Mwanamke ni kama pasi!

Kimbweka

JF-Expert Member
Jul 16, 2009
8,597
1,683
Mwanamke huwa kama pasi huchelewa kupata joto na hutunza joto kwa muda zaidi hata baada ya kumaliza kupiga pasi.Inatoke mwanaume anafika nyumbani kutoka kazini anamkuta mke naye yupo nyumbani anamsalimia then anaenda zake chumbani kubadilisha nguo za kazini.
Anapata chakula cha usiku (Dinner) then anaanza kutazama TV au kupitia magazeti yake na kuyasoma.
Muda wa kulala umefika anaenda kuoga na kuvaa pajama zake; mke naye anaenda kuoga na kufanya sawa na mume.
Wanapanda kitandani, mume anampapasa mke, mke naya anajua mzee anataka maana ndiyo sex code yake akinigusa kwa mtindo huu maana yake anataka tuwe mwili mmoja na anajisikia kama kusumbuliwa maana alikuwa hajui kama mzee atataka kutokana na kutowasiliana hata hivyo anamkubalia.
... Baada ya dakika chache wamemaliza, wapo kimya na mzee anapiga usingizi.
Mke anajiona kama ametumiwa tu kwani hakukuwa na raha yoyote ni kuumizwa tu kwani mwili haukuwa connected hisia.
Kuna tofauti gani na chura hapa?
Kuwa na mahusiano na kimapenzi kwa mtindo huu ni sawa na kuiba akili ya asili ya chura (Frog’s love making instinct)
Mwanaume ni rahisi kusisimka kimapenzi wakati mwanamke huhitaji kusisimuliwa. Mwanaume husisimuliwa na moja ya mlango wake wa fahamu kupitia kuona (sight) wakati nwanamke husisimuliwa kupitia milango yote mitano ya fahamu Kuguswa, kusikia, kuona, kuonja, kunusa na wororo (tenderness) wa mwanaume.
Mwanaume ni mfano wa bulb ya umeme uki-switch tu mara moja inawaka wakati mwanamke ni mfano wa pasi ya umeme ambayo huchukua muda hadi ipate joto na hutumia muda zaidi to cool off.
Hii ni muhimu sana ukitaka kuwa mpenzi mzuri na mpenzi mzuri hujua na kuzingatia jinsi ya kumridhisha mwenzake.
Mwanamke anaongozwa na highway ya emotions, atajisikia vizuri sana kama alikuwa na idea kwamba kutakuwa na kuwasha pasi yake ya umeme mapema.
Itakuwaje kama wakati wa kuondoka asubuhi mume akampa mke busu la uhakika na kumnong’oneza mkewe kwamba “vipi unaonaje leo usiku ukawasha pasi mapema kwani nina hamu sana kupiga pasi nguo kwani naona bulbu yangu ina mwanga wa uhakika leo".
Nahisi mke atashinda anaweza jinsi ya kuhakikisha pasi yake inawaka chapchap usiku na ikitokea na mchana akaambiwa neon linguine mwororo inaweza kuwa jioni yenye mwako wa mahaba.
Kwa mawasiliano mazuri na kupeana quality time mwanamke huweza kufunguka kiakili, kimwili na kiroho na kuwa tayari kwa usiku wa kufurahisha na kuridhishana.
Ndiyo maana wakati mwingine ukipapasa usiku unaambiwa “baba nanii leo kichwa kinaniuma sana” au “nimechoka sana” au “unapata zero participation na kuambiwa maliza haraka” au pasi inakuwa kavu kabisa matokeo yake ni pasi inagoma kuwaka na kuanza kuumizana.
Jifunze kuwa mwanaume mwororo (tenderness) wasiliana na mke, tafuta muda wa kumsikiliza, cheka naye, cheza naye, ongea naye, mpe mgusu (touch), mkumbatie na kumbusu hata kama si wakati wa sex ni wako na ni wewe uliamua kuishi naye.
Mwanaume humtengeneza mwanamake!
 
"Pasi za mkaa".....ndivyo zilivo......mpaka ipate moto ufanye kazi haswa! Mbona "pasi za umeme" zenyewe hupata moto haraka?.....Lolz!
 
"Pasi za mkaa".....ndivyo zilivo......mpaka ipate moto ufanye kazi haswa! Mbona "pasi za umeme" zeneyewe hupata moto haraka?.....Lolz!

Kumbuka pamoja na uharaka wa pasi za umeme , haifikii uharaka wa bulb kuwaka....
 
Dah... Hapa MMU tushindwe wenyewe, mana naona kila angle imeguswa.... lol

Kwa kweli kama kuna watu wamependelewa humu JF ni hapa MMU..
Kama kwa nondo hizi bado mahusiano yanalegalega basi it wasn't meant to be...
BTW dadaangu AshaDii mzima??..mara ya mwisho nilikuona kule kwa Maxence!!
 
Last edited by a moderator:
nakugonga like nikirudi kwa pc......mimi tubelight,,,,mke wangu pasi ya mkaa.....siku nikiwa off mood nakuwa energy saver,,,utantaka sasa?
 
Back
Top Bottom