Mwanamke nadhifu huvutia

Mwanamke nadhifu huvutia

Kalpana

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
37,013
Reaction score
73,645
Mwanake nadhifu anavutia sio tuu kwenye macho ya wanaume pia katika jamii nzima. Unadhifu huu sio wa mwili wake pekee bali na mazingira anayoishi hasa nyumba yake kwa ujumla. Wanawake siku hizi tumekua wavivu sana kwenye kuweka nyumba zetu nadhifu hapa utakuta mtu anajitahidi kuweka sebule tuu safi ukiingia jikoni ni hatari na vyumbani ndo usiseme. Wanawake siku hizi yuko busy kuji make up mwili wake ili tuu apige picha airushe kwenye mitandao ya kijamii.

Wamama wa nyumbani nao utaratibu wa kuoga japo mara mbili kwa siku umepotea mtu mpaka mda wa kulala ndo anaingia bafuni ni aibu mno maumbile yetu yanahitaji usafi mkubwa. Utakuta mama ananyonyesha haogi mtoto kamkojolea mara maziwa yametoka kifuani ukichanganya vyote hivyo ni kero kwa wanaotuzunguka achilia mbali waume au mabwana zetu.

Kila mtu anaweza kuwa nadhifu kulingana na umbo lake wale wanene kupita kiasi basi jitahidini usafi maana miili yenu inakua na jasho jingi kulinganisha na wembamba. Mwisho naomba tujitahidi kina dada/wanawake kujiweka nadhifu.

Karibuni kwa ushauri na maoni kama mmekumbwa na kadhia hiyo.
 
Hii hali ipo kabisa mkuu.dah tena umkute mwanamke anaenyonyesha uwiiiiiii ndo kabisaaaa.

Mkuu sasa siku nyingine ukiwa unaandika jitahidi kuacha nafasi kama hivi nilivyofanya.pole
 
Hahahaaa mbona. NIKAOGEE?

Sent from my Che2-L11 using JamiiForums mobile app
 
Ahsante kwa ujumbe.

Japokuwa kadri miaka inavyosogea wachafu wanaanza kupotea kwa sababu watu walio wengi wameanza kupata mwanga na kujua thamani ya usafi kuanzia kwenye miili yao mpaka mazingira yanayowazunguka.
 
Ahsante kwa ujumbe.

Japokuwa kadri miaka inavyosogea wachafu wanaanza kupotea kwa sababu watu walio wengi wameanza kupata mwanga na kujua thamani ya usafi kuanzia kwenye miili yao mpaka mazingira yanayowazunguka.
Dada hujambo...?

brain is the beautiful part of the body.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom