Mwanaume aliyempa talaka mke wake na kumuoa mfanyakazi wao wa ndani huko Zambia

Wanawake wa kiafrika ni mizigo mno hambebeki kwa lolote mtakalofanyiwa

Sasa wewe mwanaume anaenda kuchakarika kutafuta pesa,wewe huendi kazini upo tu nyumbani halafu ushindwe hata kazi ya kufua nguo na kuosha vyombo,sasa kazi yako ni nini?

Kwa nchi za ulaya mwanamke na mwanamme wote wanakwenda kazini,hapo wakiajiri housegirl inamake sense

Na kingine mwanamke wa Ulaya mahitaji yake anajihudumia mwenyewe hakuna usumbufu wa kupigana mizinga ya ajabu ajabu.
Huku kwetu bongo wanawake wanafanya mapenzi ni biashara, mwanamme anakugharamia kila kitu, mizinga ya kila siku anakuhudumia na bado hauna nidhamu, jeuri, nyodo, dharau

Tabu yote ya nini, hayo ni mapenzi au adhabu.
 
Yaani wanawake wa JamiiForums wamechagua kuona tu hoja wanazoweza kutetea. Mengine kama hawaoni vile.
 
hao Ni uliokutana nao wewe
 
mbona mke wangu hafanyi haya unayosema wewe na kila kitu kipo sawa hapa home. Acha uvivu we mwanamke.
 
Kuna mila na tamaduni za nje na za Afrika. Utamaduni wa Magharibi usitufanye tuache mila na desturi zetu kama alivyofanya huyo mtalikiwa. Tamaduni zinatofautiana kati ya nchi na nchi niliwahi kwenda Middle East kule mwanamke hatakiwi kutoka nje akiwa hajavaa ninja na pia mwanamke hatakiwi kwenda hata dukani wala kuendesha gari hata mpira kwenye TV mwanamke aruhusiwi kutazama.

Kule mwanamke ni kupika na kufanya shughuli za nyumbani zote na kuzaa watoto. Kitu hicho ni tafauti kwa wazungu na Amerika kule kuna haki sawa mpk zamu za kupika. Kwa Afrika tuna tamaduni zetu mie nimeoa halafu leo unikute napika au naosha vyombo hiyo katu sitafanya kutokana na mila na tamaduni zetu.

Kwetu huku mke kutompikia mume ni sababu tosha ya kuachwa na sio ndugu tu hata hakimu mahakamani anaona ni sababu tosha ya kuvunja ndoa.

Mimi binafsi mwanamke akitaka nimpende awe ananipikia nahisi upendo wangu una koneksheni kubwa na mapishi. If u want to win my heart cook for me
 
Wabunge viti maalum hili ni funzo kwenu, si kila siku mnalilia kumfurahisha huyo mnayemuita MTUKUFU, haya endeleeni mkirudi mtakuta waume zenu wameoa ma-house girl
 
Hapo umekwepa ukweli, wanawake wengi wakishaolewa, kazi inayobaki ni kumchunga mwanaume kama Mbuzi, wanakimbilia kwenye pesa, kiherehere unachoongea ni kuuliza, uko wapi, uko nani, umechelewa wapi, leo tunaenda wapi kwa dinner, tukamsalie,mama,dada,shangazi,rafiki yangu, shopping. ataka ajue mshahara,kipato, anataka kazını au kwenye biashara zako awajue watu unaofanya nao kazi/biashara, kila mahali uende naye. lakini mwisho wa yote anataka pesa. huo ndio usumbufu hasa kwa Mwanaume anayesumbua akili kutafuta maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…