Mwanamke unayeishi naye akikwambia anakuchikia toka moyoni kuna haja ya kuendelea naye?

MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
500
Ndugu wanajamvi,

Nimeona nipate angalau maoni yanayoweza kunifanya nijue njia sahihi ya kuchukua ama nichukue hatua zipi baada ya kupata maoni na ujuzi tofauti kutoka kwenu.

Je mwanamke unaeishi naye kwa zaidi ya miaka 7 na mkafanikiwa kuuza mtoto mwenye umri wa miaka minne, ni akikuambia anakuchukia sana kutoka moyoni mwake, angalia wewe unampenda sana kuja haja ya kuendelea kuishi naye?

Na kama kuna haja kuna haja ya kuendelea kuonyesha ule upendo wa dhati kwake? Ni njia zipi zinazofaa kuthibitisha hilo?

Je naweza kuchukua hatua nyingine kwa kuwa hanipendi?
Je yawezekana akawa na mtu mwingine. Huduma zote huwa namtimizia. Ila yeye hataki kabisa kunipa hadi ule mchezo wa kitandani, na nikilazimisha huwa hashuguliki kwa chochote. Ingelikuwa wewe ungefanyaje?

Naomba kuwasilisha nipate na mchango wenu wa mawazo.
 

MpiganiaUhuru

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
779
1,000
'Anakuchikia toka moyoni kuja haja' ya .....Mh!' Mungu utusaidie tu maana hakuna namna nyingine!
 

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
875
1,000
Mwambie yeye achukue maamuzi anayo ona yatakuwa na manufaa kwake na kwako. Kama atakuwa hakutaki atasema muachane; hapo utakuwa hauna jinsi zaidi ya kukubaliana na uamuzi wake, ila kama atakuwa kimya ujue huyo anatikisa kiberiti, mlainishe tu, wanawake viumbe dhaifu!! Atalegea tu!!!!
 

calisa

Member
May 8, 2017
35
95
Wee!! Unapotea nduguu huo sio upendoo!!
Huwez oteshaa mpapai jangwan afu ukatoa matundaa [HASHTAG]#kimbiaaa[/HASHTAG] muachee
 

ni ngumu

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
3,239
2,000
Mtu anakuchukiaje toka moyoni bila sababu wkt ni wapenzi na mtoto mnaye!sema umemfanya nn mtoto wa watu tukusaidie...ila km anakuchukia endelea nae mpk akuwekee sumu kwenye chakula
 

SADOCK NJIGINYA

Verified Member
Mar 26, 2013
1,168
2,000
asilimia 95 ya maoni watakwambia piga chini kwa upande wangu wewe fanya maamuzi utakayoona ni sahihi kulingana na moyo wako unavyotaka
 

Jael

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
67,180
2,000
Hebu tueleze kwanza ilikuwaje hadi akutamkie hivyo? Maana hapa tunaweza tukawa tunadeal na mihemko tu na sio real issue.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom