Iran yakosoa uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Kibinadamu la UN

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,992
17,892
Iran yakosoa uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Kibinadamu la UN

Sep 02, 2023 11:30 UTC

[https://media]Ali Bahreini

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva amekosoa uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo.

Ali Bahreini, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X kuhusu uwepo wa Marekani katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa akiitaja nchi hiyo kuwa ni utawala wenye uraibu wa vita.

Balozi wa Iran amesema: "Hebu tuangalie utawala wenye uraibu wa vita ambao unaua zaidi ya watu elfu moja kila mwaka kwa kutumia jeshi la polisi, lakini bado unakalia kiti katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa."

Merekani imerejelea tena kuwa mwanachama katika Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, miaka mitatu baada ya kuondoka katika baraza hilo, mnamo 2018.

Marekani inalaumiwa sana kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu hasa za jamii za wachache kama Wamarekani weusi na Waiislamu, na mauaji ya kiholela yanayofanywa na polisi ya nchi hiyo.

Jinai ya karibuni zaidi ya polisi ya Marekani ni ile iliyofanywa na polisi katika jimbo la Ohio ambapo mwanamke mweusi mjamzito aliyejulikana kwa jina la Ta’Kiya Young amepigwa risasi na kuuawa na sakari usalama, jambo ambalo limeibua taharuki na hasira ya umma huku kukitolewa wito mpya wa kukomeshwa ukatili unaofanywa na polisi wa nchi hiyo.

Filamu iliyotolewa jana Ijumaa imeonyesha mauaji ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 katika maegesho ya duka la mbogamboga katika mji wa Blendon, kitongoji cha mji mkuu wa jimbo la Ohio, Columbus, Agosti 24. Mamlaka husika imesema mtoto aliyekuwa tumboni wa Young hakunusurika kupigwa risasi.

Familia ya mwanamke huyo imetangaza kuwa binti yao Young ambaye ana watoto wengine wawili alitarajiwa kujifungua mtoto wake huyo baada ya miezi miwili mnamo mwezi Novemba.
 
Tukiiacha USA , tukaiangalia Irab bas tutaita halaiki sio uvunjaj wa haki tu
 
Back
Top Bottom