Mwanamke, kumchuna mumeo ni sawa na kujiibia mwenyewe!

Mwanamke, kumchuna mumeo ni sawa na kujiibia mwenyewe!

Naongea hivi maana wanawake wengi wa leo tunashindwa kutofautisha mume na mtu mpita njia au kwa maneno mengine mtu usie na uhakika nae kwamba mtaishi wote kama mume na mke.
Unakuta mwanamke keshaolewa badala ya kumshauri mume wake wajenge future yao ya baadaye na watoto wao,yeye ndo kwaaanza yuko busy anataka wigi la laki sita,anataka viatu vya laki 3, anataka iphone, nguo za Woolworth,starehe kwa sana,na kushughulikia vya tumbo tu anasahau wako kwa nyumba ya kupanga wala hana habari.
Simaanishi kwamba wanawake waume zenu wasiwapendezeshe but acheni kudemand vitu visivyo na tija badala ya kujenga future yenu. mambo ya kucompete na mashost zako so nawe unataka uonekane umo unamgeuza mumeo buzi wakati ni mume wacha.
Mwanamke Bana matumizi vizuri, weka mahesabu yako sawasawa ,mshauri mumeo mfanye mambo ya maana achana na mawigi ya laki 6,kufanya showoff wakati hamna nyumba maana kesho watoto hawatalala kwenye hilo wig la laki 6.
Umeshaolewa maana yake mko na huyo mumeo kujenga kesho yenu itayokuwa the best.
Wachaneni na vitu visivyo na maana pindi mkishaolewa, msaidie mumeo kujenga future yenu na sio kumchuna maana ni sawa na unajiibia mwenyewe.
hahahahahah pole mkuu,yaani hawa wanawake wa siku hizi wanataka uwe subira kweli kuishi nao,lakini mkuu ukishaona mtu wa namna hiyo unabadili mwelekeo vile vitu vya msingi unavifanya kimya kimya maana mwisho wa siku mwanaume ndio unaonekana kilaza kwamba umeshindwa kuiendesha familia
 
Tofauti ya ndoa na mchepuko.
Kwenye ndoa tubane matumizi kujenga familia
Kwa mchepuko leta hela tujenge mapenzi.
Wanaume wenyewe hawa vinyonga.
Leo jibane weee mjenge future kesho akizipata mnaachana kama mpangaji na mwenye nyumba.
Aku.
si kama kuachana si kuna sheria mpendwa? mnagawana mali. but mi naona tuache kuwaza negative kila wakati,kwanini uwe kwa ndoa unakuwa mguu mmoja nje mwingine ndani?.
 
We mpendwa acha hizo, kwa mkeo mama tujibane bane hali mbaya wali maharage mezani, kwa mchepuko jogoo zima linawekwa kwenye sahani mnalimaliza akaaaa tafadhali tena tafadhali sana
Teh teh..Mpendwa kwann mnawaza kuibiwa tu kila mara...Sasa hayo mambo ya kudemand mavitu yasio na tija unadhani ndo yatamzuia kuchepuka?
 
Wanaume wenyewe nyie?? Haya labda wafanye wa huko vijijini kwenu, lakini mjini humu thubutu yangu!
 
Teh teh..Mpendwa kwann mnawaza kuibiwa tu kila mara...Sasa hayo mambo ya kudemand mavitu yasio na tija unadhani ndo yatamzuia kuchepuka?
Mpendwa kuna threads nilishaandika jamaa kazaa na mtu afu huyo mtu ana watoto wengine wawili so jamaa anatunza mtoto wake na hao watoto wengine tena wa mwanamke wake, muda huko huo ana mke wanaishi wote
Hivi hapo mkewe ajibanee dada wa watu ale vidagaa af pesa inaenda kulea watoto wa watu khaaa hii ni ujinga first class
 
Kusavaivu kwa ndoa inatakiwa kukomaa nayo haswaaa, ukilemaa tu inakula kwako saaasa hiiivi!
 
Unamvumilia wewe kwa kila hali lakini huko nje yeye ndio boss,wanawake wanachoka nao wanaona bora wajiongeze. Mwanamke kiasili ni mvumilivu ila mkituendea kinyume msitegemee matokeo yaleyale. Inachosha mtu anaposhindwa ku appreciate inabidi uende na upepo tu.
 
Mara kaka ake ex nae anaomba hela ya pombe he he kujibana vepe, wanaoweza kujibana wajibane tu hadi wajambe
 
Nipange matumizi wakati Kuna mwenzangu hapangiwi matumizi akuuuu
Wanaume wa sasa sio kama zama za hapo nyuma. Unakuta mwanamke anajibana, anajitahidi muwe na maendeleo, yeye busy na mchepuko...unajidai kupanga matumizi na kufanya maendeleo yeye busy na michepuko, mbaya zaidi mchepuko haubaniwi......Mleta mada fanya uchunguzi makini ndo useme kuwa wanawake wanachuna waume zao. Asilimia 90% ya wanawake walioko kwenye ndoa wanalia sana kwa kufanywa wao spare.
 
Atakuwa amekaririshwa huyu,
Ila nanusa thread yake nyingine yaja yenye kichwa cha habar LAITI NINGEJUA!

Jibane weeeeeeee , siku ikifika uanze kusema kwa nini mimi! ! !
Kweny
Maisha ya kufikirika nayo yana raha yake teh kichwani naona naishi kwenye bonge la house nimepaki range yangu nkicheki pembeni garden moja matatraa kumbe kiuhalisia nimepanga chumba kimoja hata baiskeli Sina
 
Wanaume wa sasa sio kama zama za hapo nyuma. Unakuta mwanamke anajibana, anajitahidi muwe na maendeleo, yeye busy na mchepuko...unajidai kupanga matumizi na kufanya maendeleo yeye busy na michepuko, mbaya zaidi mchepuko haubaniwi......Mleta mada fanya uchunguzi makini ndo useme kuwa wanawake wanachuna waume zao. Asilimia 90% ya wanawake walioko kwenye ndoa wanalia sana kwa kufanywa wao spare.
Huko kujibana anajibana mwanamke tu, ila mwanaume akuuu hakuna kujibana
 
Ndio madhara ya kuoa mburulaz....mi nafkiri kuna makabila mengine ni ma mburulaz by nature. Kwa asilimia flan huwez oa mchagga ukajuta. Tehe
 
Usipomchuna wewe nje anaenda kuchunwa....bora mke uumchune lakini lengo likiwa na kuijenga familia kwa kuhakikisha mahitaji yote ya muhimu na lazma yanapatikana........
Umemaliza yote.....
 
Back
Top Bottom