SUZANE
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 740
- 502
Nawapenda wote!!
Ni juzi tu nilialikwa kwenye kitchen party ya jirani yangu Mwanauba, nilijuta kwanini nilikwenda maana nilijikuta nikipoteza raha yangu yote.....
Mama mmoja ambaye alialikwa kumfunda Mwanauba alikuwa akiongea maneno ambayo yalikuwa yakiniuzi kila alipoendelea kuongea, nilitembeza macho yangu huku na huku kutizama wenzangu kama walipokeaje yale mahusia ya kungwi kwa bibi harusi Yule mtarajiwa, chakushangaza watu walikuwa na furaha ya ajabu, hasa wanawake waliokwenye ndoa wa pale mtaani, walishangilia na kupiga vigelegele za shangwe!!
Moyoni sikuona kama huo ndio ulikuwa wakati muafaka wakusemea maneno yale pale ukumbini, nilidhani mambo ya ndani watakua wameshamwambia Mwanauba na pale ukumbini ni kuserebuka tu Utamu wa Yesu!!
Alianza hivi, Mwanangu Mwanauba ukibeba ndoo ubebe na kidumu mkononi, kuna bahati mbaya mwanangu waweza jikwaa ndoo ikaanguka na maji yakamwagika ukabaki na kidumu kikakufaa kuoshea vyombo, kumbuka siku zote chombo hakiendi ila kwa nyenzo mwanangu, Mwanauba mkono mmoja hauchinji ng'ombe hata siku moja kaa ukijua hilo mwanangu, hakika Mwanauba tendegu moja halisimamishi kitanda tumia akili!!
Watu walipiga kelele za furaha wakati kungwi Yule akimalizia na kusema hivi, mwanangu Mwanauba namalizia na kusema hivi, jifya moja haliinjiki chungu, sharti matatu ili chungu kikae vema jikoni asante MC asante sana!!!
Mie nilibaki hoi nikijiuliza hawa makungwi wanatufundisha nini?? Wanaifundisha nini jamii?? Je Mwanauba jirani yangu amejifunza kitu gani pale!! Mbona wakina mama nanihii walikuwa wakishangilia sana na kupiga vigelegele kwa kuonyesha waliambiwa kitu ambacho wanakifanya au walitamani kukifanya hivyo walikosa mshauri tu!!
Baada ya sherehe nilijirudia zangu nyumbani kwangu kama shomoro alienyeshewa na mvua!!
Nawatakia wakati mwema rafiki zangu!!