Mwanamke Mghana alivyojifungua mtoto kwenye ndege kuelekea USA

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
1,235
3,194
Safari ya ndege iliyotarajiwa kuwa yenye utulivu kutoka Accra Ghana kuelekea Marekani iligeuka kuwa uzoefu ambao mwanamke mmoja mjamzito kutoka Ghana hatausahau maishani mwake, pamoja na wasafiri waliokuwemo ndani ya ndege ya Marekani United Airlines chapa UA 977.

Mwanamke mjamzito alipata uchungu wa uzazi,bila kutarajiwa na ikabidi rubani na wahudumu wa ndege kushugulikia suala hilo.

Mwanamke huyo ambaye alitarajiwa kujifungua mwishoni mwa mwezi wa Februari alishitushwa na kwamba mtoto wake mchanga aliamua kuzaliwa mapema.

Aliyeshuhudia tukio hilo, Nancy Adobea Anane ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo aliiambia BBC Idhaa ya Kipidgin kuwa tangu marubani walipotangaza watu walikuwa hawajafahamu kilichotokea.

"Wengi wao walisikia tangazo la kuomba usaidizi kutoka kwa daktari, lakini hawakujuani nini kilichokuwa kinaendelea" Nancy Adobea Anane aliiambia BBC Pidgin.

Akielezea hali iliyokuwa ndani ya ndege hiyo, Nancy alisema lilikuwa ni jambo la " mshituko na shangwe."

"Kujifungua kwake kulikuwa kwa haraka, kama dakika 30 hadi 45…kelele na kilio cha mtoto mchanga kikasikika… lilikuwa ni jambo la kufurahisha sana" anasema.
Shuhuda mmoja aliwaelezea waandishi wa habari jinsi sehemu ya ndege hiyo ilivyogeuzwa kuwa wodi ya kumpokea mtoto mchanga.

Dr Ansah-Addo ambaye ni Mghana anayefanyika kazi nchini Marekani alijitokeza kusaidia baada ya rubani kuomba usaidizi wa kimatibabu ndani ya ndege hiyo.

Chanzo: BBC
 
Itakapotua ndege ndipo anauvaa uraia wake . Wakitua Amsterdam atakuwa raia wa uhalanzi na kama hawatui, basi break ya kwanza ni JF Kennedy kwa ndege nyingi za kutoka ghana na anauvaa uraia wa marekani
 
Back
Top Bottom