Mwanaume aliyempa talaka mke wake na kumuoa mfanyakazi wao wa ndani huko Zambia

Sasa kama ishu ni kuajiri mtu hamna sababu ya kuoa kwa kweli...

Tuendelee kustareheshana maana mke kuoa kwetu ist a norm na kusudi ni ili mleane pamoja na watoto. Umlishe umvishe nae awe sehemu ya msaada katika maisha yako akupikie, akuweke nadhifu na ahakikishe mji na watoto wako salama.

A wife should make a house to be a home for the head of the family and the off-springs. Kama hayawezi hayo basi mke hatoshi katika nafasi yake.
Yaani unasema wanaume gani wanaovisha wanawake, wakati sikuhizi kila jinsia inachakarika na kazi, mtoke wote kwenye kazi mke aanze na kuosha vyombo, sijui watoto na kupika wewe mwanaume una relax na kuperuzi JF eti kisa ni mke huo ka si utumwa kitu gani, maisha yenyewe mafupi haya kisa mwanaume Bora kila mtu achukue hamsini zake kwa kweli kwanza maisha haya na hela zangu na watoto kwanini niwe mtumwa wa mtu aisee,

Kuwa mwanamke Africa ni utumwa wallah eti mtu mzima mwenzako umulee kwani kawa mtoto, Mimi kwa kweli akafie huko mbele, badala niwaze wanangu na kupata mahela mengi nipumzike nimerudi nimechoka nianze kuhangaika na uwezo wa kuwa na mdada msaidizi ninao, Ila niteseke kumfuraisha mtu mzima mwenzangu never on earth
 
Wanaonaga kama wanasumbuliwa hivi...Ila kipindi cha uchumba hata kwao atatoroka kudadadeki mradi akuridhishe tu ufanye maamuzi ya kubeba jumla haraka.

Yani kokote utapotaka hata ubavuni mwa gari pakiwa na kagiza tu hamna wapitaji utapewa ushirikiano...Kimbembe ni ukishaoa sasa, hutaamini kama ndiye yule. Masharti kibao..sababu za ajabu mara hivi mara vile.
 
Yaani unasema wanaume gani wanaovisha wanawake, wakati sikuhizi kila jinsia inachakarika na kazi, mtoke wote kwenye kazi mke aanze na kuosha vyombo, sijui watoto na kupika wewe mwanaume una relax na kuperuzi JF eti kisa ni mke huo ka si utumwa kitu gani, maisha yenyewe mafupi haya kisa mwanaume Bora kila mtu achukue hamsini zake kwa kweli kwanza maisha haya na hela zangu na watoto kwanini niwe mtumwa wa mtu aisee,
Kuwa mwanamke afriica ni utumwa wallah eti mtu mzima mwenzako umulee kwani kawa mtoto, Mimi kwa kweli akafie huko mbele, badala niwaze wanangu na kupata mahela mengi nipumxike nimerudi nimechoka nianze kuhangaika na uwezo wa kuwa na mdada msaidizi ninao, Ila niteseke kumfuraisha mtu mzima mwenzangu never on earth
Imeisha hio, itoshe tu kusema sio lazima wote tuimbe. Wengine mtabaki kama mashabiki. Ndio kanuni za maisha.
 
Sasa huyu mtumishi naye akishazoea tu, ataanza kufanya yaleyale aliyokuwa anafanya huyu mtalikiwa
Hawezi kuwa na hiyo jeuri wakati kaona mwenzie katimuliwa. Tena ataishi kwa hofu sana juu ya hasira ya mumewe 😂!

Nadhani ushawahi kuona jinsi ambavyo watu wana behave mtu akifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu hata maofisini tu.
 
Very stupid
Na wanawake wasipendeze??? Akitaka kuweka kucha napo inawakera halafu mahawara zenu wote huko nje wanaweka makope wanafuga makucha...kisa umemuoa ndo umfanye kama ajuza for what??! Yani nyie wote mliopanik Mungu amewapa wake wa kuendana na nyie hao wanawake muwashike sana sana siku akikuponyoka ulie na usage meno, makamu wa rais anatimiza wajibu wake kwakuwa labda na mumewe anatimiza ya kwake..nilichokuwa nakitolea mfano ni nyie wanaume wa kulia lia kusaidiana majukumu na wake zenu habari za hela zikija ndo unajifanya kama wewe kuwa responsible huwezi., ndo mana nikauliza hapo juu huyo mwanaume anaemuacha mkewe kisa hafui yeye alikua amekamilika kwa lipi?? Majukumu yake yote anafanya?? Nikaenda mbali zaidi kuuliza kama hata huwa anakumbuka kumnunulia mkewe nguo za ndani au anadhani ni wajibu wa nani??
Ukiyafanya full responsibilities za mke huwezi kuwa na mda wa kutia tia makucha.
Pia mwanaume hawezi kuwa focused na maswala ya aina hio kama uko fully responsible as a mother of the family. Unamkirimu vyema na kumsikiliza mahitaji yake.

Tatizo lenu wanawake wa sikuhizi mnafikiri kuwa mke mbele ya mumeo its like unamfanyia favor! Too much EGO inawaponza and That stupidity ndio inaleta haya yote.
 
View attachment 1713163
View attachment 1713185
Mwanaume huyu toka jamii kutoka Ndola aliamua kumuacha mke wake waliyeoana miaka saba iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili. Mwanamke huyu alienda mahakamani ilikutafuta suluhu ya ndoa yake na maridhiano na mume wake, akiomba mahakama imsaidie kunusuru ndoa yake na kuongeza kuwa hajui kwanini mume wake aliamua kuchukua uamuzi wa kumuacha na kuoa mfanya kazi wao wa ndani.

- Mwanamke huyu aliiambia mahakama kuwa anampenda mume wake na haamini kama kweli ameamua kufanya kitu kama kile na kutaka kujua sababu zilizopelekea mume wake afanye hivyo.

- Mahakama ilipomuuliza mwanaume juu ya suala hilo alisema hawezi kubadili msimamo wake na hawezi kumuacha mke wake mpya wala hawezi kumrudia mke wake wa zamani maana maamzi yake ndio yalikuwa yameshafika mwisho na kushukuru kumpata mtu sahihi kwake na kusema mwanzo alifanya makosa kwenye kuchgua mke bila yeye kumjua mwanamke huyo vizuri.
Akaendelea kuaiambia mahakama kuwa mke wake huyo wa zamani alikuwa mzembe kupita kiasi, hakuweza hata kufanya kazi za ndani zinazomhusu kama mama wa familia na badala yake hata yale majukumu yake kwa mumewe aliyaacha mikononi mwa mfanyakazi wao wa ndani ambaye alijikuta kuwa ndio msaada mkubwa kwa mwanaume huyu , mfanyakazi wao wa ndani ndio aliyefua nguo zote za mwanaume huyo huku mke wake akiwa hana habari nae, hakutaka hata kukaa na kuongea na mume wake isipokuwa mfanyakazi wa ndani alikuwa akimuona amerudi toka kazini anampokea na kumuandalia maji ya kuoga, kisha anampa chakula na kukaa na kuongea nae sebuleni huku akimpa pole kwa uchovu na kumtia nguvu pindi anapoonekana kuchoka sana au kuwa na mawazo.

-Kuhusiana na suala hilo wazee walishawakalisha chini na ili kuwapatanisha bila mafanikio yeyote kwa wanandoa hao.

Alichokuwa akikifanya mwanamke huyu nyumbani ni kuwa bize kutoa maelekezo kwa mfanyakazi huyo wa ndani na kumfokea muda wote na kuwa bize na simu huku mfanya kazi wa ndani akiwa bize na mwanaume baba wa familia, hivyo niliona kila mtu abaki na kitu anachopenda kuwa bize nacho muda wote, mfanyakazi wa ndani anapenda kuwa bize na baba wa familia basi ni vyema awe nae aliatimize majukumu yake kwa baba wa familia vizuri, na mke wake kwa sababu yuko bize na simu basi nimuachie nafasi akae na kuchati kwa uhuru ili kila jambo liende sawa pia kwa upande wake.
Mume aliendelea kusema hata siku za mwisho wa juma (weekends) akiwa hayuko kazini mwanamke hakuona umuhimu wa kupika chakula kwa ajili ya mume wake kama alivyokuwa akifanya siku za mwanzo wa ndoa yao,badala yake alikuwa akifanya maandalizi ya kwenda kwenye sherehe za harusi na kamati za Kitchen Party, anarudi amelewa kitu ambacho mwanzo alikuwa hafanyi, na kama angekuwa anafanya nisingemuoa kabisa.

-Mume akaenda mbele zaidi na kuiomba mahakama iangalie kwa makini kucha ndefu za mwanamke huyo kama kweli zinaonesha mwanamke anayeweza kujishughulisha na shughuli za nyumbani kama mke wa mtu, muulizeni ana miaka mingapi hajawahi kupika chakula, kufanya kazi za nyumbani zaidi ya kuagiza, nani amekuwa akitandika kitanda changu kwa muda wa miezi nane sasa ?, Ni lini amejishughulisha hata kutunza na kuangalia watoto kama kweli ni mwanamke anayefaa kuwa mke, hayo yote mfanyakazi wa ndani ambaye ni mke wangu sasa ndio amekuwa akiyafanya siku zote.

Baada ya mahakama kujiridhisha na maneno ya mume ikatengua ndoa hiyo ili sasa mwanamke aendelee kuchat bila kikomo, ahudhurie sherehe za fungate, harusi na kufuga kucha huku mfanyakazi wa ndani akiwa boss ndani ya nyumba mwenye kujua na kujali majukumu yake kwa undani.

Wanaweke wengi huyajua makosa yao na ukimya wa mwanaume humfanya ayaendeleze bila kujua mwanaume muda mwingine yuko kimya akiwaza hatima ya jambo hilo na mwisho anaweza kuja na uamzi mwingine

Kuna la kujifunza.
Huyo demu wa chini ni demu wa kichaga.Picha yake inatumiwa kimakosa kaenda polisi kuripoti.mcheki insta @official_april_16.
 
sawa naweza kuajiri mtu wa kufanya hayo yote, Sasa wewe kazi yako au majukum yako kwangu yanakuwa yapi? Yani Nini umuhimu wako kwangu wewe km mke as long as hata kuzaa naweza kutafuta wa kunizalia Kama walivyofanya Kim na Kanye West
 
Huyo mume anahitaji dish washer, washing machine, smart-kitchen!, si aseme tu kafuata hilo guu, hakuna masufuria, ugali katika law of attraction!!! Asimbambikizie tope mke wake wa zamani, kuachwa kunauma ila to be told you are responsible for such a mess is soo UNFAIR
Kwani ndoa lengo ni nini ? Nyote muwe sawa au mmoja awe chini ya mwenzake ?

Piki, mwanamke yake nyumba na kuihudumia nyumba, na vilivyomo.
 
Wanaume hawana shukrani hata ujitume vipi ku cheat kuko pale pale tu na ka amenichoka heri aniache sio kutafUta excuse sijui dada wa kazi na blah blah
Hivi kwa akili ya kawaida sababu za mdau alizo muacha kwazo mkewe si za msingi ?
 
Back
Top Bottom