Mwanasiasa mzoefu anapotoa kauli ya kipumbavu usifanye haraka kuitafsiri na kumhukumu

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,563
Kwanza kulikuwa na kauli kwamba "Zitto akirudi auwawe kwa usaliti"

Halafu ikaja kauli nyingine, "serikali isitangaze watu wanaokufa kwa Corona virus, tutangaze wale waliopona tu"

Mwingine akasema :Corona ni sawa na wapinzani"

Wengi wetu tulikimbilia kutoa shutuma na kulaumu sana wanasiasa waliotoa kauli hizi, na kuziita za kipumbavu.

Wapo wanasiasa wanatoa kauli za kipumbavu sana kwa kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana, lakini pia wapo wanasiasa wanaotoa kauli za kipumbavu sana kwa kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana. Wale wa kundi la kwanza mara zote wanatoa kauli za kipumbavu. Hawa wa kundi la pili huwa si mara zote wanatoa kauli za kipumbavu

Je umejiuliza kwamba tunapohukumu mwanasiasa kutoa kauli ya kipumbavu, huenda wapumbavu ni sisi ambao hatuchukui muda kutafakari kwa nini kauli hizi zilitolewa? Je tulijiuliza lengo wanasiasa kutoa kauli hizi lilikuwa ni nini? Lakini twapaswa kuwa makini pia kuona kwamba kauli nyingine za kipumbavu ni upumbavu kwa sababu kuna historia ya upumbavu.
 
ulishawahi kujiuliza pia lengo la zitto kuzusha kuwa mr president is dead na akamuweka yule mama kukagua gwaride?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sisi wengine tulielewa kwamba kuna mpango ambao ZIto alishaupanga akiwa siyo peke yake labda na kwa msaada wa watu wengine ndani na nje àkiamini uneshafanikiwa kwa aslimia 100. Ndiyo maama akatoa ile picha kwa majivuno na kiburi kile.
 
Sisi wengine tulielewa kwamba kuna mpango ambao ZIto alishaupanga akiwa siyo peke yake labda na kwa msaada wa watu wengine ndani na nje àkiamini uneshafanikiwa kwa aslimia 100. Ndiyo maama akatoa ile picha kwa majivuno na kiburi kile.
Mmmh, interesting. Kwa hiyo tukichukua parallel, mtu akisema serikali isitangaze wanaokufa kwa Coronavirus ni kwamba anatoa ujumbe kuwa serikali haitangazi wanaokufa kwa virus?
 
Hii thread inalalamikia jambo? Uwezo wako wa kusoma ukaelewa ni mdogo sana, unajidhihirisha wazi.
Sasa hayo mashairi yako uliyo yaandika ulikuwa unafikiri Ni nini mjinga siku zote hujiona mwerevu na husema angalia uwezo wako mdogo sana
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom