika sababu nimefungua mkoba wake, Je wana JF mimi kama mume mtu siruhusiwi kugusa mkoba wa mke wangu na kuufungua??
2. Alikasirika mimi kuwasha laptop yake kwa madai kwamba ile ni kitu binafsi kama ilivyo simu so nilipaswa kusubiri aniwashie!! Wana JF laptop pia ni restricted kwa mume/mke???

Kifupi mie sijaongea nae kitu mpaka sasa coz mihasira mingi na nimejikuta nina mengi yanazunguka kichwani nataka kwanza nitulie ili nilianzisha tuelewane vizuri!!!

Ila bado najiuliza nilikuwa sahihi ama nimekosea??? Wana JF mnaonaje hili????

Nawasilisha
 
Act like an african husband ,si ni mke wako kabisa anachokutisha nini ?.Likely kuna biashara haramu (anauza share zako)
anafanya that`s why anakuwa mkali ,sijui hawa viumbe wameumbwaje jamani wanamatatizo mno ,pole sana mkuu
 
Huyo mkeo hakueshimu mpaka anakuwakia hivyo? mimi ninavyoelewa mkishaoana mnakuwa wamoja sasa mwenzetu privacy inatoka wapi? Privacy huja kwa maelewano na maridhiano lakini sio yakuwa amriwa tena na mkeo aliyepashwa kukuheshimu mbali ya hapo ukiangalia mazingira ya tukio sio ya kuwa ulikuwa unampekua lakini lilikuwa suala la urgency.
Ni vizuri kukaa na mkeo mpendwa na kumuonya juu ya tabia yake, kwani kaonyesha kujishuku as if kuna kitu anaficha............its better you find out what it is.
 
Mkuu, mke ni partner wa karibu sana na haipaswi kuwa na restrictions zozote za kugusa mkoba wala kitu kingine chochote. Kwenye mikoba ya wanawake wanabeba simu, pedi za kike kama tarehe ni karibu na hedhi, lipstick, chewing gum, perfume etc. Hapo kuna cha ajabu? Ukoona mkeo anakuwa mbogo kwa kugusa kitu kama laptop au simu basi ujue kuna siri nzito!! Tafuta kujua siri hiyo ama kwa amani au shari. Wanawake kimsingi huwa wapole kama hana cha kuficha lakini ukiona vinginenvyo tafakari!!
 
Tulia na chukulia kama mkeo nae alighafilika baada ya kuona mkoba wake umefunguliwa,inawezekana ni jambo ambalo huwa hapendi ndio maana kalisema,vipi mama akiwa anapitia wallet yako utamind?
 
iyo laptop ina zaidi ya uo mkoba kuna kitu ambacho alikuwa anakificha so ana waswas unaweza kujua ndo maana kawa mbogo jaribu kumfanyia uchunguzi wa hali ya juu c mke wko utajua tu. There is sm thng going on.
 
Huyo mkeo hakueshimu mpaka anakuwakia hivyo? mimi ninavyoelewa mkishaoana mnakuwa wamoja sasa mwenzetu privacy inatoka wapi? Privacy huja kwa maelewano na maridhiano lakini sio yakuwa amriwa tena na mkeo aliyepashwa kukuheshimu mbali ya hapo ukiangalia mazingira ya tukio sio ya kuwa ulikuwa unampekua lakini lilikuwa suala la urgency.
Ni vizuri kukaa na mkeo mpendwa na kumuonya juu ya tabia yake, kwani kaonyesha kujishuku as if kuna kitu anaficha............its better you find out what it is.

Mdada una maneno ya busara sana.... Basi tu!!!!

Mtoa mada fuata huu ushauri.......
 
Kimsingi una haki ya kujiuliza,usipojiuliza utakua juha.
'
Lakini kukaa kimya ni kuongeza tatizo,majadiliano yanaweza yakakupa majibu ya sababu ya yeye kuchukia.
'
Kumbuka yeye kama ni mke mwema atajua umuhimu wa kujadili jambo lililosababisha mkwaruzano.
'
Kumbukeni kujadiliana kwa upendo na lengo lenu lisiwe kupata mshindi ila suluhu ili kuepusha mgongano wakati mwingine.
'
Jadilianeni mjifunze!
 
Sisi wanawake ni selfish sana sana ,mfano rahisi utakuta wote mnafanya kazi ila hela itakayotumika ni ya mume tuuu kwa kila kitu home ya kwako niyakuvaa tu soooo selfish .huyo dada ana jambo la ziada lakukuambia juu ya kauli yake .mimilait ningezaliwa mwanaume nsingeruhusu kuchezewa namna hiyo muna thamani kubwa sie viumbe dhaifu na wadogo sana kwenu.mwite kwa sauti mwambie kaa pale explain kila neno ulilolitoa siku ile alaaah unammezea mate ya nini hataki mwambie akapumzike kwao.na at last usipumbazike kingono akiri hayo maneno yake .mwanaume bila udicteta haya matoto ya kike hayaendi,,ni bora kufuga mabata 10 kuliko mwanamke 1.huwa namwambia mume wangu mwanaume lazima uongee kwa sauti ijulikane nibaba ameongea la sivyo hata watoto watakupanda kichwani!!we bana bana pua atakuaibihs hivohivo mbele za watu.
 
Umeoa au umeolewa....?????

Si bora yawe hayo? Maana ndoa nyingi watu wanaishi ili mradi wanaonekana ni familia,lakini si mke kweli,na si mume kweli..
Kwa hiyo ni ile wao wanaita heshima,Ati Mr X ameongozana na Mrs X.. Na wana watoto wao,basi.
Lakini yakiwakabili mambo magumu ya ndoa,mfano kusucrifice baadhi ya mambo au vitu,utawajua.
 
ukute anayake kwenye saved files hizo..yeye ana kijamaa chake wanavyochapana. Au kwenye pochi yake..unaliwa mke wewe.
 
tangu nimeolewa miongo kadhaa nyuma mume wangu akishika pochi yangu ujue kaniomba kitu nimemwambia kachukue kwenye pochi....... Tena sometimes ataileta ili nimtokee.....nitamuuliza kwa nini..

Ila kwa case yako inaonyesha kama kuna jambo mkeo anakuficha......laptop ina siri nyuma yake....halafu mbona kakwambia kwa lugha isiyo na staha? Hakufundwa kwao?
 
ukiona mkeo anakuwekea limit ujue kuna shida, chunguza utabaini ukweli.
 
Ndugu yangu mikoba ya kina mama huwa inabeba vitu vingi. Ninahisi mkeo alikwenda kwa mganga akapewa midawa, sasa wewe kuchungulia bagi yake ikawa noma, utawezaje kuangalia mihirizi? na kama wewe ni mcha Mungu ndiyo basi tena, Kuwa mwangalifu, ungemwacha akutolee yeye mwenyewe hiyo laptop.
 
Huyo mkeo hakueshimu mpaka anakuwakia hivyo? mimi ninavyoelewa mkishaoana mnakuwa wamoja sasa mwenzetu privacy inatoka wapi? Privacy huja kwa maelewano na maridhiano lakini sio yakuwa amriwa tena na mkeo aliyepashwa kukuheshimu mbali ya hapo ukiangalia mazingira ya tukio sio ya kuwa ulikuwa unampekua lakini lilikuwa suala la urgency.
Ni vizuri kukaa na mkeo mpendwa na kumuonya juu ya tabia yake, kwani kaonyesha kujishuku as if kuna kitu anaficha............its better you find out what it is.
nimeshakupendea huku kwene comment.
badotu kukuona nikwambie livelive.
 
Sisi wanawake ni selfish sana sana ,mfano rahisi utakuta wote mnafanya kazi ila hela itakayotumika ni ya mume tuuu kwa kila kitu home ya kwako niyakuvaa tu soooo selfish .huyo dada ana jambo la ziada lakukuambia juu ya kauli yake .mimilait ningezaliwa mwanaume nsingeruhusu kuchezewa namna hiyo muna thamani kubwa sie viumbe dhaifu na wadogo sana kwenu.mwite kwa sauti mwambie kaa pale explain kila neno ulilolitoa siku ile alaaah unammezea mate ya nini hataki mwambie akapumzike kwao.na at last usipumbazike kingono akiri hayo maneno yake .mwanaume bila udicteta haya matoto ya kike hayaendi,,ni bora kufuga mabata 10 kuliko mwanamke 1.huwa namwambia mume wangu mwanaume lazima uongee kwa sauti ijulikane nibaba ameongea la sivyo hata watoto watakupanda kichwani!!we bana bana pua atakuaibihs hivohivo mbele za watu.

Samahani kuna mtu ametumia ID yako na kuchakachua maoni na ushauri akijidai ni wewe ninaekufahamu...Ni hayo tu mpendwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom