Mwanaume kwenda shoping ama sokoni ni vibaya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume kwenda shoping ama sokoni ni vibaya?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BabaTina, Feb 3, 2009.

 1. BabaTina

  BabaTina JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 362
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 80
  wanajamii wenzangu mie naomba mnisaidie eti wanaume wa makabila yetu ya kiafrica huwa wanaona noma kwenda sokoni ni kweli ?

  pili kuna umuhimu wowote wa kufanya budgeting kwa ajili ya shoping au popote tu pale utakapotokutana na kitu ukakitamani unanunua ?

  haya maswali mie yananitatiza sana....tusaidiane jamani
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Nimeo na nimeishi na mke wangu kwa zaidi ya miaka 10 sasa. Kwa zaidi ya miaka 2 nimekuwa nikienda sokoni kila jmosi kwa kuwa mke wangu anafanya kazi hadi siku hiyo. Kama kuna umbaya wowote labda ni kwa wale wenye matatizo binafsi (kind of inferiority complex). Najisikia raha sana kuona familia yangu inapata mahitaji yote muhimu na mimi nikiwa nimeshiriki kikamilifu kuhakikisha yanawafikia.

  Kwangu mimi, ni muhimu kuwa na budget vinginevyo unaonekana ****. Utaendaje sokoni bila kujua unachotaka kununua? Kwa bidhaa za matumizi ya kila siku, ni vuzuri kuwa na orodha ya vitu ambavyo mnavitumia. Ila kama unakuta kitu kingine unchodhani ni kizuri, unaweza kubadili orodha yako au kununua kidogo kwa majaribio. Tatizo linakuwa kwa vitu kama nguo, viatu n.k hasa hasa kwa akina mama. Ushauri wangu ni kupunguza tamaa ya kununua vitu hovyo. Kwa hiyo unaweza kuona kitu kizuri, ukajizuia kununua ili upate muda ya kufanya maamuzi.
   
 3. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwanam-ume kwenda sokoni ni sawa sawa, bila kujali kabila lake.(Kumbuka wakati wa ma-KABILA hakukuwa na ma-SOKO, kulikuwa na ma-GULIO)

  Kupanga Bajeti ya nini cha kununua unapoenda sokoni ni ishara ya u-KOMAVU wa akili
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwenda sokoni ni kwa yoyote (mme ama mke), vile vile kuwa na budget ni muhimu katika kufanya saving. Mme na mke ni vizuri washauriane vitu gani vya kununua kwa siku, wiki ama mwezi. Ni ngumu na upotevu wa fedha kujinunulia vitu kila unapotamani, labda kama uwezo ni mkubwa sana.

  Kuhusu jamii zionazo kuwa kazi ya kwenda sokoni ni ya mke. Hayo ndio mambo ya "Mfumo Dume", sokoni kazi ya mke, kufua mke, kusafisha nyumba, kuchota maji kama yanapatikana mbali mke, kubeba mtoto kama mnatembea pamoja mke nk. Huu mfumo unaondoka taratibu.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mume anafanya kazi gani?
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kufanya budget ya shopping ni muhimu sana katika familia zetu ambazo vipato vyetu ni vya kawaida na tuna mambo mengi ya kufanya pia! So unaweza kupanga labda kwa wiki au siku au mwezi mtatumia kiasi gani na kununua nini! Hata na hivyo, unaweza ukapita sehemu na kukuta kitu fulani kizuri kwa familia ukaamua kununua si mbaya!

  Suala la nani aende sokoni mi nafikiri inategemeana sana na uhusika jikoni, kama mwanamme pia huwa yupo jikoni pia, nivizuri hata ukaenda sokoni cuase utanunua vitu muhimu unavyohitaji kwenye mapishi yako...lakini kama huhusiki sana jikoni nafikiri ni vema ukaachia vijana wa jikoni, silazima awe mkeo!

  Kwa ujumla, mwanamme kwenda sokoni si kitu kibaya kabisa.....just ni arrangement zenu kwenye familia!
   
 7. BabaTina

  BabaTina JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 362
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 80
  bila ya shaka nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote mlionisaidia kupata majibu kwa maswali haya yalokuwa yakinisumbua akili yangu.
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kuna baadhi ya wanaume wanaona noma kwenda sokoni hasa hasa kwa vitu vinavyohusiana na jikoni. Sababu kubwa nadhani ni mfumo dume ambao umegawa majukumu ya jikoni kwa wanawake (ukionekana una play role ya mwanamke watu wananza kujiuliza kulikoni!).

  Hata hivyo, kuja kwa maduka ya kisasa (supermarkest, malls etc) kunabadilisha kwa kiasi kikubwa attitude ya wanaume. Ukitembelea maduka haya utakuta wanaume wengi tu wakifanya shopping ya vyakula na vitu vinginevyo vya jikoni (mara nyingi wakiwa na wenza wao). Hili linajitokeza zaidi kwa wanaume walioelimika (wengi hawaoni tatizo kwenda sokoni wakiongozana na mamsapu).

  Mfumo dume unamfanya mwanamke kuwa mjuvi zaidi wa masuala ya jikoni(au mambo ya nyumbani kwa ujumla) kuliko mwanaume na hivyo yupo katika nafasi nzuri ya kujua mahitaji kwa usahihi zaidi kuliko mwanaume. Hivyo bado kwa sehemu kubwa wanawake ndio wanaokwenda sokoni kwa vitu yanayohusiana na jikoni.

  Umefanya vizuri kuunganisha maswali haya kwa pamoja.

  Ni vizuri kuwa na bajeti ya fedha na kiasi/aina ya vitu mnavyohitaji (needs) na mnavyotaka(wants). Ni lazima mnunue kwanza vitu mnavyohitaji na baadae mnaweza kununua vitu mnavyotaka (kama fungu bado linaruhusu).

  Wanawake mara nyingi wanaanguka kwenye mtego wa kununua vitu wanavotaka kwanza (impulse purchase behaviour) kabla ya vitu wanavyovihitaji. Mama anaweza akatoka na pesa nyumbani ya kununua mchele lakini akapita njiani akaona kiatu kizuri na papo hapo plan ikabadilika!Hivyo kujihusisha kwa mwanaume katika shopping kunasaidia ku-balance hivyo vitu viwili (needs and wants) na pia hata kukuza/kuimarisha mapenzi yenu.
   
 9. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nimependa observation yako kuhusiana na hili ulilosema maana kuna wanaume wengine wana-assume ni lazima mke afanye yote haya pamoja na mengine mengi kama kufua, kutunza nyumba etc shughuli ambazo anaona ni za kike. Swali inakuja pale ambapo huyu mama ni mfanyakazi na analeta kipato ndani ya nyumba. Anapobanwa na shughuli akimuomba mumewe kwenda kufanya haya na mume anakuja juu kama mbogo na anaona heri watu siku hiyo walale njaa kuliko yeye kwenda sokoni.

  Nimeshuhudia yafuatayo;
  1. Baba akimaka tena kwa matusi mengi yenye dharau kwa mwanamke tena hapo anazungumza na mkewe tena kwa sauti mbele ya watu, kuwa ni heri watu wafe njaa kuliko yeye kwenda sokoni

  2. baba akimpiga mkewe kisa mkewe ka-suggest aandae list ya shopping kwa sababu yeye (mkewe) anawahi kwenda kufanya kazi. Mkewe alipata kipigo cha mbwa, ndugu yangu usiombe, sababu ya kuandika list ya shopping na kwenda sokoni kununua chakula ambacho yeye atakula na watoto wake watakula hapo badaye.

  Basi ikiwa mama ndio mjuvi wa mambo ya jikoni basi wanaume wawe wajuvi wa kujenga maisha za familia zao. unakuta the same person anashindwa hata kuendeleza maisha ya familia yake then why endeleza mfumo dume ikiwa haukusaidii na hauleti maelewano ndani ya nyumba yako? Basi tuelezane wanaume ni wajuvi wa nini hasa katika maisha ya nyumbani? Kutawala nyumba zao? Kupiga wake zao? Kuwa waamuzi wa mwisho katika yote?


   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Feb 3, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya mahusiano magumu sana. Kila jinsia inapenda kulaumu jinsia nyingine kuwa ndio yenye matatizo. Mi naona ni bora mtu kuwa mwenyewe (single) tu kuliko kuwa kwenye uhusiano na mtu. Lakini huo ni uamuzi wa mtu...
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,730
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu sioni ubaya wowote ule wa mwanaume kwenda sokoni au shopping. Kuhusu kufanya budget ni muhimu hasa katika uchumi huu wa leo maana utaona vingi utakavyotamani na kama huna budget basi si ajabu ukatumia zaidi kuliko kipato chako na matokeo yake kujiongezea madeni yasiyokuwa na ulazima wowote ule.

  Mchango wangu wa thumni..:)
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Feb 4, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Babatina... Unaweza kuwa mfano bora katika familia yako kwa kuonyesha kwa vitendo kuwa wewe ni baba uliye bora kabisa. Kwa kuyafanya yale yote ambayo kwa wanaume wengi kinadharia ni rahisi, ila vitendo ndio kila mtu na siri yake.

  Nikuulize swali, kwani huko sokoni ni kitchen Party au wauzaji wake ni wanawake tu!? Soko ni la kila anayejisikia kwenda kuuza na kununua. Liwe Gurio, soko mjinga, soko kuu au la kimataifa. Soko ni la wote.
  Kwa nyongeza, hizi kazi za kupika, kufua, kuogesha watoto au kwa ujumla kazi za nyumbani. Kwani wapi tumeelekezwa kuwa ni za kike!? Au ndio kama alivyodokeza mdau hapa.
  Tatizo lingine ni ndugu, marafiki na majirani wanao tuzunguka. Imefikia kiwango tunaishi kwa kuwaogopa wao. Wanaume wengi wanaishi na majinamizi kwenye vichwa vyao... eti wakionekana wanafanya manunuzi sokoni au wakikutwa wanapika na mke yupo chumbani anasoma gazeti au kuangalia TV wataonekana kuwa wamelishwa this called "LIMBWATA" au dawa za mapenzi... huu ni ukosefu wa ufahamu. Hivi ni nani anatupangia, au kunipangia mimi au wewe jinsi ya kuishi na kusaidiana ndani ya nyumba?
  Si kazi huyo baba aliye andikiwa list ya shopping na mkewe akipata kijinafasi cha kwenda zake ughaibuni na kufanikiwa kuoa mwanamke wa kizungu kama si kukaa naye kimada, utamkuta yeye ndiye mpishi ndani ya nyumba. Kusafisha na kazi zote za ndani... ukiuliza utasikia "...Aaah thi unajuwa tena gero frendi wangu kana ka nthungu hapendi kupika...!"

  Babatina ukiwa na nafasi onyesha kuwa ulipokuwa bachela ulikuwa ulali njaa kwa kupika maanjumati. Na kule gulioni/soko mjinga unawajuwa wauzaji wa mboga mboga za leo leo... na wapi unapatikana utumbo safi wa ng'ombe...!

  Lakini ni wangapi wapo tayari kukutwa wapo Jikoni wakikuna nazi na Dada, Kaka, Wazazi, Wajomba, marafiki na majirani zao wanapokuja kuwatembelea...!?

  Kumbuka walio wengi wameathirika na huu mfumo unaopelea mwanamme kwenda kufanyakazi na mwanamke kubaki nyumbani. Akiangalia watoto.

  Hapo ndipo zikapatika hizo kazi za jikoni kuwa ni za kike...! Lakini je ikitokea kuwa Baba kakumbwa na ugonjwa wa ridandasi... Hakajikuta yupo chali miguu juu... Na mama watoto yupo anapiga mzigo... utafanyaje au ndio utakuwa mtu wa kwenda kushinda Tea cafe!?

  Wanaume wakati mwingine tunakuwa wabinafsi sana... Linapokuja swala la kuwa Professional basi Ma'chef 99.999% ni wanaume.
  Majumbani wanakuwa wakorofi, hawataki hata kukaribia jikoni.

  Pia kumbuka Mali bila Daftari, uisha bila Habari! Kupanga Budget ni muhimu sana.

  Kila la heri Bro!
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Feb 4, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ila kuna tofauti ya kapu kujaa mamsapu akienda na 'bajeti' sokoni, na mume akienda sokoni kwa 'bajeti' hiyo hiyo...

  mara nyingi, ni vizuri mke kwenda, au mume na mke kwenda sokoni, kuepuka mume kuja bughudhiwa na mamsapu kwa kununua bidhaa siyo.
   
 14. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ...suala la sokoni ni dilema, mimi wa ubavu wangu hataki niibuke sokoni wala nini anadai atachekwa na wenzake kuwa ana mwanaume mbahili, however nilikuwa nakomaa mwanzoni ila nikasalimu amri, ila kwa ujumla ni suala zuri la kusaidiana, to cut the story short ni kuwa nilikuwa naliwa cha juu na wife kwa kwenda mbele, budget ya wiki ukimpa mnaishia alhamisi kila wiki!!nikaamua niwe natia timu mwenyewe market!!
   
 15. T

  Tom JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mahusiano ya mke na mume yote sawa tu mradi ni ndani ya sheria za nchi lakini lazima iwe maelewano, hata hivyo kimila, kama vile mume kulipa MAHARI wakati wa kuoa pia shughuli za jikoni ni muhimu kuwa chini ya mke la sivyo ndugu wa mume hawataridhika kuona ndugu yao anaenda sokoni.
  MUME KUONA NOMA KWENDA SOKONI ni MOJA ya TABOO, kama MAHARI nk ambazo zinaendelea kufa taratibu tokana na mabadiliko ya mahusiano ya kiuchumi ndani ya nyumba zetu.
  Budget si hiari, ni lazima kama sio fisadi.
   
 16. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimefurahishwa na mada hii. Kwa upande wangu kwenda sokoni kwa mwanaume si tatizo. Ila kuna kutokuelewa kwani wengine wakiona mume anaenda sokono wananjua mume amewekewa au amepewa limbwata. Kwa ushauri wangu mume kwenda shoping si tatizo.
   
 17. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Mimi naomba kuuliza, hivi Limbwata ni nini hasa (chakula, maji etc)? Linafanya kazi au ni imani tu?
   
 18. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Binafsi nadhani limbwata ni imani tu. Ila kuna mambo mengi ambayo watu wa sehemu tofauti wanaamini ni limbwata, kiwemo miti shamba na vitu vingine. Mfano wengine wanadai kuwa nyama iliyowekwa sehemu za siri za mwanamke akilishwa mwanamme anakuwa zezeta! Sasa haya mapenzi ya siku hizi ya kulambana nyeti ni limbwata? Labda ndo maana wanaume wengi siku hizi wanaenda sokoni, kupika, kufua nepi n.k!!
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Dec 19, 2013
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  haya wanaume fungukeni, unaagizwa nyanya na vitunguu na wife utaenda au?
   
 20. N

  NIFEDIPINE Senior Member

  #20
  Dec 19, 2013
  Joined: Aug 16, 2013
  Messages: 155
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Mwanaume kwenda sokoni si vibaya kabisa. Tena inaonyesha jinsi gani uko responsible na familia yako. Jambo la msingi ni kuweka bajeti kwa ajili ya manunuzi ya mwezi. Ikifika mwanzo wa mwezi nenda sokoni kanunue mchele,unga,mafuta ya kupikikia n.k vitakavyoweza kutumika kwa family yako atleast ndani ya mwezi au zaidi kulingana na uchumi ulio nao. Kama unafanya hivyo keep it up
   
Loading...