Mwanangu amegongwa na Pikipiki

Mwanangu amegongwa na Pikipiki

Galadudu

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
2,304
Reaction score
780
Wamenigongea mtoto wangu asubuhi hii anavuka kwenda shule akiwa kwenye Zebra, magari yote yamesimama lakini yeye akajifanya ana haraka sana akaunga na baada ya kumgonga akataka kukimbia.

Sasa hapa tupo Hospitali, tukitoka hapa huyo jamaa nitamshughulikia mi mwenyewe, nna hasira nae sana.
 
Pole sana Galadudu kwa yaliyokupata, tunaomba Mungu amponye mwanao haraka. As for the bodabodas hilo ni janga, serikali inapaswa iwaze mara mbili juu ya uamuzi wa kuruhusu bodaboda nchini
 
Wamenigongea mtoto wangu asubuhi hii anavuka kwenda shule akiwa kwenye zebra, magari yote yamesimama lakini yeye akajifanya ana haraka sana akaunga na baada ya kumgonga akataka kukimbia. Sasa hapa tupo hospital, tukitoka hapa huyo jamaa nitamshughulikia mi mwenyewe, nna hasira nae sana.

Pole Mkuu kwa yaliyokukuta! Tumwombe MUNGU kwa maombezi ya mama bikra Maria amponye Haraka huyo malaika arudie kwenye afya yake! Jana huku kwetu wamegonga tena Mtoto Wa chekechea anatoka shule yuko na mama yake. Bahati mbaya mtoto yule alifariki dunia! MUNGU ampe pumziko la milele!!

Hii serikali ya ccm iliona ime-win kura za vijana kumbe imetuletea majanga!!
 
Mkuu msamehe tu huyo, unawezakuta hata yeye ni mgonjwa.
 
wabodaboda wanaongoza kukuza maendeleo ya viwanda vyetu.








hasa vinavyotengeneza VIROBA.
 
pole sana,hawa jamaa hawana hakili kabisa ..jana wameua mwanajeshi mmoja pale lugalo,zebra kama kawaida na boxer zao wakamfyatua mjeshi akafa hapo hapo.
 
bodaboda zisiruhusiwe barabara za lami,wahishie kupeleka watu huko ilo ndio suluhisho ajari nyingi zitapungua.
 
Pole sana Mkuu.. Bodaboda ni janga ambalo sijaona juhudi yeyote ya kujaribu kukabiliana na janga lenyewe zaidi ya wanasiasa kuendelea kubariki janga..
 
Wamenigongea mtoto wangu asubuhi hii anavuka kwenda shule akiwa kwenye Zebra, magari yote yamesimama lakini yeye akajifanya ana haraka sana akaunga na baada ya kumgonga akataka kukimbia.

Sasa hapa tupo Hospitali, tukitoka hapa huyo jamaa nitamshughulikia mi mwenyewe, nna hasira nae sana.
Pole sana mkuu ila punguza munkari acha sheria ichukue mkondo wake
 
pole mkuu.. ila ukimkamata umpige tu, basi watakuja bodaboda 100 hapo kwako kuandamana bora umsamehe tu
 
Back
Top Bottom