Mwanamme kumuomba pesa mpenzi wake, imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamme kumuomba pesa mpenzi wake, imekaaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sal, Nov 9, 2011.

 1. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wama JF naomba ushauri wenu, mwanamme kuomba pesa kwa mpenzi wake, ni sawa?
  Nina mpenzi ambaye kutwa ana shida yeye, mimi sijawahi kumuomba, lakini yeye ndio kila siku ana matatizo ya kutaka pesa, na sio ndogo. Nimechoka, sasa hivi nimeamua kumchunia. Naomba uzoefu wenu wakaka, hii maana yake nini? Anadai kipato changu kikubwa kuzidi yeye, na hapa katangaza ndoa. Ushauri wenu ni muhimu kabla sijajiingiza kichwa kichwa.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  wewe 'umemzoesha' afanye nini?
  unam honga na yeye anaenda kuhonga mwingine....
  kazi ni kwako
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kama ni mara chache its ok kuna kukwama. Ila kwa nature wanaume huwa wagumu kuomba pesa,ingawa wanaume wa siku hizi 'marioo' atakuomba mpaka ujute,

  huyo mwanaume wako kakugeuza gombe la maziwa full kukukamua. Inawezekana umemzoesha kajenga tabia, mwanaume wa ukweli asingekwambie kipato chake kidogo bali angefight azikamate kuliko wewe.

  Dada zinduka ukifanya mashkara utakua unampa hela ya kuhongea.
   
 4. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mi sioni tatizo hapo.We kama umempenda kweli mpe tu,tena hata zote ulizonazo!Ukipenda boga......!?
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Is it? Sio kama ana shida
   
 6. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Hii imekaa kama UK nchi za Afrika... Mwambie Mpenzi wake Awatambue Mashoga la Sivo Utasitisha Kumpa Pesa zinazomsaidia
   
 7. KAPERO

  KAPERO Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana mama. unajua, huwa kwa kawaida hutegemea mwanzo wenu ulikuaje. ikiwa kipato chako ni kizuri sana sio vibaya kumhudumia mpenzi wako.. ila jichunge sana isije ikawa umetana na kina papaa,, hawa wanaume wanao suka nyele na kutoga masikio.. hawa wanaodai haki isiyo patana na akili za viumbe wa Mungu.. hawa wakinababa wanao dai haki ya kuolewa..

  hizo hela ukimpa mwambie akuletee risiti maana.. ama kama anafanya mradi basi hakikisha mikataba yote unasimamia. na kama haijulikani anafanyi nini hizo fedha halali za jasho lako, bora ukawasaidie wazee wajane ana wenye shida.. utakua umetunza vema hazina yako.. huyo mvivu atakuja kuku zingua hata ukajuta kumfahamu.

  akili kichwani kwako. angalia utalia mie hata siwapendi kupe wanyonyaji na wezi. tapeli huyo ushaumia wewe sepa tu. jipange upya,..
  tena nilitaka kusahau mwambie akatafute kazi alipe zote ulizo mkopesha. piga hesabu unijulishe ni ngapi tena ikiwezekana uniletee huyo mtu. nataka nimfungulie ashitaka ya wizi wa kuaminika. haro bahati gani hiyo sisi tunahonga renyewe rinakula rushwa na mapenzi pia. duh nalionea gere hiro rijamaa rirete haraka mama.
   
 8. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  si haki sawa? Kama mna mapenzi ya dhati msaidie mwenzio. Pia msaidie jinsi ya kukuza kipato chake na kubana matumizi ili aweze kuishi kulingana na kipato chake bila kutembeza bakuli......anaweza kukuta sehemu nyingine kuna masharti kama ya kameruni.
   
 9. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Hizi ni enzi za usawa. Ukata hauchagui jinsia, rangi, kabila n.k. hivyo kama wewe una ukwasi endelea kumsaidia mpenzi wako, kumchunia maana yake unapenda akuburudishe tu huku wewe ukishindwa kumsaidia kwa matatizo ya kiuchumi aliyo nayo.
   
 10. gozo

  gozo JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  marioo..
   
 11. lutamyo

  lutamyo JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hivi ingekuwa wewe unamuomba omba kama wafanyavyo wengine ungesema... Hii ndo haki sawa mimi nakushauri 2 acha na hawa we mpe tu mwenzio so long as anakupa raha na kukufurahisha.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Wanaume wengi siku hizi wamekuwa maliyooo tutawasaidiaje sasa! Ingawa kuomba hela does not mean mwanaume amekugeuza atm,kama ana genuine issues. Kusaidiana ni jambo la kawaida
   
 13. M

  MyTz JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  changu chako, chako cha kwako mwenyewe...
  mtoto wa kike acha ubinafsi wewe, kuwa wawili ni pamoja na kusaidiana kimaisha...
  kuhusu swali lako...imekaa vyema!!!
   
 14. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  piga chini fasta!! Eboo anakugeuza atm!!! MiIMARIOO inaniboa kuliko majabanzi!!
   
 15. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  mbona mke wangu hata kipato hata kidogo na nampa bila malalamiko?hapo inategemea,labda huyo wako ndio hawa vijana wetu wa siku hizi,matumizi ya mashauzi sana!kazi kwako,suka u nyoa
   
 16. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hii thread imenitia hasira kidogo............

  Niliwahi kumsaidia mtu fulani (Najua atasoma hapa) kwa kujua kuwa ni genuine reason bwana weeee baada ya muda tukakorofishana na kufikia hatua ya kutoleana maneno makali sana alichoniambia ndicho kinanifanya nashindwa kumsaidia kwa dhati mpaka leo namsaidia kwa shingo upande na ni wakati huu ambao najua kabisa ana genuine reason bali kutokana na ile kauli yake Nanukuu kwa hasira "Ungejua ile pesa yako ndio inamtunza huyo fulani...aka mpango wa kando" Tena akaongeza msumari wa moto kwenye kidonda "Hata hizi simu nazokutukana nazo ni wewe ndo ulinitumia kutoka huko uliko" Imagine aahhh ngoja naona povu limenipanda ghafla.................................ngoja nitoke kwenye hii thread
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  dada nini tena? Mimi mkaka akinitokea namwambia nasoma nimefulia mbaya mwenyewe anatoka nduki balaa
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  kusaidiana kupo lakini ikizidi nayo kero.......kila mara shida yeye khaaa... atafute njia ya kuongeza kipato asikufanye wewe ndio njia ya kuongeza mapato yake
   
 19. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wanawake wanataka haki sawa when it comes to relationships. Sasa mojawapo ya haki hizo, ni hii ya kuombwa na mwanaume wako. Siku hizi wako wanaume wengi tu ambao wanawaomba "mshiko wake au wapenzi wao" na mara nyingi wanawake huona hii ni abnormal.

  Lakini ukweli tujue kuwa ile cultural veil ya kwenye mahusiano inapovunjika, basi kuna matokeo ambayo wengi hawakuyatarajia. Mojawapo ni kuwa kuna wanaume wengi tu wenye mentallity ya utegemezi ambao, given the chances, wangependa hata wawe kina baba wa nyumbani.

  Wapo na ni wengi tu. Sasa hapo inategemea kama mwanamke uko tayari kubeba role ya kuwa PROVIDER. Ila ni hizi tamaduni tu tunazozichukia ndo zilikuwa zinawafanya wanaume wa namna hiyo kuwa waoga kuomba au kuwa tegemezi kwa wake zao.

  Bila hizi tamaduni, yes wanawake wengi mjiandae nanyi kuwa watoaji tu! Wanaume wapenda mitelemko wapo tu, tena wengi tu!
   
 20. m

  maliyamungu JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 481
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Wadada wa siku hizi wabinafsi sana nyinyi mnavyosaidiwa? Au sio hela mav*zi.
   
Loading...