Mwanamme kumuomba pesa mpenzi wake, imekaaje?

Mpaka unaandika humu JF inaonekana hili ni tatizo kubwa na huna pa kutokea maana hujaweza fanya hivyo kwa siku zote ambazo mwenzi wako amekuwa akikuomba msaada huo.
Kuna mambo ya msingi ya kuangalia hasa kwa wapendanao,je kipato chako kinatosha kumpa kila anapohitaji?Kama ndivyo basi angalia ni wakati gani wa kutoa na wakati gani usitoe maana inawezekana kweli akawa na matatizo ambayo labda hamjaweza kukaa chini na kuyazungumza kwa undani na kujua namna ya kuyatatua.
Kwa ushauri kaa chini na mwenza wako mzungumze kuhusu maisha maana hapa inaonekana kabisa hata kama ndoa katangaza ila hakuna mmoja kati yenu aliye wazi kwa mwenzake na hamna mpango wa kushirikiana katika matumizi jambo ambalo ni hatari mkiingia katika ndoa.
 
Nianze nakukupa pole, maana nijuavyo mwanaume muwajibikaji katika mapenzi hathubutu kumuomba hela GF wake na akibanwa sana basi ataomba amkopeshe. Pole yangu ina maana kwamba, lazima, narudia tena lazima siku moja utagundua kwamba hizo hela unazompa anahonga kwa demu mwingine. Na ukitaka ujue kwamba huo uhusiano wenu umeshikiliwa na hako katabia kako kampa hela, acha kumpa, utaniambia....
 
Tamaduni zetu zimetuumba kuamini kuwa mme ni PROVIDER na mke mpokeaji. Ndo maana kuna cases nyingi tu ambazo hata nazifahamu mke ana kipato kikubwa kuliko mme lakini bado, anafanya topping-up ya kipato chake kwa kuchukua kwa mme. Na inaonekana ni sawa tu hata katika macho ya watazamaji wengi. Wengi wanaona kuwa ni haki yao kula vya mme.

Tunasahau kuwa hii imeletwa na tamaduni tu. Kuna wanaume wengi wangependa kuwadandia sana wake zao kimahitaji, ila wanaogopa tu, au wake hawana cha kudandia! Mfumo unapobadirika kuwa wanawake na wanaume wana equal chances za kutengeneza kipato, basi tutarajie wanaume wengi sana kuingia kwenye udandiaji.

Tena wanaume wa hivi wako tayari kujishusha kwa mke awe chini, ili mradi afaidi vya bure. Wanawake wengi huwaona watu wa hivi kuwa ni wenye mapenzi ya ukweli, kumbe ni wadandiaji wa maslahi tu. Msemo wa marioo, ndo unaanza kushika kasi, ila siku za usoni tutarajie marioo wengi tu!
 
  • Thanks
Reactions: Sal
(Sal=chumvi) shida haina mwenyewe,we msaidie ili akatatue matatizo yake. Nalog off
 
Kusaidiana kawaida waliopitia university wanajua kuna kipndi mtu pesa zinakuishia na kama huna mtu anayekufaham chuon maisha yakuia magumu mana hata nyumban ukiomba msaada watakwambia husubiri! Mi mwenyewe namtegemea sana gf wangu endapo boom litachelewa bas yeye anakuwa responsible kuakiksha kuwa at least maisha yanakuwa mapes kiupande wangu,
 
Sioni tatizo kama kweli anazitumia hizo pesa kutatua matatizo yake, lakini kama anahonga wengine hapo sasa ndio pana shida.
 
Mara ya kwanza ni OCCURENCE,
Mara ya pili ni COINCIDENCE
Mara ya tatu ni DESIGN

Huwezi kuwa wee ndo unaishiwa kila siku hata kama kipato chako kidogo! Umeshaona kuwa kuna mahali pa kulalia, ndo maana ume-relax katika ku-control matumizi.
 
  • Thanks
Reactions: Sal
piga chini fasta!! Eboo anakugeuza atm!!! MiIMARIOO inaniboa kuliko majabanzi!!

So it is always wrong to think that love is a two way traffic. It is only a one way traffic, a man gives and a woman receives.

'Raha mnapata wote cha ajabu gharama kwako' - Nikki Mbishi
 
Hpa kwa upande wangu kuna mawili km ni mpnz tu na sio mume,kamwe huwa sitoi cash nitamnunulia zawadi au kumkopesha na atakapokuwa mume hapo kilicho changu kitakuwa chake pia,lzm tutashea matatizo na kuyatatua!otherwise hata iweje kamwe sihongi mwanaume.
Nakushauri acha kbs kumpa hizo hela then msikilizie itakuwaje na hiyo ndoa itatimia coz anaweza tangaza ndoa ili akuchune vizuri na kusepa zake ubaki unalia lia!
 
kama ana shida zinazoeleweka sidhani km kuna tatzo...pia mtu km anakupiga vibomu utamjua tu the way anavyokuja kuongea nawe. jitahd kumsoma vzr au wakt mwingne jarbu kumwambia kuwa kwa sasa cna hela umuone reaction yake.
 
hpa kwa upande wangu kuna mawili km ni mpnz tu na sio mume,kamwe huwa sitoi cash nitamnunulia zawadi au kumkopesha na atakapokuwa mume hapo kilicho changu kitakuwa chake pia,lzm tutashea matatizo na kuyatatua!otherwise hata iweje kamwe sihongi mwanaume.
Nakushauri acha kbs kumpa hizo hela then msikilizie itakuwaje na hiyo ndoa itatimia coz anaweza tangaza ndoa ili akuchune vizuri na kusepa zake ubaki unalia lia!

cantalisia..
 
Wama JF naomba ushauri wenu, mwanamme kuomba pesa kwa mpenzi wake, ni sawa?
Nina mpenzi ambaye kutwa ana shida yeye, mimi sijawahi kumuomba, lakini yeye ndio kila siku ana matatizo ya kutaka pesa, na sio ndogo. Nimechoka, sasa hivi nimeamua kumchunia. Naomba uzoefu wenu wakaka, hii maana yake nini? Anadai kipato changu kikubwa kuzidi yeye, na hapa katangaza ndoa. Ushauri wenu ni muhimu kabla sijajiingiza kichwa kichwa.

Kwa experience yangu, mwanaume muomba hela kwa mwanamke wake huyo ni sawa na shogo
 
Akikuomba hiyo pesa anasema anaenda fanyia nini? Ni vizuri mshauriane katika matumizi. Maisha ni kusaidiana, kama unaona yeye hakusaidii chochote isipokuwa yale mambo mengine, jaribu kumshauri apunguze matumizi yasiyokuwa ya lazima.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom