Samahani wataalam, kuna suala nashindwa kuelewa hapa, mwanangu ameangukia uchogo toka kitandani mpaka chini akaanza kutapika then akalala asubuhi kaanza kutapika tena, shida inaweza kuwa ni nini haswa? (Mtoto anamiezi 9)
Hiyo sio dalili nzuri, muda sio mrefu huenda akapata dege dege, akawa analia ovyo ovyo au kupoteza fahamu. Kuna jirani yangu mtoto wake alipata kitu kama hicho, na athari zake zimekuja kuwa mbaya baadaye sana hata baada ya kupona.
Huyo huenda kaumia ubongo, na huko kutapika niliwahi kumsikia mtaalamu fulani akisema huenda kunaashiria kuna mgangamizo mkubwa kichwani (alisema ni Rising of intracranial pressure?!)
Halafu mtoto akianguka akilala sana sio vizuri. Hii mitandao inawamaliza akili. Sasa mtoto kaanguka kwa nini usimpeleke hospital kwanza. Hivi muda wa kulogin unaupata wapi ?
Kuna vitu vya kuuliza kwenye mitandao na vitu vya kukimbizana hospital wazazi wa siku hizi tumeshindwa kutofautisha. Sijui ni uvivu wa kwenda hospital au shida ni nini
Wachangiaji wote wanajifanya wajuaaaajiiii. Mleta mada kwani wapi kasema hajampeleka hospital.
Kwa wale wenye watoto wataungana na mimi watoto hua wanaanguka sana yaani mpaka tunaogopa sema ndio unamuamuambia mtoto huko ndio kukua.
Sipingani na wanaotaka aende hospital coz huyu mpaka ametapika ni shida ila mnatakiwa mjue watoto hua wanaanguka sana yaaani na Mungu hua anawasasaidia sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.