Mwanamke mbinafsi hua mnaishi nae vipi??

Mwanamke mbinafsi hua mnaishi nae vipi??

BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Posts
921
Reaction score
2,244
Kuna mwana mmoja dereva wa bajaj, sasa kuna usiku mmoja alikesha ila biashara haikuwa nzuri. Asubuhi mkewe anataka hela ya pampas, akamwambia kama ana kaakiba akanunue, ila mchana akiingia mzigoni atampa, demu kakomaa ila jamaa akambembeleza, baadae akamfunga mtoto vikanga.

Sasa mwana siku hiyo alichelewa kuamka halafu simu, alijitupia alivyo rudi usiku wa jana, mke kaenda kununua vitafunio. Mwamba tafuta sana simu yake wapi, vurugua kitanda, kwenye makochi, upande wake kabatini ila wapi.

Akasema ngoja aangalie upande wa mkewe, kupekua pekua anakutana 1.2m, anamuuliza mkewe kwa aibu anadai mzee wao aliuza kiwanja alimpa kila mtu 1.5m kwa hiyo yeye kishatumia 300k kabakiwa na hiyo 1.2m, mwana alichoka, yaani mkewe kutoa mia tano kwenye 1.2m ya pampas alishindwa.
 
Wanawake ni wabinafsi kiasili na wengi wanakimbilika kukaa na wanaume kwa ajili ya kuhudumiwa.

Mfano hapo amekataa kutoa 500 ya hizo Pampasi .

Ila hata ukiumwa anaweza akakuacha .

Ndo maana Kama kijana wa kiume unabidi kuwa provider Ila usije ukasahu kuweka Akiba yako na kujikatia Bima kubwa ya Afya na ya Baishara .

These creatures are so selfish
 
Kama ni kweli timua huyo mwanamke sioni haja ya kuwa na mtu mbinafsi Mimi

Ndiyo ni jukumu la mwanaume kuhudumia kila kitu, Kuna wakati mambo yanagoma kabisa, Ila tunapambana upande wa pili napo unapata au kuna buma

Then mtu ana mpunga ambao atakuwa ni kutunzana na mashoga zake, kuweka nywele na nguo,

Huyo hakawii kununua uchawi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom