Paul Alex
JF-Expert Member
- Jul 14, 2012
- 4,342
- 9,824
Wakati Serikali ya Rais John Magufuli ikiendelea kutoa maagizo katika taasisi na vitengo mbalimbali ili kuboresha utendaji, baadhi ya maagizo hayo yameanza kupingwa mahakamani.
Miongoni mwa maagizo hayo ni yale yanayolenga kupambana na ukwepaji kodi na kubomoa nyumba na majengo yaliyojengwa kinyume na taratibu.
Ubomoaji wa nyumba zilizojengwa mabondeni, kwenye kingo za mito na fukwe chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), umesitishwa kwa amri ya Mahakama baada ya wananchi kulalamikia kutopewa makazi mbadala.
Agizo jingine lililolalamikiwa ni lile la Rais Magufuli kwa watumishi wa Hazina la kuwataka wakusanye kodi bila kuangalia sura ambalo limelalamikiwa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwamba utekelezaji wake unawalenga wafadhili wa Chadema kwa kuwatoza kodi kubwa kuwakomoa. TRA imepinga madai hayo ikisema inafuata sheria.
Mbali na hilo, Chama cha Mawakala wa Forodha (Taffa), nacho kimefungua kesi Mahakama Kuu, kupinga hatua ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuwadai fedha za tozo ambazo kinadai kimeshailipa.
Wiki iliyopita, TPA ilizitaka taasisi 284 kuwasilisha nyaraka za malipo ya tozo za mwaka 2014 ili kuthibitisha iwapo wamelipa.
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) nalo pia limeomba Serikali itoe ufafanuzi kuhusu misamaha ya kodi kwa taasisi za dini ili kuondoa changamoto zinazoweza kusababisha upendeleo.
Ombi hilo lilikuja baada ya TRA kuliandikia barua Baraza hilo kabla ya kutoa msamaha wa gari. Bakwata ilisema kama utaratibu wa kudai taarifa za matumizi ya misamaha ya nyuma umeanzishwa, Serikali inatakiwa kuweka wazi wanufaika wote wa misamaha hiyo na isiwaachie maofisa wa TRA kufanya kazi hiyo.
Akizungumzia Serikali kushtakiwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema kufanya hivyo ni haki ya mtu kisheria. Kuhusu pingamizi la Taffa kupinga agizo la TPA, Profesa Mbarawa alisema wapo ambao wameshatekeleza agizo hilo.
Maoni ya wasomi
Akizungumzia suala hilo, Profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua), Damian Gabagambi alisema baadhi ya mawaziri, wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa Serikali wanafanya kazi kwa woga ili kumfurahisha Rais. “…Pamoja na nia nzuri ya Rais Magufuli, kuna kila dalili kwamba watu wanafanya mambo kwa ushabiki bila kufuata sheria.” Alisema matatizo ya muda mrefu hayawezi kutatuliwa kwa muda mfupi huku baadhi ya watu wakiachwa na maumivu.
“Nchi inaendeshwa kwa taratibu, kuna kanuni za kuongoza watu… tusifanye majaribio,” alisema.
Mtaalamu wa masuala ya Katiba, Profesa Ruth Meena alisema katika utendaji lazima kuwe na hatua ambazo zinamwezesha mtu kufanya kazi kwa ufanisi.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hayo ni matokeo ya uamuzi wa haraka unaochukuliwa na baadhi ya viongozi hao ambao alisema wanaiga utendaji wa Rais Magufuli jambo ambalo alisema si sawa ndiyo maana wengine wanakimbilia mahakamani kwa sababu wanaona hawatendewi haki.

Last edited by a moderator: