Mwanasheria Mkuu amekerwa na kauli ya Balozi wa Uswisi juu ya "Mabilioni ya Uswisi"

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,463
3,212
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amekerwa na kauli ya Balozi wa Uswisi nchini Olivier Chave, aliyesema kuwa Serikali ya Tanzania haijaonyesha nia ya dhati kutaka kuchunguza na kupata ukweli wa mabilioni yafedha yaliyofichwa nchini humo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na
Mwananchi Jumamosi katikati ya wiki hii, Werema, alitaja hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu suala hilo kuwa ni kuwasiliana na mamlaka husika nchini Uswisi na kuundwa kwa kamati maalumu ya kufuatilia suala hilo.

Jaji Werema alisema kuwa hawezi kumjibu
chochote balozi huyo kwa kuwa ni mtu mdogo
kwake. “Najua kuwa huyu balozi ana kinga, ila siyo adabu hata kidogo kuzungumza maneno yale kwenye nchi ya watu. Kama ingekuwa ni balozi wa Tanzania huko Uswisi kasema maneno haya, angeambiwa tu arudi nyumbani kupumzika hadi watakapomhitaji,” alisema Werema.

Januari 11, mwaka huu, Balozi Chave aliliambia gazeti hili katika maojiano maalumu kuwa hadi sasa hakuna jitihada zozote zilizofanywa na Serikali ya Tanzania kutaka ufumbuzi wa tuhuma za watu walioficha fedha nchini humo.

Katika ufafanuzi wake, Werema alisema kwamba tayari timu iliyoundwa imeshafanya kikao cha kwanza Januari 9, mwaka huu na sasa inaendelea kutekeleza majukumu iliyopewa.

Alifafanua kuwa timu hiyo iliundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya kupata kibali cha Rais Jakaya Kikwete na itafanya kazi zake kwa usiri mkubwa kutokana na unyeti wa suala hilo.

Werema alieleza kuwa hadi kufikia Aprili mwaka
huu, watakuwa na jambo la kueleza umma
kutokana na uchunguzi huo.
“Suala hili ni nyeti, ndiyo maana unaona sisi wengine tumefunga midomo yetu. Tunafanya kazi kama Chui na Simba, huku hakuna Kambale wala nini,” alisema na kuongeza:
“Kazi iliyo mbele yetu ni ngumu, tunafanya kazi hii na benki zinazofanya shughuli zake kwa usiri mkubwa, ingekuwa zipo huku kwetu hizi fedha tungezipata, kwa hiyo Watanzania watuombee tuimalize kazi hii vizuri.”

Alibainisha kuwa, watakuwa na vikao vingi ikiwamo cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na
usalama, ili kujadili suala hilo na kuangalia namna ya kulikamilisha.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi la leo
 
Kamati ya kazi gani kwenye hili? Kama Zito kawatafunia kwa 90% wao wanataka nini tena. Tena cha ajabu wamekimbilia kukwea ndege kwenda uswis wakati hata hawajaenda kumwona zito kupata ushahidi alionao. Wadau si mmewasiki wakisema watakua na vikao vingi mpaka mwezi April, kaazi ipo
 
Jaji hajui tofauti ya kutoonyesha nia na kutofanya kitu. Unaweza ukafanya mengi tu lakini huna nia thabiti
 
Huhitaji kuuliza Tanzania ni nchi yenye uongozi wa namna gani unapokuta watu kama Werema ni Mwanasheria Mkuu akitoa kauli kama hizi.

Werema ni nafasi nzuri ya JK kuambiwa show me your Attorney General and I will tell you what kind of president you are.
 
Back
Top Bottom