Mwanaume KAMILI

Mwanaume kamili ni yule anaejiamini. .
Anaelewa thamani ya mwanamke na kumthamini!

Mwanaume kamili ni yule anaefahamu majukumu yake. .
Aliye tayari kusaidia, bila kusubiri mpaka atake!

Mwanaume kamili ni yule anaejielewa. .
Anaerudi nyumbani bila ya kulewa!

Mwanaume kamili anajua muda wa kurudi nyumbani. .
Hasubiri mama na wana wakamtafute kilabuni!

Mwanaume kamili anajua anapohitajika. .
Hujitahidi 'kuwepo' hata akichoka!

Mwanaume kamili anatambua umuhimu wake katika malezi. .
Anajua kuzaa pekee hakumfanyi mzazi!

Mwanaume kamili anajitahidi kuwa mwaminifu. .
Na hamwachi mwenzie atoke bila kumsifu!

Mwanaume kamili hufikiri kabla ya kutenda. .
Hafanyi makusudi kuumiza anaowapenda!

Mwanaume kamili hutumia neno 'samahani'. .
Hana makuu na kujikweza asilani!

Mwanaume kamili hupendeka. .
Hufanya iwe rahisi kwa mwenzi kucheka!!

Hongereni "wanaume kamili" wote ndani ya JF na uraiani. Kwa niaba ya wote wanaowakubali TUNAWAPENDA SANA. . Y'all are deeply appreciated!

Asante kwa kutupa sifa za mwanaume wako wa kufikirika. Kwenye utawala tungeiita hii ya kwako kuwa ni VISION ya mwanaume ambaye wewe unadhani kuwa ni kamili.
 
Asante kwa kutupa sifa za mwanaume wako wa kufikirika. Kwenye utawala tungeiita hii ya kwako kuwa ni VISION ya mwanaume ambaye wewe unadhani kuwa ni kamili.

Hapo cha kufikirika ni kipi haswa?
Kutokulewa? Kujali familia? Kutimiza majukumu? Kijielewe? . . . . . . .?
 
Aaah mkuu sipingi ila niko kiperspective zaidi...kunywa/kulewa...umegusa ikulu mkuu ha ha haaa.....sifa zoooooooote nnazo ila hii ya kurudi umekunywa, sorry kulewa....hold on.... mama Gaude anakuja upande huu!
 
Front gentleman, real man, perfect man to mwanaume kamili (complete man?).
Unfortunately, no one qualifies for that.
 
Hahahahaha. . .
Ukinywa sio lazima ulewe unajua!!
Acha kumtesa mama Gaude kwa kumsubirisha usiku usiku mkono kiunoni na mwingine kichwani kwa wasiwasi.
 
Hii nimeipenda kwa kweli, nimepata picha the type of mwanaume wapenda.... Ulie mdiscribe yupo Perfect, In reality ni ngumu saana kumpata but wenye bahati zao wanapata, na hopefully utawa mmoja wao.....

Kwa upande wangu Mwanaume kamili ni yule ambae ananielewa ipasavo na on top of that ananijali mno hata kama hajanipenda mno! akinielewa ipasavo atajua nini nataka, wakati gani nataka hicho kitu; Atanijua tabia zangu zoote, nikiwa sad/emotional/sensitive/happy/horny/depressed - na atatafuta njia mbadala wa kunifanya niwe normal. In short on one to one... Atanifanya nijiskie I am special and Woman indeed. Atakua baba mzuri wa watoto wangu na kutimiza wajibu wake kama baba na Mume. Ana Utu kwa wanadamu woote sio tu wakaribu wake.....

Mwanaume kamili huendana na mazingira yoote, hana mtindo wa kuuza sura, wakati wa kazi ni wakati wa kazi! Wakati wa kuuza sura ni wakati wa kuuza sura! He is at home anywhere... iwe shamba, iwe kazini (ofisini), iwe kijiweni, iwe kwa wakwe, iwe nyumbani kwake na hasa kila chumba (i.e jikoni), iwe mbele ya kundi kubwa, iwe mkutano, He rules..... either by being a low key player or high key player.... Awe anajua ana madhaifu na asiwe muoga wa kuonesha hayo madhaifu (walau kwangu kama mpenzi wake). Ajue kua yeye ni mwanadamu kama wengine, ili a-appriciate wanadamu wali mzunguka regardless hali zao...

