Mwanasheria mkuu wa zanzibar asesema ukweli leo kuwa hakuna muungano adai yakuwa muungano upo tu kama kiini macho lakini kiuhalisia muungano haupo hilo kalisema leo katika semina ambayo inaendelea muda huu kwa waheshimiwa wawakilishi wa baraza la mapinduzi zanzibar. Tizameni ZBC ni live muda huu. Baadhi ya waheshimiwa wawakilishi wamekwisha changia ambao ni Raza, Mshimba Vuai Nahodha na Jussa ikihuacha Vuai wengine wanataka kesho watangaze mgogoro wa muunganoBaadhi ya mambo ambayo mwanasheria kazungumzia ni kuhusu ushikishwaji wa upande wa zanzibar katika mambo ya muungano kuwa ni kiini macho, akaunti ya pamoja toka ipitishwe mwaka 1996 hadi leo hakuna account hiyo wala utekelezaji wake, Raisi wa jamuhuru kumteua waziri mkuu bila kushauriana na makamu wa rais, pia kuwateuwa mawaziri bila kushauriana na makamu wa raisi, raisi wa muungano kuwa na kinga ya kutokushtakiwa kwa upande mmoja kwa kuwa mambo ya uhaini sio ya muungano na mengine mengi. Wanajamii Kila mtu kamsifu mwanasheria kwa kusema ukweli jana Mzee Hassani moyo alisema viongozi wa zanzibar miaka ya sasa ni waoga na wako kimaslai zaidi