Mwanasheria atekwa, apigwa, aachwa porini

Mwanasheria atekwa, apigwa, aachwa porini

Status
Not open for further replies.

Babb-Babbjrtz

Member
Joined
Feb 13, 2012
Posts
57
Reaction score
7
SAKATA la ubomoaji majumba ya kifahari yaliyojengwa katika fukwe za Dar es Salaam limechukua sura mpya baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa kufichua siri ya uhalifu.

Waziri amesema mbali na yeye kutishwa kuuawa, pia Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Heche Manchare ametekwa na watu wasiojulikana wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na kumpiga kisha kumtelekeza eneo ambalo hakulitaja.
 
Riwaya mpya imeanza!! Polisi "muhusika mkuu" sijui tukimbilie wapi!!
 
Gazeti la habari leo limeandika kwamba Mwanasheria wa NEMC bwana Manchare Heche ametekwa na kupigwana watu wasiojulikana..itakumbukwa Nemc iliendesha zoezi la kubomoa majengo yaliyojengwa kinyume cha sheria hivi karibuni, na hilolinahusishwa na kipigo hicho..
 
Wito wangu kwa Serikali, ichukue hatua katika masuala ya msingi ya Kitaifa kama haya..hii hali haikubaliki hata kidogo, kundi la watu lina mtisha mpaka waziri sasa tunasemaje kuhusu serikali isiyoweza kuzuia upuuzi kama huu
 
You guyz(government) are dead sleaping while people are constructing,once they finish and dwelln nyie mnakuja 4 demolition,na bado,mtatupwa sana mambwePwande huko. Huo ni uonevu.
 
Sasa ni dhahiri kbs ya kwamba serikali ya jk ni DHAIFU full.

Ngoja tuwasikilizie wanachotaka kufanya!
 
Nahisi kuna agenda ya siri vile! Anataka tuamini kwamba Mwanasheria amepigwa na watu wenye hasira ya kupoteza nyumba zao hivyo na Dr. Ulimboka alitekwa na watu wenye hasira ya kupoteza ndugu zao. Nahisi haya ndo mazingira yanayojengwa!!!
 
QUOTE=Somoche;4253993]Wito wangu kwa Serikali, ichukue hatua katika masuala ya msingi ya Kitaifa kama haya..hii hali haikubaliki hata kidogo, kundi la watu lina mtisha mpaka waziri sasa tunasemaje kuhusu serikali isiyoweza kuzuia upuuzi kama huu[/QUOTE]

Huu ni Upepo tu- Baba Mwa'asha.
 
Kubomowa sawa kama wamejenge sehemu ambazo haziruhusiwi kisheria.

But wale waliowapatia HATI za UJENZI wamechukuliwa hatua gani?

Na kama kweli wana hati HALALI ZA UJENZI from the same Govt basi inabidi walipwe fidia kabla ya kubomolewa.

Serikali isicheze double stds lazima iingie gharama kwa UZEMBE uliofanya na watendaji wake.
 
You guyz(government) are dead sleaping while people are constructing,once they finish and dwelln nyie mnakuja 4 demolition,na bado,mtatupwa sana mambwePwande huko. Huo ni uonevu.

Nadhani wewe utakua wa kwanza kuisadia idara ya upelelezi kuhusu hili,ni vema watu wote tuheshimu na kutii mamlaka, sio kukimbilia kuteka na kupiga watumishi tena wataalam wetu huu ni ujinga na upuuzi wa kizamani sana..killing our own professionals simply means we are a dead Nation, we cannot move an inch without technical personnel ambao tunawateka na kuwapiga...mtu mwenye akili timamu atafata taratibu zote including kununua kiwanja halali sio kujenga mtoni, atapata hati halali na kupewa building permint aanze ujenzi wake halali, sasa ww unatetea watu waojenga kwenye mito halafu unashabikia watumishi wa serikli kupigwa..akili zako ndogo sana kabisa..pole sana Heche Mungu atakusaidia wewe ni kamanda Bora ukaifia nchi yako...
 
Tunakoelekea ni kubaya, ukisema kweli na kusimama katika kweli TZ maisha yako yanakuwa hatarini, Please God intervene!
 
CCM wanaamini haya yanayotokea ni kwaajili ya wapinzani tu! Lakini hizi damu hazitaishia kwa wapinzani.

Hao wanaotekeleza haya wanaweza kufanya hata kwa wana CCM wanaodhani wako salama! yetu macho na endeleeni kushabikia nchi inavyoharibika mkidhani inawaharibikia Chadema na wanaharakati!
 
Sitegemei kuona nilichokiona kwa Nyerere siku rais Mkapa au jK akifa. Labda Mwinyi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom