Mwanamke wangu hana siri, yaani asisikie kitu!

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Habari zenu wakuu,

Natumaini mwaka unaisha vizuri kwa wanaomaliza tofauti basi pole iwafikie!

Najitokeza hapa tuweze kushirikiana kwa pamoja nijue ni kwa mwanamke wangu tu au ni tabia za wanawake wengine wote, maana imekua kero sasa hii yaani kitu unamshirikisha mtu wako wa karibu na unamwamini tena unamwambia yeye pekee lakini azipiti ata siku mbili tatu hayo maneno unayakuta ofisini kwako, mtaani na kwa mashost zake ndio usiuulize kabisa!

Juzi kati hapa nilipatwa na habari si njema sana za kifamilia nyumbani kwetu basi nikaona vyema nimshirikishe mwenzangu lakini sasa habari zimeenea kila kona naulizwa!

Hivi Mungu aliwapa ubongo gani nyie wanawake hata siri tu kukaa na jambo moyoni inakua ngumu kweli?

Kwa hali hii ukute anawasimuliaga kila kitu jinsi navyomgeuza kila siku.


Niwatakie heri ya mwaka mpya wakuu JF
 
Sio tabia nzur kwa KE kutoa siri za mmewe ama familia yake inaonekana hajapatiwa mafunzo kabla ya ndoa anyway kutunza siri yoyote pia ni tabia ya mtu regardless ya ME au KE kama kweli no mke wako mkanye ila kama ndio tabia yake kuacha ni vigumu hivyo issue za muhimu usiwe unamwambia maana atazimwaga mtaani ILA kama bado girlfriend piga chini hafai kuwa mke
 
Wanasema mwanamke anaweza kutunza siri kwa muda gani vileeee!!! Kwahiyo akiiyoa sio kosa lake bali ni muda wa kuitunza umeisha.
Aiseee!
sio kosa lake?
kwaiyo nawewe ndio uko kumbe
 
Mwanamke ni kama mtoto, ishi naye kwa umakini. Kaa naye chini mwambie kinagaubaga tabia yake hiyo na pia kuwa mkali kidogo na umkanye sana, na angalia anajutia na kuomba msamaha. Kama anakiburi unaweza shirikisha watu unaoa waamini sana wachache wa pande yako na yake. Akiendelea na tabia hiyo bora umwache maana ni hatari kwa maisha yenu. Ipo siku siri nyeti za ndani zitavuja.
 
Wanawake wanabeba siri kubwa sana vifuani mwao....mfano anaweza kuwa amenyanyuliwa na wanaume zaidi ya 1000 alipokuwa binti na akaitunza siri hiyo hadi kufa.......
Sasa ukikutana na asiye na Siri mkanye nina uhakika atabadilika.....
Kweli mkuu! Ngoja nimwandalie dawa yake huyu
 
Huyo sio..Kuna mambo anatakiwa akae nayo asiseme kwa watu. Kama ni girlfriend tupa huko ila kama ni wife imekula kwako.
Mkuu haiwezi kula kwangu kizembe namna hii

Lazima anyooshwe kama pasi tu, haya ni mapuuza
 
wewe yamekushinda kuyatunza yeye ataweza wapi

siku ukiweza tunga siri zako wewe ndo siku na yeye hatakuwa na la kusimulia kwa watu.
Ni kweli mkuu
ila kumbuka ukioa unakua ni mwili mmoja we na mkeo

So jambo langu lazima nayeye limhusu
 
Back
Top Bottom