Zijue baadhi ya sheria za vita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Misingi ya sheria hizi imeanzia mwaka wa 1949 katika mkutano wa kimataifa wa kidiplomasia ulifanya marekebisho katika sheria nyengine za kimataifa za hapo awali

Vita vinapotokea katika maeneo mbali mbali vinaibua mjadala mpana, wa jinsi gani sheria za kimataifa zinatakiwa kulindwa, ambazo ndio msingi mkuu wa kuwalinda wale wasiokuwa na hatia, hasa wanawake, watoto, wazee na kuendelea.

Misingi ya sheria hizi imeanzia mwaka wa 1949 katika mkutano wa kimataifa wa kidiplomasia uliofanya marekebisho katika sheria nyengine za kimataifa za hapo awali. Sheria hizi zilijikita zaidi kuhakikisha usalama wa waathiriwa wa vita .

Mkutano huo ulifanya makongamano manne, ambayo yalipitishwa huko Geneva mnamo Agosti 12, 1949.

Je, sheria hizo za kimataifa za vita ni zipi ?

Kwanza kabisa usalama wa raia wasiokuwa na hatia.

Wakati wowote wa vita, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za vita, ni kinyume kushambulia majengo ya kiraia kama makazi, nyumba za ibada, shule na hospitali na miundombinu muhimu kama ikiwemo madaraja, barabara, vyanzo vya umeme na vyanzo vya maji.

Kuua au kumjeruhi mtu ambaye amejisalimisha au hawezi tena kupigana pia ni ukiukaji wa sheria hizo.

Kujali waliojeruhiwa
Waliojeruhiwa na wagonjwa daima wana haki ya kutunzwa na kupata matibabu, bila kujali wapo upande gani wa mgogoro.

Wafanyakazi wa matibabu na misaada ambao wako kazini katika maeneo haya ni sharti kulindwa kwa sababu hawaegemei upande wowote. Waandishi wa habari pia ni katika kundi la watu ambao hawapaswi kushambuliwa.

Pande zote zinazozozana lazima zichukue hatua zote zinazofaa kuhakikisha raia wanaotoka pande zote wanafikiwa na msaada ya kibinaadamu ikiwemo matibabu, chakula, maji au makazi.

Hivyo ni sharti kuwepo kwa makubaliano ya njia salama itakayotumika kwa shughuli hizo.

Pia ni haki ya wananchi kupewa tahadhari ya kuondoka katika maeneo hatari iwapo kuna mpango wa kushambuliwa maeneo hayo. Raia hawapaswi kamwe kuzuiwa kukimbia na kwenda sehemu salama.

Kulingana na Mikataba ya Geneva, ni marufuku kwa pande zozote zinazozozana kutumia silaha za maangamizi kama vile mabomu ya nuklia, mabomu ya ardhini, fosforasi nyeupe na kuendelea.

Anayevunja sheria hizi anafaa kushtakiwa katika mahakama ya nchi husika, au Mahakama ya Kimataifa ya Makossa ya Jinai- ICC.

Umoja wa Mataifa unaweza kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo ili kuchukua hatua stahiki.

Hata hivyo, tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi kumekuwana ukiukwaji wa sheria hizi pindi panapotokea migogoro.

TRT
 
Sheria za vita au utu wakati wa vita kwa kimombo, International Humanitarian law ni moja kati ya sheria pana sana zaidi ya mleta mada alichokileta jukwaani, hongera sana kwa kuketa suala hili wakati ambao vita vya Israel na palestina vinapiganwa huko Gaza.

Sheria hizi kama mleta mada ulivoeleza zipo kwaajili ya kuregulate hali ya vita and means and methods of warfare kabla, baada na wakati wa vita. Sheria hizi huitwa Geneva Conventions 1-4 and their Additional protocols 1-3. Sheria hizi pia hutofautiana kimatumizi kulingana na aina ya Vita inayopiganwa, yaani INTERNATIONAL ARMED CONLICT au NON INTERNATIONAL ARMED CONFLICT.

Sasa moja kati ya aspect pana sana katika hizi sheria na ambapo watu wengi huchanganya madensa na wakati mwingine Belligerent parties huchanganyikiwa juu ya kuheshimu hizi sheria ni during THE CONDUCT OF HOSTILITIES ambapo hapo sasa zile principles za vita hutakiwa kufuatwa yaani, PRECAUTIONARY., NECESSITY, DISNTICTION PRINCIPLES kwa kuzingatia MILITARY OBJECTS and CIVILIAN OBJECTS.

