Mwanasiasa gani amekushangaza 2015-2017

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,182
1,490
Habari wakuu kama Kichwa cha Habari kinavyojieleza hapo juu ni mwanasiasa gani aliyekushangaza zaidi kuanzia mwaka wa uchaguzi mkuu mpaka leo kwa ndani ya Nchi yetu lakini hata kwa Nje ya Nchi yetu pia itakuwa sawa

Mimi wakwangu kwa ndani ya Nchi ni LIPUMBA
na kwa Nje ya Nchi ni Trump

-Lipumba kwa namna alivyokuwa na maisha ya kujivunjia heshima tena akiwa kama Profesa

-Trump kanishangaza kwa kumuacha Korea Kaskazini bila kumpiga mpaka leo wakati sababu alikuwanazo zote!

Naomba kuwasilisha
 
Edward lowassa

Kuingia ukawa asubuhi, jion kupewa dhamana ya kupeperusha bendera ya kugombea urais

Tena kaingia kwa watu waliomtusi miaka 8 mfululizo
magufuli kwa kuligawanya taifa na kuona upinzani km uadui//// kuleta njaa na kudidimiza uchumi................na magumashi meengi km yale ya kutuaminisha anapmbana na ufisadi kupandikiza chuki miongoni mwa watz...............................
 
aliyenishangaza ni jamaa mmoja aliyedundwa gongo sijui lilikuwa la kichwani au la mgongoni na mpinzani wake ndani ya chama chao hadi kuzimia

aliyempiga akapeta kinoma lakini afya yake ikazingua sana mpaka yule aliyepigwa akapewa ukuu wa wilaya ndo mpigaji akapata nafuu na kupona.

nilishangaa sana
 
Mie Kanishangaza Sana Mbunge Msomi wa Arumeru Mashariki Ndg Joshua Nassari kwny Mkutano wa Bunge la Bajeti kutumia Nafasi adimu ya kuongelea Matatizo ya Wananchi wake yeye akawa bize kuzungumzia Nyanya na Mboga Mboga zilizoharibiwa Shambani kwa Mbowe
 
Back
Top Bottom