Mwanamke ni kama bunda la karata

Mwanamke ni kama bunda la karata

Namlaumu mnunua karata!
Wachezaji nao hovyo!
Si wacheze kwa macho ili karata zibaki kama zilivyo!

Hata hivyo lawama ziende kwa wachezaji!
Wasingefungua box karata zingechakaaje!

Nani aliewafundisha watu kuchezea karata?
Karata hazina mtetezi maskini!

Nani anamiliki karata?
Karata za nani?
Naomba karata zitunzwe mpaka apatikane mwenyewe!

Bila mchezaji hakuna jina karata !
Raha ya karata zichezwe!
 
Wanawake ni muhimu sana kwa Mwanaume na jamii yote kwa ujumla, kama kuna ambaye umekosana naye si wote, ni kama unavyokosana na Wanaume wenzako. Ukipata mwanamke akakupenda utahisi unaishi peponi. ila ikiwa bahati mbaya inabidi utafute suluhisho.
 
Omba lazi kwa wanawake huo ni uzalilishaji wa kijinsi.
 
makubwa ...mwanaume kumbi kumbi...mwanamke bunda la karata....kwani leo umekula nini ati?
 
Wanawake ni muhimu sana kwa Mwanaume na jamii yote kwa ujumla, kama kuna ambaye umekosana naye si wote, ni kama unavyokosana na Wanaume wenzako. Ukipata mwanamke akakupenda utahisi unaishi peponi. ila ikiwa bahati mbaya inabidi utafute suluhisho.
Jidanganye Amna mwanamke anayempenda mwanaumee!!!
 
Hamna lolote hayo ya tamaa sijui kupenda mteremko yapo kila upande mkuu.

Kwa hili umenifanya nikumbuke kale kausemi ka kila mwamba ngoma lazima avutie kwake ila ukweli nyie ndio wachakazaji.

Yaani hamjui kudumu na hizo karata.
Karata zote tunazokutana nazo zimeshatumika
 
Back
Top Bottom