Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Kwanza kulikuwa na kauli kwamba "Zitto akirudi auwawe kwa usaliti"
Halafu ikaja kauli nyingine, "serikali isitangaze watu wanaokufa kwa Corona virus, tutangaze wale waliopona tu"
Mwingine akasema :Corona ni sawa na wapinzani"
Wengi wetu tulikimbilia kutoa shutuma na kulaumu sana wanasiasa waliotoa kauli hizi, na kuziita za kipumbavu.
Wapo wanasiasa wanatoa kauli za kipumbavu sana kwa kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, lakini pia wapo wanasiasa wanaotoa kauli za kipumbavu sana kwa kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana. Wale wa kundi la kwanza mara zote wanatoa kauli za kipumbavu. Hawa wa kundi la pili huwa si mara zote wanatoa kauli za kipumbavu
Je umejiuliza kwamba tunapohukumu mwanasiasa kutoa kauli ya kipumbavu, huenda wapumbavu ni sisi ambao hatuchukui muda kutafakari kwa nini kauli hizi zilitolewa? Je tulijiuliza lengo wanasiasa kutoa kauli hizi lilikuwa ni nini? Lakini twapaswa kuwa makini pia kuona kwamba kauli nyingine za kipumbavu ni upumbavu kwa sababu kuna historia ya upumbavu.