Mwanamke unayeishi naye akikwambia anakuchikia toka moyoni kuna haja ya kuendelea naye?

Hizo ni hasira tuu na inawezekana huwa hamaanishi. Wanawake silaha yao kubwa ni maneno ya kuuumiza ndo tunatumia kumuadhibu mwingine.

Ila kama anakuambia hayo mkiwa katika mazingira ya kawaida kabisaa hakuna ugomvi inabidi ujiandae anaweza kukuacha au kuna mwanaume mwingine anakula mzigo..... Jaribu kumfuatilia kwa makini utagundua kitu.

Akikuambia nakuchukia mwambie naomba tuachane halafu uone atakavyolipokea
 
Ndugu wanajamvi; nimeona nipate angalau maoni yanayoweza kunifanya nijue njia sahihi ya kuchukua ama nichukue hatua zipi baada ya kupata maoni na ujuzi tofauti kutoka kwenu.

Je mwanamke unaeishi naye kwa zaidi ya miaka 7 na mkafanikiwa kuuza mtoto mwenye umri wa miaka minne, ni akikuambia anakuchukia sana kutoka moyoni mwake, angali ww unampenda sana kuja haja ya kuendelea kuishi naye?

Na kama kuna haja kuna haja ya kuendelea kuonyesha ule upendo wa dhati kwake? Ni njia zipi zinazofaa kuthibitisha hilo?

Je naweza kuchukua hatua nyingine kwa kuwa hanipendi?
Je yawezekana akawa na mtu mwingine. Huduma zote huwa namtimizia. Ila yeye hataki kabisa kunipa hadi ule mchezo wa kitandani, na nikilazimisha huwa hashuguliki kwa chochote. Ingelikuwa ww ungefanyaje?

Naomba kuwasilisha nipate na mchango wenu wa mawazo.
Hapo inatakiwa umuache mara moja,ana anayempenda na kung'ang'ana kuishi naye atakuua.Mimi ilinitokea siku moja kidogo nigongwe na lori,kesho yake akanambia bora ungegongwa ukafa,wakati naplan niondoke nimuachie nyumba akaondoka mwenyewe na sikuwahi kumfuata tena na wazazi wake hawajawahi kunipigia simu au kuniita,mwaka na nusu umepita sasa.
 
Hebu tueleze kwanza ilikuwaje hadi akutamkie hivyo? Maana hapa tunaweza tukawa tunadeal na mihemko tu na sio real issue.
Hii ni mihemko tu ajadiliane naye wayamalize. Kuna kitu amemkosea naye analipiza kisasi huyo mama
 
Ipo shida hapo hawezi kuibuka tu na kufikia hatua hiyo jitafakarini upya mungu amewaunganisha hadi na baraka ya mtoto .plz usimpe shetani nafasi.
 
in
Ndugu wanajamvi; nimeona nipate angalau maoni yanayoweza kunifanya nijue njia sahihi ya kuchukua ama nichukue hatua zipi baada ya kupata maoni na ujuzi tofauti kutoka kwenu.

Je mwanamke unaeishi naye kwa zaidi ya miaka 7 na mkafanikiwa kuuza mtoto mwenye umri wa miaka minne, ni akikuambia anakuchukia sana kutoka moyoni mwake, angali ww unampenda sana kuja haja ya kuendelea kuishi naye?

Na kama kuna haja kuna haja ya kuendelea kuonyesha ule upendo wa dhati kwake? Ni njia zipi zinazofaa kuthibitisha hilo?

Je naweza kuchukua hatua nyingine kwa kuwa hanipendi?
Je yawezekana akawa na mtu mwingine. Huduma zote huwa namtimizia. Ila yeye hataki kabisa kunipa hadi ule mchezo wa kitandani, na nikilazimisha huwa hashuguliki kwa chochote. Ingelikuwa ww ungefanyaje?

Naomba kuwasilisha nipate na mchango wenu wa mawazo.
inategemea na mazingira yalikuwaje mpaka akakuambia hivyo inawezekana mlikuwa kwenye ugomvi ndo akasema hivyo,mara nyingi inaweza kuwa hasira tu ila hamaanishi hivyo ila endelea kumchunguza na kukaa chini kumuelewesha.
 
