Mwanasheria atekwa, apigwa, aachwa porini

Status
Not open for further replies.
Dah...bonge la muvi sijui litaishaje yaani jamaa ukiwa tofauti nao tu wanakumabwepande yetu macho.............
 
Nahisi kuna agenda ya siri vile! Anataka tuamini kwamba Mwanasheria amepigwa na watu wenye hasira ya kupoteza nyumba zao hivyo na Dr. Ulimboka alitekwa na watu wenye hasira ya kupoteza ndugu zao. Nahisi haya ndo mazingira yanayojengwa!!!
Ni vizuri kuwaza, ila usipoteze logic. Yanawezekana wala yasiwe na uhusiano na Dr. Uli. Yale mamia ya mamilioni si kila mtu anaweza kuyapata tena, wengine ndio zilikua nyumba zao hizo hizo... ! Tuwe reasonable at times katika kuargue. Pole Dr. Uli, Pole Heche
 
SAKATA la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa kufichua siri ya uhalifu.

Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.

Huyu mtekaji sasa atakuwa ametoka KOSSOVO na anaweza kwenda kutubu kwenye Makanisa ya Kenya na Polisi wa Kenya watamkamata na kumleta kwa afande Kova
 
Tunakoelekea ni kubaya, ukisema kweli na kusimama katika kweli TZ maisha yako yanakuwa hatarini, Please God intervene!
Mkuu, Mungu anasema "Jisaidie nami Nitakusaidia". Kila kitu sio lazima Mungu aingilie. Kuna mengine yako ndani ya uwezo wa binadamu.
 
Kubomowa sawa kama wamejenge sehemu ambazo haziruhusiwi kisheria.

But wale waliowapatia HATI za UJENZI wamechukuliwa hatua gani?

Na kama kweli wana hati HALALI ZA UJENZI from the same Govt basi inabidi walipwe fidia kabla ya kubomolewa.

Serikali isicheze double stds lazima iingie gharama kwa UZEMBE uliofanya na watendaji wake.

Waache wapigwe na ikibidi wafe kwa kuwatia umaskini wenzao mpaka nyumba inasimama walikuwa wapi kama wameweza kuwavunjia hata kuwazuia kujenga wangeweza wanasubiri pesa za watu zipotee ndiyo wajue sehemu hairuhusiwi,Mkurugenzi, Afisa Afya na kinara wao AFISA ARDHI kwa nini wasikatwe vichwa kwa upuuzi huu? Tumechoka kupewa umasikini wakulazimishwa kwa ujinga wa watu wachache ambao hawachukuliwi hatua zozote hivi ingelikuwa anayetoa kibali cha ujenzi na hati miliki katika maeneo ysiyoruhusiwa ndiye anatakiwa kulipa gharama ya hasara inayotokana na maamuzi yake ya kijinga nani angejenga ufukweni? Acheni kuonea watu
 
Nadhani wewe utakua wa kwanza kuisadia idara ya upelelezi kuhusu hili,ni vema watu wote tuheshimu na kutii mamlaka, sio kukimbilia kuteka na kupiga watumishi tena wataalam wetu huu ni ujinga na upuuzi wa kizamani sana..killing our own professionals simply means we are a dead Nation, we cannot move an inch without technical personnel ambao tunawateka na kuwapiga...mtu mwenye akili timamu atafata taratibu zote including kununua kiwanja halali sio kujenga mtoni, atapata hati halali na kupewa building permint aanze ujenzi wake halali, sasa ww unatetea watu waojenga kwenye mito halafu unashabikia watumishi wa serikli kupigwa..akili zako ndogo sana kabisa..pole sana Heche Mungu atakusaidia wewe ni kamanda Bora ukaifia nchi yako...

Heche anakuwa mbuzi wakafara kwa makosa ya watu wengine swali langu kwako wewe unayita wenzako wana akili ndogo ukidhani wewe unazo nyingi wakati nyumba zinajengwa Serikali ilikuwa likizo? Kama serikali imeweza kuzibomoa ni ukweli usiopingika kuwa ilikuwa na uwezo pia wa kuzuia ujenzi katika eneo hilo kwa nini wamewasubiri wamalize ndipo wawabomolee je, nani alitoa kibali cha ujenzi Afisa ardhi amechukuliwa hatua gani? Mkurugenzi naye amefanywa nini kwa uzembe unaosababbisha watu waichukie serikali yao? Kama huna majibu ya maswali hayo wewe ndiyo huna akili kuliko huyo anayesema bora wapigwe. Wamachinga wamekuwa wakipewa leseni na kujenga vibanda mahali pasipostahili baada ya muda serikali hiyohiyo huja kuwavunjia kwa madai maeneo hayaruhusiwi bila kuchunguza wala kutaka kujua mjenzi alipata kibali kwa nani na huyo aliyetoka kibali hana ramani ya mji huo kuwa eneo hilo linatakiwa kujengwa au la! Fahamu raia ana imani na watumishi wa Serikali hivyo wanachokisema kwa dhamana zao huaminika na jamii sasa ikiwa jamii inadanganywa na watumishi wa umma ni nani atakayewaelekeza wananchi maeneo halali na yasiyo halali kujengwa? Usiwe mwepesi kuhukumu wenzako hawana akili wakati wewe ndiyo huna akili za kufikiri kwa kina na kujua chimbuko la tatizo liwapi badala yake unalaumu aliyepewa kiwanja mlilie aliyetoa kiwanja na kibali cha ujenzi kwa kuwa yeye ndiye mwenye dhamana ya kulifahamu eneo husika na kumwelimisha mwananchi.
 
Baada ya tukio la Dkt. Ulimboka tuliona wachangiaji wengi wakishabikia tuko lile, na wengine tukaonya kuwa leo wengine wanashabikia bila kuangalia undani. Utekaji unazidi kuongezeka siku baada ya siku, watu wenye nia mbaya na wanaopenda njia fupi kujipatia maslahi wataendelea kutumia fursa hii wakati sisi tunazidi kutoa hukumu bila uchunguzi wa kina kubaini wahusika wa wakweli wa mauaji na utekaji. Tutakaa nao baa, tutakula nao na kuongea nao hukumu tunazotoa kwa watu au taasisi nyingine wakati wao wanazidi kujineemesha kwa ujinga wetu.

Ni wakati sasa wa kuacha vyombo husika kufanya uchunguzi wao ili kujua ukweli, endapo majibu hayatatolewa au hayataridhisha basi tuhoji matokeo na siyo kuhukumu.
 
Au serikali inataka kutupiga Changa la Macho. Picha za aliyepigwa na alipotibiwa au anapotibiwa zipo?
 
sakata la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za dar es salaam limechukua sura mpya baada ya waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais, mazingira, dk terezya huvisa kufichua siri ya uhalifu.

Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia mwanasheria wa baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (nemc), heche manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.
wanakigamboni mpooooooooooo! Hiyo ndo agenda inayokuja kwenu hakuna cha mji mpya wala nini wanataka beach mabwana zao wanazitaka...zimeshauzwa......kaeni mkao wa kula kigamboni ...mtajuta kuichagua ccm.
 
Nchi sasa ina organized criminals who must be apprehended by the state machineries in order to restore confidence to the sitting government.
 
wasubiri mtuhumiwa safari hii ataenda kutubu kwa rwakatare, M-B na atakua msudan kus, mabwepande-part 2....star covu
 
katekwa na usalama huyo ili kuneutralize saga ya ulimboka ionekane naye alitekwa kwa sababu za visasi
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom