Mwanaume aliyempa talaka mke wake na kumuoa mfanyakazi wao wa ndani huko Zambia

Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
Wanawake wa kiafrika ni mizigo mno hambebeki kwa lolote mtakalofanyiwa

Sasa wewe mwanaume anaenda kuchakarika kutafuta pesa,wewe huendi kazini upo tu nyumbani halafu ushindwe hata kazi ya kufua nguo na kuosha vyombo,sasa kazi yako ni nini?

Kwa nchi za ulaya mwanamke na mwanamme wote wanakwenda kazini,hapo wakiajiri housegirl inamake sense

Na kingine mwanamke wa Ulaya mahitaji yake anajihudumia mwenyewe hakuna usumbufu wa kupigana mizinga ya ajabu ajabu.
Huku kwetu bongo wanawake wanafanya mapenzi ni biashara, mwanamme anakugharamia kila kitu, mizinga ya kila siku anakuhudumia na bado hauna nidhamu, jeuri, nyodo, dharau

Tabu yote ya nini, hayo ni mapenzi au adhabu.
 
mbona mwanaume kaongea vitu vya msingi sana ambavyo ata uko nchi za magharibi wanavizingatia? mfano kuna mahala kalalamika kua mkewe hana muda nae kabisa kuna wakati anahitaji faraja,kubadilishana mawazo na muda wake pia lakin vyote hivi amekua anavita kwa house girl, mke yuko busy na simu muda wote na ikifika weekend ni vikao na harusi
Yaani wanawake wa JamiiForums wamechagua kuona tu hoja wanazoweza kutetea. Mengine kama hawaoni vile.
 
Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
hao Ni uliokutana nao wewe
 
Mwanamke sio kijakazi na akisahau hukumbushwa yeye ni nani. Amezaa tayari nimtu aliyechoka kukulelea watoto wako.

Hivi wanaume hebu chukueni upande wetu.
Unabeba mtoto miezi tisa hiyo miezi tisa tu kuibeba ni kazi halafu uje uzae ukishampata mtoto umnyonyeshe umfanye alale hadi azoee dunia na mazingira sio kazi rahisi ndio maana mama hueshimiwa huletewa msichana wa kazi ili afue ,apike , aoshe vyombo na ikiwezekana aletwe mwingine kwa ajili ya usaidizi.
Maisha ya kulea sio kazi rahisi ila wa baba kusaidia ni kazi sana .
Wao wanakuja tu wanakulalamikia kama yeye alizaliwa na baba chakula kiko wapi .
Hajui siku nzima ulipitia nini kulea nikazi.

Ila kama uyaya sawa.
Wewe unamakosa maana miezi sita tu ndio unapumzika.
Ila kama huna yaya kulea nikazi .
Huyo bwana hana akili si amesema yule mke wa mwanzo alifanya hayo mwanzoni ukiwa na familia try to understand you are wife mlikuwa wenyewe utatunzwa but if ukiwa na mtoto kwa heri baba.
Ukiwa mwelewa tafuta kipoozeo mke asijue .
mbona mke wangu hafanyi haya unayosema wewe na kila kitu kipo sawa hapa home. Acha uvivu we mwanamke.
 
Wanaume wa kiafrika ndo akili zenu zilipoishia..unafikiri ukishaoa mke umejipatia na mfanyakazi wa ndani, yeye huyo mume alikua amekamilika kwa lipi?? Sijaona sababu ya kuacha mke hapo na huyo msichana wa kazi ajiandae baada ya miaka kadhaa na yy atatafutiwa sababu., kama ninkazi wanawake kibao wanafanya kila kitu kwa waume zao bado wanaachwa na kufanyiwa ushenzi..bado tuna safari ndefu sana kwa mtindo huu Africa itabaki kuwa bara la giza milele na milele

