Mwanangu ameangukia kisogo, anatapika nifanyaje

Mpeleke tu hospitali haraka sana.

Hiyo sio dalili nzuri, muda sio mrefu huenda akapata dege dege, akawa analia ovyo ovyo au kupoteza fahamu. Kuna jirani yangu mtoto wake alipata kitu kama hicho, na athari zake zimekuja kuwa mbaya baadaye sana hata baada ya kupona.

Huyo huenda kaumia ubongo, na huko kutapika niliwahi kumsikia mtaalamu fulani akisema huenda kunaashiria kuna mgangamizo mkubwa kichwani (alisema ni Rising of intracranial pressure?!)
 
Kwa mujibu wa daktari..Kama mtu ameamia kichwa..kutapika sio jambo zuri hata kidogo..mpeleke hospital kubwa Sasa hivi.
 
Inamaana asingetapika usingempeleka hospital hata kama ameanguka kiasi hicho?
 
Halafu mtoto akianguka akilala sana sio vizuri. Hii mitandao inawamaliza akili. Sasa mtoto kaanguka kwa nini usimpeleke hospital kwanza. Hivi muda wa kulogin unaupata wapi ?
 
Yaani mtoto wako kaangukia kisogo akatapika, ukaweza kalala nae bila kumpeleka hospitali, na asubuhi akaendelea kutapika...... ukaamua uje kuulizia hapa jf ukitegemea kupewa suluhu!?

Mmmh siku za mwisho
 
Kuna vitu vya kuuliza kwenye mitandao na vitu vya kukimbizana hospital wazazi wa siku hizi tumeshindwa kutofautisha. Sijui ni uvivu wa kwenda hospital au shida ni nini
 
Wachangiaji wote wanajifanya wajuaaaajiiii. Mleta mada kwani wapi kasema hajampeleka hospital.
Kwa wale wenye watoto wataungana na mimi watoto hua wanaanguka sana yaani mpaka tunaogopa sema ndio unamuamuambia mtoto huko ndio kukua.
Sipingani na wanaotaka aende hospital coz huyu mpaka ametapika ni shida ila mnatakiwa mjue watoto hua wanaanguka sana yaaani na Mungu hua anawasasaidia sana.
 
mpeleke hospitali haraka sana..huu utandawazi unawafanya wengine walemae ubongo..
 
Yaani mtoto wako kaangukia kisogo akatapika, ukaweza kalala nae bila kumpeleka hospitali, na asubuhi akaendelea kutapika...... ukaamua uje kuulizia hapa jf ukitegemea kupewa suluhu!?

Mmmh siku za mwisho
aisee ni hatari sana.

sijui tunakwama wapi?!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom