Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu, ameshindwa kumshauri 'kisheria/kikatiba' Rais Samia S Hassan

Kwanza, wakati Mama Samia anatangaza kifo cha Hayati JPM, alitangaza siku 14 za maombolezo ilihali kwenye katiba zinatajwa siku 21. Baadae Katibu Mwenezi CCM ndg Polepole akatangaza siku 21 kwa niaba ya chama 'MKANGANYIKO'. Wananchi walihoji kwanini Makam alitangaza siku 14 badala ya 21 'Mwanasheria' hakuliona hili.

Pili, mara tu baada ya kuapa na kutoa hotuba fupi, taarifa iliyotolewa ni kwamba Rais anaenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Baadae TLS wakatoa mwongozo wa kikatiba na kisheria kuhusu Baraza hilo kuwa kwasasa 'halipo'. Mwanasheria Mkuu na wanasheria wengine wa serikali mlikuwa wapi? Mbona hamjasema chochote? Washauri wa Rais mnamsaidiaje Rais?

Pia soma

Wakati mwingine ndiyo maana tunaamini taarifa za mitandaoni kuliko za serikali
CHADEMA ndio walikuwa wa kwanza kutangaza maombolezo ya siku 21ya kifo Raisi na CCM Wakafuata baadaye
 
Kuna watu wengine hata ukiangalia muonekano wa vichwa vyao tu unapata picha ya kilichomo ndani ya kichwa hicho.
 
Back
Top Bottom