Mwanamke nadhifu huvutia

Mwanamke nadhifu huvutia

Hii hali ipo kabisa mkuu.dah tena umkute mwanamke anaenyonyesha uwiiiiiii ndo kabisaaaa.

Mkuu sasa siku nyingine ukiwa unaandika jitahidi kuacha nafasi kama hivi nilivyofanya.pole
Hahaa hahaa haya bana. Nilikua naogopa kuweka space nilijua patajaa haraka😀
 
Mwanake nadhifu anavutia sio tuu kwenye macho ya wanaume pia katika jamii nzima. Unadhifu huu sio wa mwili wake pekee bali na mazingira anayoishi hasa nyumba yake kwa ujumla. Wanawake siku hizi tumekua wavivu sana kwenye kuweka nyumba zetu nadhifu hapa utakuta mtu anajitahidi kuweka sebule tuu safi ukiingia jikoni ni hatari na vyumbani ndo usiseme. Wanawake siku hizi yuko busy kuji make up mwili wake ili tuu apige picha airushe kwenye mitandao ya kijamii.

Wamama wa nyumbani nao utaratibu wa kuoga japo mara mbili kwa siku umepotea mtu mpaka mda wa kulala ndo anaingia bafuni ni aibu mno maumbile yetu yanahitaji usafi mkubwa. Utakuta mama ananyonyesha haogi mtoto kamkojolea mara maziwa yametoka kifuani ukichanganya vyote hivyo ni kero kwa wanaotuzunguka achilia mbali waume au mabwana zetu.

Kila mtu anaweza kuwa nadhifu kulingana na umbo lake wale wanene kupita kiasi basi jitahidini usafi maana miili yenu inakua na jasho jingi kulinganisha na wembamba. Mwisho naomba tujitahidi kina dada/wanawake kujiweka nadhifu.

Karibuni kwa ushauri na maoni kama mmekumbwa na kadhia hiyo.
Hapa burudani kabisa.inasomeka bila kupepesa macho.big up
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom