Kaka chunguza tabia ya mwanamke husika maana ndiye unayemuoa na si kabila, jitambue mwenyewe ni kitu gani kinachokuvutia kwa mwanamke, tabia gani unazotaka mkeo awe nazo, sura gani unayotaka mkeo awe nayeo, umbo gani n.k kisha angalia kama huyo unayetaka kumuoa anavyo vigezo hivyo? kama hana jiulize kama unaweza kuwa nae na ukampenda kwa dhati licha ya mapungufu aliyonayo? kama jibu ni ndiyo oa kaka. Mivuto ya wanawake hutofautiana kutoka mwanaume mmoja na mwingine, kinachokuvutia kinaweza kisinivutie hata kidogo na kinachonivutia kisikuvutie wewe si kwa sura tu bali hata tabia, hivyo nakushauri mchunguze kwa kina ili ugundue kama anakidhi hitaji la moyo wako ama la!