Halaf cha ajabu hawa wanaume wanaoongea ongea amevunja ndoa yake na mikono yake mwenyewe anataka yeye apikiwe afuliwe afanyiwe majukumu yote ya mume ajabu muulize yeye kamnunulia lini mkewe hata chupi utasikia maisha ni kusaidiana mara na yeye ana kazi anunue mwenyewe, hapo analalamika hvo si ajabu wote wanafanya kazi na wote wanachoka kwa kiwango kile kile bado mtu ana thubutu kusema hafui mara hatandiki alafu zikija bili mwanaume mzima anaweka mezani agawane na mkewe nyie wanaume weusi mna shida jamani yani sijui mna akili za aina gani
Kuna mila na tamaduni za nje na za Afrika. Utamaduni wa Magharibi usitufanye tuache mila na desturi zetu kama alivyofanya huyo mtalikiwa. Tamaduni zinatofautiana kati ya nchi na nchi niliwahi kwenda Middle East kule mwanamke hatakiwi kutoka nje akiwa hajavaa ninja na pia mwanamke hatakiwi kwenda hata dukani wala kuendesha gari hata mpira kwenye TV mwanamke aruhusiwi kutazama.

Kule mwanamke ni kupika na kufanya shughuli za nyumbani zote na kuzaa watoto. Kitu hicho ni tafauti kwa wazungu na Amerika kule kuna haki sawa mpk zamu za kupika. Kwa Afrika tuna tamaduni zetu mie nimeoa halafu leo unikute napika au naosha vyombo hiyo katu sitafanya kutokana na mila na tamaduni zetu.

Kwetu huku mke kutompikia mume ni sababu tosha ya kuachwa na sio ndugu tu hata hakimu mahakamani anaona ni sababu tosha ya kuvunja ndoa.

Mimi binafsi mwanamke akitaka nimpende awe ananipikia nahisi upendo wangu una koneksheni kubwa na mapishi. If u want to win my heart cook for me
 
View attachment 1713163
View attachment 1713185
Mwanaume huyu toka jamii kutoka Ndola aliamua kumuacha mke wake waliyeoana miaka saba iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Mwanamke huyu alienda mahakamani ilikutafuta suluhu ya ndoa yake na maridhiano na mume wake, akiomba mahakama imsaidie kunusuru ndoa yake na kuongeza kuwa hajui kwanini mume wake aliamua kuchukua uamuzi wa kumuacha na kuoa mfanya kazi wao wa ndani.

- Mwanamke huyu aliiambia mahakama kuwa anampenda mume wake na haamini kama kweli ameamua kufanya kitu kama kile na kutaka kujua sababu zilizopelekea mume wake afanye hivyo.

- Mahakama ilipomuuliza mwanaume juu ya suala hilo alisema hawezi kubadili msimamo wake na hawezi kumuacha mke wake mpya wala hawezi kumrudia mke wake wa zamani maana maamzi yake ndio yalikuwa yameshafika mwisho na kushukuru kumpata mtu sahihi kwake na kusema mwanzo alifanya makosa kwenye kuchgua mke bila yeye kumjua mwanamke huyo vizuri.
Akaendelea kuaiambia mahakama kuwa mke wake huyo wa zamani alikuwa mzembe kupita kiasi, hakuweza hata kufanya kazi za ndani zinazomhusu kama mama wa familia na badala yake hata yale majukumu yake kwa mumewe aliyaacha mikononi mwa mfanyakazi wao wa ndani ambaye alijikuta kuwa ndio msaada mkubwa kwa mwanaume huyu , mfanyakazi wao wa ndani ndio aliyefua nguo zote za mwanaume huyo huku mke wake akiwa hana habari nae, hakutaka hata kukaa na kuongea na mume wake isipokuwa mfanyakazi wa ndani alikuwa akimuona amerudi toka kazini anampokea na kumuandalia maji ya kuoga, kisha anampa chakula na kukaa na kuongea nae sebuleni huku akimpa pole kwa uchovu na kumtia nguvu pindi anapoonekana kuchoka sana au kuwa na mawazo.

-Kuhusiana na suala hilo wazee walishawakalisha chini na ili kuwapatanisha bila mafanikio yeyote kwa wanandoa hao.

Alichokuwa akikifanya mwanamke huyu nyumbani ni kuwa bize kutoa maelekezo kwa mfanyakazi huyo wa ndani na kumfokea muda wote na kuwa bize na simu huku mfanya kazi wa ndani akiwa bize na mwanaume baba wa familia, hivyo niliona kila mtu abaki na kitu anachopenda kuwa bize nacho muda wote, mfanyakazi wa ndani anapenda kuwa bize na baba wa familia basi ni vyema awe nae aliatimize majukumu yake kwa baba wa familia vizuri, na mke wake kwa sababu yuko bize na simu basi nimuachie nafasi akae na kuchati kwa uhuru ili kila jambo liende sawa pia kwa upande wake.
Mume aliendelea kusema hata siku za mwisho wa juma (weekends) akiwa hayuko kazini mwanamke hakuona umuhimu wa kupika chakula kwa ajili ya mume wake kama alivyokuwa akifanya siku za mwanzo wa ndoa yao,badala yake alikuwa akifanya maandalizi ya kwenda kwenye sherehe za harusi na kamati za Kitchen Party, anarudi amelewa kitu ambacho mwanzo alikuwa hafanyi, na kama angekuwa anafanya nisingemuoa kabisa.

-Mume akaenda mbele zaidi na kuiomba mahakama iangalie kwa makini kucha ndefu za mwanamke huyo kama kweli zinaonesha mwanamke anayeweza kujishughulisha na shughuli za nyumbani kama mke wa mtu, muulizeni ana miaka mingapi hajawahi kupika chakula, kufanya kazi za nyumbani zaidi ya kuagiza, nani amekuwa akitandika kitanda changu kwa muda wa miezi nane sasa ?, Ni lini amejishughulisha hata kutunza na kuangalia watoto kama kweli ni mwanamke anayefaa kuwa mke, hayo yote mfanyakazi wa ndani ambaye ni mke wangu sasa ndio amekuwa akiyafanya siku zote.

Baada ya mahakama kujiridhisha na maneno ya mume ikatengua ndoa hiyo ili sasa mwanamke aendelee kuchat bila kikomo, ahudhurie sherehe za fungate, harusi na kufuga kucha huku mfanyakazi wa ndani akiwa boss ndani ya nyumba mwenye kujua na kujali majukumu yake kwa undani.

Wanaweke wengi huyajua makosa yao na ukimya wa mwanaume humfanya ayaendeleze bila kujua mwanaume muda mwingine yuko kimya akiwaza hatima ya jambo hilo na mwisho anaweza kuja na uamzi mwingine

Kuna la kujifunza.
Wabunge viti maalum hili ni funzo kwenu, si kila siku mnalilia kumfurahisha huyo mnayemuita MTUKUFU, haya endeleeni mkirudi mtakuta waume zenu wameoa ma-house girl
 
Mtu mke na mtu mme hukutana na kuanza mapenzi motomoto

Wakishazoeana ubunifu huisha, hakuna kujitoa kwa mwenzie kila mtu anamtegea mwenzie ndo awe na amsha amsha.

Na atayekuwa na kiherehere cha kuwa na amsha amsha ili mahusiano yasilege ataonekana msumbufu, mkabaji, hana shughuli za kufanya kazi kufatiliana na kubanana.....

Watu hubadilika kutokana na nyakati, mazingira, watu wanaowazunguka n.k.

Ukiona uko kwenye mahusiano na mtu na anakuheshimu huyo mtu mrejeshee heshima, nakwambia lazima mstaafu pamoja hata kama mapenzi yameisha.

Mpende mkeo...

Mpende mmeo.....

Mpende mwanao....

Alisikika Machinga mmoja akinadi mataulo ya mtumba maeneo ya Karume jijini Daslamu 😅.
Hapo umekwepa ukweli, wanawake wengi wakishaolewa, kazi inayobaki ni kumchunga mwanaume kama Mbuzi, wanakimbilia kwenye pesa, kiherehere unachoongea ni kuuliza, uko wapi, uko nani, umechelewa wapi, leo tunaenda wapi kwa dinner, tukamsalie,mama,dada,shangazi,rafiki yangu, shopping. ataka ajue mshahara,kipato, anataka kazını au kwenye biashara zako awajue watu unaofanya nao kazi/biashara, kila mahali uende naye. lakini mwisho wa yote anataka pesa. huo ndio usumbufu hasa kwa Mwanaume anayesumbua akili kutafuta maisha.
 
81 Reactions
Reply
Back
Top Bottom