Mwanaume kamili ni yule mwanaume hata his fellow men wish to be like him.....

Hii ya kwako imekaribiana na uhalisia kwa kiasi kikubwa. Ila kuna misemo imenitoa ushamba hasa ukizingatia mimi ni born bush.
  • Hivi kuuza sura ndio kufanya nini tena?
  • He rules..... either by being a low key player or high key player.... Hii inataka nyama kidogo.
  • Hii ya kutembelea jikoni itakuwa ngumu kidogo. Huchelewi kuambiwa unamendea house girl a.ka. beki tatu.
  • "Atanifanya nijiskie I am special and Woman indeed" Hii nayo ina utata kidogo. Inabidi uongezee nyama kidogo ili walau tujue ni mambo gani yakifanyika utajisikia kuwa "special and woman in deed". Na mwanaume atajuaje unapojisikia hivyo - i.e. feedback gani atarajie?
Ukinifafanulia hayo tu nitakuwa nimekuelewa vyema na unaweza ukatunga mtihani nikafaulu.
 
Front gentleman, real man, perfect man to mwanaume kamili (complete man?).
Unfortunately, no one qualifies for that.

Hhhm. . .
Real man? Perfect man? Haya bana. . .
Hata hivyo kila kimoja kinajitegemea and i'd like to keep it that way!!

Alafu huyo 'No one' unless ni jina la mtu sioni sababu ya kuongelea kila mtu wakati wapo wanaojua sifa wanazo!!
 
Mkuu saa tisa niko home (kazi yangu inaruhusu)...ila fridge langu sasa....almost brandy zote zipo...ila frankly sikuwah kulewa!
 
Hapo cha kufikirika ni kipi haswa?
Kutokulewa? Kujali familia? Kutimiza majukumu? Kijielewe? . . . . . . .?

Refer comment ya Ashadii. Kama kwa mtazamo wako hivyo vigezo ulivoviweka ndio kipimo cha mwanaume kamili, basi utaishia kuwa stress zisizo na mpango. Jaribu kuchakachua kidogo hizo sifa ili ziendane na hali halisi.
 
Nichakachue kwa faida ya nani?
Hizo stress ntapewa na nani?
 
he he he safi sana but mimi nalewaga although narudi nyumbani mapema.i also enjoy getting drunk with my bby grl,hilo nalo kosa?
 
Ujumbe kwa wanaume, kama unataka mwanamke kamili, mke mwema etc fanya kazi uwe na uhakika wa fwedha!

Though hata baadhi ya wanaume wanaofanya kazi na kuwa na uhakika wa fwedha wana nyumba ndogo. Inawezekana mwanaume akawa na mwanamke kamili lakini akaamua pia kuwa na nyumba ndogo?
 
Kwa upande wangu Mwanaume kamili ni yule ambae ananielewa ipasavo na on top of that ananijali mno hata kama hajanipenda mno! akinielewa ipasavo atajua nini nataka, wakati gani nataka hicho kitu; Atanijua tabia zangu zoote, nikiwa sad/emotional/sensitive/happy/horny/depressed - na atatafuta njia mbadala wa kunifanya niwe normal. In short on one to one... Atanifanya nijiskie I am special and Woman indeed.

Na news tutaangalia saa ngapi?
Kuna na magazeti ya kusoma pia. LOL.
A complete man is the one who has the understanding of the life and any field in the universe.
 
he he he safi sana but mimi nalewaga although narudi nyumbani mapema.i also enjoy getting drunk with my bby grl,hilo nalo kosa?
What's your definition of kulewa?

Yangu ni kunywa pombe mpaka akili zinaruka, badala ya kufungua mlango unahangaika kuingiza ufunguo ukutani. Ukiandaliwa chakula mkono unanawa kwenye bakuli ya mboga. . .

Kama hufiki huko kote basi endelea kufurahia.
 
Though hata baadhi ya wanaume wanaofanya kazi na kuwa na uhakika wa fwedha wana nyumba ndogo. Inawezekana mwanaume akawa na mwanamke kamili lakini akaamua pia kuwa na nyumba ndogo?

of course that is inevitable, ila siku nikijua stop ya kwanza angaza, tukitoka salama lolote linaweza fuata, wanasema never say never.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom