MWANAUME KUWA NA RAFIKI WA KIKE

Habari wana jamii wenzangu
Wenye upendo na utani unaotufanya
Tufurahi na kuelimika tukiingia katika mjumuiko huu wa majukwaa yetu.

Husikeni na kichwa cha habari hapo juu,
Mimi kijana wala sio mzee so bado najifundisha mambo mengi ya kwenye jamii zetu.
Najua humu tuna watu wazima waliopitia mengi kabla yetu sisi kizazi cha Mh. Mwinyi tulozaliwa na kukuta ile ruksa nadhani mnatutambua vizuri.
Binafsi ninae rafiki yangu wakike ambae huwa tunajadili mambo mbalimbali yakijamii
Kiutamaduni, maendeleo na elimu mbalimbali.
Tulisoma wote shule ya msingi ijapokua hapo hatukua marafiki kivile, na ilimu ya sekondari tulisoma shule tofauti.
Tumekutana tu tena tu ukubwani na kwasasa ana mchumba na mimi nina katoto kangu kazuri ka Iringa huko.

NB: nimeeka bayana isije wanamazengo wakasema tunatafunana.

Huo ulikua ni mfano tu na urafiki ni mkubwa kiasi tunashare karibia mambo mengi hata akipata tatizo au nikipata tunashauriana.

Nia ni kutaka kusikia machache kutoka kwenu kwamba ushkaji wa mwanamke na mwanaume huwa mnautazama katika mtazamo gani na huwa una tija zipi na hasara zipi hii nafikiri itajenga ufaham fulani baina yetu vijana natumaini majibu yatakua ya busara na maono ya kiutu uzima.

Pia tukieza fahamu haya yote nafikiri tutajenga jamii nzuri yenye mitazamo chanya kuhusu masuala kama haya.

Karibuni mtupe darasa pia vijana tupeane maarifa katika hili.

Ahsanteni.
Kwan ukimtafuna kuna ubaya gan kijana,.. y makin tings harder to uaself
 
Back
Top Bottom