Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajiuzulu, ameshindwa kumshauri 'kisheria/kikatiba' Rais Samia S Hassan

Watu watatu 3 hawa;

1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, nafikili anaitwa Kilangi

2. DPP

3. Solicitor General - Gabriel Malata.

Hawa watu walichangia sana kuminya haki za Watanzania.
Tuzidi kumuombea mama Samia awaondoe kabisa hawa watu
 
Inatakiwa kwenye ofisi zoote tangu alipoapishwa Samia kuwe na picha yake Mh. Rais Samia.

Lakini naona kwenye kitengo cha Protocol kuna shida mahali; Samia kupewa pen nyeusi badala ya nyekundu, kuendelea kuonekana picha ya JPM wakati tuna Rais mpya n.k
Huyo mwanasheria ni bomu kabisa
 
Mwigulu Nchemba Wajibu TLS:
Nimesoma andiko la TLS, kwa heshima zote kwa chombo chetu hiki kilichopewa mamlaka kisheria, Nimeshtuka sana, I wish to say,

Kwanza KATIBA HAIJAVUNJWA KWA MHE RAIS SAMIA SULUHU kuapa, na wala hakuna Mkanganyiko wowote wa Kikatiba, kwa yeye kutoteua PM na Baraza jipya. Mmekaa wote kweli mkaona hivyo!
Kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 42(5) kuna watu wa aina mbili wanaweza kuwa Rais. Moja, Rais Mteule ambaye anatokana na Ibara ya 42(1). Mbili, Mtu anayeshika kiti cha Rais ambaye anatokana na ibara ya 37(5) na 50(2)(d) ambaye ni Makamu wa Rais. Kwa Mazingira haya, Makamu wa Rais, baada ya kifo cha Rais, anakuwa Kaimu Rais baadae ndio ameapa na kuwa RAIS wa Nchi. Rais Mteule anapatikana kutokana na uchaguzi. Hivyo basi ibara ya 57(2)(f) ya Katiba haitumiki katika mazingira haya. Kwa mjibu wa Sheria, Mhe Rais alitakiwa kutoa taarifa hii kwenye Baraza la Mawaziri baada ya kuapa na alifanya hivyo, maana yake Baraza lipo.

Hata hivyo kwa tamaduni za Kiafrika, kitanzania na Misingi ya UTU, SIONI KAMA NI JAMBO JEMA SANA KUANZA KUJADILI MGAWANYO WA MADARAKA TUNGALI HATA HATUJAMZIKA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU. HUU SIO MSIBA MDOGO, JAMBO HILI ZITO LIKO MIKONONI MWA RAIS WETU MAMA SAMIA SULUHU, HALAFU SISI TUANZE KUMPATIA MAMBO YA MARA TEUA PM, MARA VUNJA BARAZA, KATIBA INAELEKEZA RAIS KUAPA NA NAMNA YA KUMPATA MAKAMU WA RAIS.

KWA MJIBU WA KATIBA RAIS ANARUHUSIWA KUVUNJA BARAZA MUDA WOWOTE NA KUPANGA ATAKAVYO HATA SIO KWA MAZINGIRA KUAPA KWAKE,

KWANINI HATUIONI HEKIMA YAKE YA KUSHUGHULIKIA MSIBA KUMSITIRI KWANZA ALIYEKUWA KIONGOZI WETU? TUNAANZA NA MAZISHI AU MIRATHI? 😭😭😭😭

Hawa ndio walimzunguka bwana yule!! Enzi hizo kila kitu cha sheria walikuwa wanakandamizia kwa Lissu. Lissu akisema kulia geuka wote kuanzia mkuu wao wakitii na waligeuka.
 
katika mambo ya kupigania kurekebisha katika katiba ni kama haya yanayoleta mkanganyiko sasa siyo mnalalamikia tu mambo mengine yasiyo na msingi hebu angalia katiba inasema baada ya kuapa ataliongoza balaza la mawaziri tls wanasema halipo sasa kipi ni kipi ataongozaje balaza ambalo kwamujibu wa tls halipo katiba haikutoa maelezo yanayojitosheleza
 
Inawezekana sie tuna sema samia kakosea kumbe rais alikufa kabla ya yar 17 labda ndio maana samia akasema maombolezo iwe siku 14 tu maana yake alikufa mapema
 
Walushazoea kuvunja sheria za nchi, ilishakuwa kawaida kwa utawala wa jiwe kukanyaga sheria.

Pili, mazingira ya kutangaza kifo hayakuwa rafiki kufanya mashauriano na Mwanasheria. Tangazo lilirekodiwa Tanga likatumwa TBC.

Mfumo na wenye Chama walikuwa hawataki kutangaza kifo, mtifuano ulikuwa unaendelea ndani kwa ndani kuhakikisha Mama Samia haapishwi kuwa Rais. Mama ni km aliwafanyia surprise.

Lilikuwa tangazo la kibabe.
Walitaka kumdhuluma mama haki yake! Kwa ufupi ma-CCM ni mapumbavu! Nasikia jeshi liliwapa masaa vinginevyo lingetangaza Rais wake, TISS na Ma-ccm yakanywea! Pumbavu kabisa! Mama ayapige chino yote yaliyoteuliwa na Magu aanze upya! Mbona miaka mitano ni mingi hii?
 
Yote haya ni shauri ya Jiwe! Mzee alikuwa inagawa vyeo kindugu, maana huyu wanatoka mkoa mmoja na ni jamaa yake wa karibu sana! Mama atafute mtu sahihi! Amweke hata huyo Rais wa TLS atamsaidia sana!
Acha uongo hakuna chembe ya ukaribu wala kabila. Mzushi wewe.
 
Walitaka kumdhuluma mama haki yake! Kwa ufupi ma-CCM ni mapumbavu! Nasikia jeshi liliwapa masaa vinginevyo lingetangaza Rais wake, TISS na Ma-ccm yakanywea! Pumbavu kabisa! Mama ayapige chino yote yaliyoteuliwa na Magu aanze upya! Mbona miaka mitano ni mingi hii?
Acha uongo wa kupindukia! Ndiyo maana ikatungwa sheria kwa watu kama ninyi na usidhani avatasr inakuficha. Kama unamtegemea Mello, hawezi kutetea.
 
Fuatilia vizuri, viongozi wengi wa serikali huwa hawajui sheria wala katiba kwa upana wake,na wenye wajibu wa kisheria hufanya kuendana na mdundo wa kiongozi. wakati wa Magufuli ilikuwa ni rahisi sana kuongoza maana alikuwa hafuati sheria, bali alikuwa anatumia njia aliyooita nia njema ikiongozwa na uzalendo, hivyo mwanasheria Mkuu wa serikali, majaji, mahakimu na wengine walikuwa wanatekeleza sheria sio kama zilivyo, bali alivyokuwa anataka Magufuli. Sasa inaonekana bado mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu na wengineo bado wako kwenye hangover ya utawala wa Magufuli.
Ushahidi!
 
Wewe ni wa ajabu kabisa !Taifa la Tanzania lilipata Kiongozi Rais JPM ambaye alijitambua na akawa zaidi upande wa wananchi walio wengi na akajitofautisha na Watangulizi wake tukimuondoa Mwl JK Nyerere.

Ukombozi kamili wa Watanzania wengi utapatikana kama watanzania ambao pia ni wengi maskini walio katika vyombo vya ulinzi na Usalama/ Majeshi yetu watajitambua na kuacha kutumiwa na baadhi ya wanasiasa ndivyo sivyo.

Wanasiasa wanaringia hayo Majeshi hawana lolote lengine, pasipo kushikwa mkono na wajeda wa nyanja zote hawana jeuri yeyote.

Wànajeshi na vyombo vya ulinzi na usalama wakikataa kwa kumaanisha maadili ya hovyo ya baadhi ya wanasisa pasi shaka wanasiasa hao watafuata mstariiii nyookaaà.
Kama unataka kuona uzuri wa jeshi andalia Ugana, Congio, Nyamar (Burma), Burundi, na Libya! Hiyo nafasi ya kuandika humu hutaipata maana internet zitafungwa. Tuone kama utasimama Kariakoo kuropoka unayoropoka.
 
Kwanza, wakati Mama Samia anatangaza kifo cha Hayati JPM, alitangaza siku 14 za maombolezo ilihali kwenye katiba zinatajwa siku 21. Baadae Katibu Mwenezi CCM ndg Polepole akatangaza siku 21 kwa niaba ya chama 'MKANGANYIKO'. Wananchi walihoji kwanini Makam alitangaza siku 14 badala ya 21 'Mwanasheria' hakuliona hili.

Pili, mara tu baada ya kuapa na kutoa hotuba fupi, taarifa iliyotolewa ni kwamba Rais anaenda kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri.

Baadae TLS wakatoa mwongozo wa kikatiba na kisheria kuhusu Baraza hilo kuwa kwasasa 'halipo'. Mwanasheria Mkuu na wanasheria wengine wa serikali mlikuwa wapi? Mbona hamjasema chochote? Washauri wa Rais mnamsaidiaje Rais?

Pia soma

Wakati mwingine ndiyo maana tunaamini taarifa za mitandaoni kuliko za serikali
Tusubiri tumzike baba,ndipo tuliamshe dude
 
Kama unataka kuona uzuri wa jeshi andalia Ugana, Congio, Nyamar (Burma), Burundi, na Libya! Hiyo nafasi ya kuandika humu hutaipata maana internet zitafungwa. Tuone kama utasimama Kariakoo kuropoka unayoropoka.
Hiyo simu yako ina-scratch etiii
 
Back
Top Bottom