Kiongozi akuna mwanamke anae weza kuwa anakuchukia kutoka moyoni na ukakaa nae miaka yote iyo angesha ondoka,kuna kitu umefanya na unakijua sio bure,sasa wanaume wa kweli uwa tunakubali makosa unapo jua kosa lako na kuomba msamaha,na kama ujui jifanye fala uulize kosa lako utaambiwa, mme ishi miaka saba unafikiaje uamuzi wakumuacha unazani mtu ambae ujaishi nae kabisa ndo amta achana,bora uyo anaweza kukuvumilia miaka ikaenda maana anakujua kwa muda,tumia busara wanawake ni wale wale hata ubadilishe mpaka wapi usipotumia busara panapo itajika mwisho ni ..........
Tumia busara kwa faida ya mwanao
 
Hizo ni hasira tuu na inawezekana huwa hamaanishi. Wanawake silaha yao kubwa ni maneno ya kuuumiza ndo tunatumia kumuadhibu mwingine.

Ila kama anakuambia hayo mkiwa katika mazingira ya kawaida kabisaa hakuna ugomvi inabidi ujiandae anaweza kukuacha au kuna mwanaume mwingine anakula mzigo..... Jaribu kumfuatilia kwa makini utagundua kitu.

Akikuambia nakuchukia mwambie naomba tuachane halafu uone atakavyolipokea
Angesema ukweli tungemsaidia
 
Ndugu wanajamvi; nimeona nipate angalau maoni yanayoweza kunifanya nijue njia sahihi ya kuchukua ama nichukue hatua zipi baada ya kupata maoni na ujuzi tofauti kutoka kwenu.

Je mwanamke unaeishi naye kwa zaidi ya miaka 7 na mkafanikiwa kuuza mtoto mwenye umri wa miaka minne, ni akikuambia anakuchukia sana kutoka moyoni mwake, angali ww unampenda sana kuja haja ya kuendelea kuishi naye?

Na kama kuna haja kuna haja ya kuendelea kuonyesha ule upendo wa dhati kwake? Ni njia zipi zinazofaa kuthibitisha hilo?

Je naweza kuchukua hatua nyingine kwa kuwa hanipendi?
Je yawezekana akawa na mtu mwingine. Huduma zote huwa namtimizia. Ila yeye hataki kabisa kunipa hadi ule mchezo wa kitandani, na nikilazimisha huwa hashuguliki kwa chochote. Ingelikuwa ww ungefanyaje?

Naomba kuwasilisha nipate na mchango wenu wa mawazo.
Kuna pepo amepiga hodi kwenye mahusiano yako, mtafute Mungu harak kwa njia ya maombi
 
Mbona umezungumza kwa upande wako tu? Everything comes from somewhere ndugu
 
Ktk hali ya hasira, lakini si mara ya kwanza kurudia kauli kama hizo. Amekuwa akirudia mara kwa mara sana.
Yawezekana huwa anatamka hivyo kama njia mojawapo ya kupunguza hasira zake.
Tafuta muda ikiwezekana mtoe out zungumza nae kuhusu mashaka yako juu ya kauli hiyo.

Mtu pekee wa kukueleza ukweli juu ya jambo hilo ni yeye pekee.
 
Mpe psychological torture..Yani nuia moyoni kutosema chchote zaidi ya Salam kama akikupa...toa matumizi usiguse msosi wake...zidisha mapenzi kwa mtoto Yani awe ndo kampn yko Ukiwa home...usimuonyeshe kama una mchepuko Hata kama unao...asipowaita washauri ndani ya mwz mmoja Basi ni kweli hakupendi
 
Hizo ni hasira tuu na inawezekana huwa hamaanishi. Wanawake silaha yao kubwa ni maneno ya kuuumiza ndo tunatumia kumuadhibu mwingine.

Ila kama anakuambia hayo mkiwa katika mazingira ya kawaida kabisaa hakuna ugomvi inabidi ujiandae anaweza kukuacha au kuna mwanaume mwingine anakula mzigo..... Jaribu kumfuatilia kwa makini utagundua kitu.

Akikuambia nakuchukia mwambie naomba tuachane halafu uone atakavyolipokea

Nimekuelewa sana, una ushauri nilioupenda. Hebu ngoja nijaribu kufanyia kazi maoni yako
 
Nashangaa sana watu mnaolazimisha upendo! dhubutu, wenzetu waliona kama sio case wakanunua kabisa mwishowe wanajua walichonunua.

We tembea acha kuwa king'ang'anizi
 
Back
Top Bottom