Justine Marack

JF-Expert Member
Jul 31, 2014
567
1,550
Mwanangu wa kike anaogopa sana wafu.
Hufikia mpaka kuwalazimisha marafiki zake nao waogope wafu.
Huyu Binti huwatishia kuwanyima peremende ikiwa rafiki zake hawataogopa mfu.
Kuna mfu Mmoja mashuhuri sana. Kila tulianza kumzungumzia basi Binti huyu kukimbilia kubadili mada au kwenda kwa jirani zangu.
Sasa na huyu wakiume naye amenza kuogopa wafu. Dada yake amefanikiwa kumjaza hofu.
Jamani nisaidieni kumuelimisha Binti yangu kuwa wafu hawarudii uhai.
 
Kwa Mila na desturi za kiafrika wafu ni 'the living dead, ni living spirits ambazo haziwezi kutenganishwa na wanaoishi. Nawapa hongera hao watoto wana akili, maono na spiritual zaidi kuliko baba yao.
 
😂😂😂😂😂😂sababu anahusika kwenye mkasa wa hao wafu hasa huyo mashuhuri
 
Inaonesha mwanao amekuzidi imani na upeo wa akili.

1) Amekuzidi imani kwasababu hakuna kiumbe kisichoogopa kifo na wafu. Hata mitume iliogopa kifo sambamba na kuogopa wafu na madhambi yao walioyatanguliza mbele kwa muumba wao.

Na mtu akifa, kitabu chake cha hesabu cha maombi yake binafsi hufungwa rasmi, kwamba hawezi kujiombea hata msamaha kwa muumba wake (Isipokua sadaka/maombi ya kuendelea alizoacha au anazofanyiwa, na dhambi za kuendelea alizoacha - mfano Kama aliacha danguro basi kila dhambi zinazotendeka humo ana asilimia zake huko anakoenda n.k).

2) Amekuzidi upeo wa akili kwasababu mtu mwenye akili ya kawaida wafu ni kitu kisicho ogopeka na kisichokua na madhara. Ila hakika, kwa mtu mwenye upeo mkubwa wa akili mfu ni kitu cha kuogopwa sana kwasababu huwa kinaambatana na mambo mengi tusioyaona kwa macho ya kawaida. Na pia watu wabaya hutumia wafu au vitu vilivyotumika kumuandaa mfu kufanyia mambo mabaya sana, kama vile uchawi na ulozi.

Huyo mtoto ni mwema, mpende na mlinde sana.
 
Mwanangu wa kike anaogopa sana wafu.
Hufikia mpaka kuwalazimisha marafiki zake nao waogope wafu.
Huyu Binti huwatishia kuwanyima peremende ikiwa rafiki zake hawataogopa mfu.
Kuna mfu Mmoja mashuhuri sana. Kila tulianza kumzungumzia basi Binti huyu kukimbilia kubadili mada au kwenda kwa jirani zangu.
Sasa na huyu wakiume naye amenza kuogopa wafu. Dada yake amefanikiwa kumjaza hofu.
Jamani nisaidieni kumuelimisha Binti yangu kuwa wafu hawarudii uhai.
Ndo mkome kuwalaza mabinti na maiti ndani. Mtu akifa zika siku hiyo hiyo.
 
Hyo roho ikatae mapema Ni mbaya sana ilinifanya niogope makaburi sana
Nilikuwa naogopa sana makaburi ila nilipofika kidato cha 5 nilisoma shule ambayo ni lazima upite makaburini (katikati) au pembezoni mwa makaburi ndipo ufike shuleni, na makaburi hayakuwa na uzio.

Mwanzoni niliokuwa mwoga ila baadae nilizoea kabisa, tulikuwa tunapita hata saa 8 usiku tukiwa tumetoka Club (Shimoni Ebony). Waliosoma JJ Mungai Mafinga wanalitambua hili. Na yale makaburi ilikuwa ni daily lazima mtu azikwe.
 
Mimi kaburi la mtu au watu nisiyowajua huwa sina hofu kabisa, ila kama huyo mtu ananihusu basi huwa napata hofu kidogo
 
Anaogopa kitu ambacho hakitomdhuru ambao ni wafu; mwambie walio hai ndo wakuwaoogopa sio wafu
 
Back
Top Bottom