Katika hizo principle kuzifuata na kuziheshimu wakati wa vita ili kutimiza matakwa ya sheria kama ambavyo mleta mada umeeleza huketa ugumu sana wakati wa kupigana vita kwani pande zote huzijua sheria hizi na hutumia udhaifu wake kufanya yao, na ndio maana ukiona raia wanashambuliwa haimaanishi conclusion ni sheria zimevunjwa, kwani kuna vitu hufanya hao raia kukosa sifa ya kulindwa wakati wa vita.

Hongera kwa mada sema MADA NI KUBWA SANA
 
Misingi ya sheria hizi imeanzia mwaka wa 1949 katika mkutano wa kimataifa wa kidiplomasia ulifanya marekebisho katika sheria nyengine za kimataifa za hapo awali

Vita vinapotokea katika maeneo mbali mbali vinaibua mjadala mpana, wa jinsi gani sheria za kimataifa zinatakiwa kulindwa, ambazo ndio msingi mkuu wa kuwalinda wale wasiokuwa na hatia, hasa wanawake, watoto, wazee na kuendelea.

Misingi ya sheria hizi imeanzia mwaka wa 1949 katika mkutano wa kimataifa wa kidiplomasia uliofanya marekebisho katika sheria nyengine za kimataifa za hapo awali. Sheria hizi zilijikita zaidi kuhakikisha usalama wa waathiriwa wa vita .

Mkutano huo ulifanya makongamano manne, ambayo yalipitishwa huko Geneva mnamo Agosti 12, 1949.

Je, sheria hizo za kimataifa za vita ni zipi ?

Kwanza kabisa usalama wa raia wasiokuwa na hatia.

Wakati wowote wa vita, kwa mujibu wa sheria za kimataifa za vita, ni kinyume kushambulia majengo ya kiraia kama makazi, nyumba za ibada, shule na hospitali na miundombinu muhimu kama ikiwemo madaraja, barabara, vyanzo vya umeme na vyanzo vya maji.

Kuua au kumjeruhi mtu ambaye amejisalimisha au hawezi tena kupigana pia ni ukiukaji wa sheria hizo.

Kujali waliojeruhiwa
Waliojeruhiwa na wagonjwa daima wana haki ya kutunzwa na kupata matibabu, bila kujali wapo upande gani wa mgogoro.

Wafanyakazi wa matibabu na misaada ambao wako kazini katika maeneo haya ni sharti kulindwa kwa sababu hawaegemei upande wowote. Waandishi wa habari pia ni katika kundi la watu ambao hawapaswi kushambuliwa.

Pande zote zinazozozana lazima zichukue hatua zote zinazofaa kuhakikisha raia wanaotoka pande zote wanafikiwa na msaada ya kibinaadamu ikiwemo matibabu, chakula, maji au makazi.

Hivyo ni sharti kuwepo kwa makubaliano ya njia salama itakayotumika kwa shughuli hizo.

Pia ni haki ya wananchi kupewa tahadhari ya kuondoka katika maeneo hatari iwapo kuna mpango wa kushambuliwa maeneo hayo. Raia hawapaswi kamwe kuzuiwa kukimbia na kwenda sehemu salama.

Kulingana na Mikataba ya Geneva, ni marufuku kwa pande zozote zinazozozana kutumia silaha za maangamizi kama vile mabomu ya nuklia, mabomu ya ardhini, fosforasi nyeupe na kuendelea.

Anayevunja sheria hizi anafaa kushtakiwa katika mahakama ya nchi husika, au Mahakama ya Kimataifa ya Makossa ya Jinai- ICC.

Umoja wa Mataifa unaweza kuunda tume ya kuchunguza tuhuma hizo ili kuchukua hatua stahiki.

Hata hivyo, tafiti zinaonyesha kuwa mara nyingi kumekuwana ukiukwaji wa sheria hizi pindi panapotokea migogoro.

TRT
Hapo Gaza hizo sheria hazifuatwi na wenye dunia wapo kimya.
 
Ni hii yote ni kwasababu vita muda mwingine inasababishwa na wanasiasa walioshindwa kuelewana kwenye mambo yao na kuanza kutunishiana misuli
Maana la sivyo vita ni nchi kila mtu anatakiwa awe mbele kupigana
 
Back
Top Bottom