Mwanamke kukuweka sero anastahili kusamehewa?

bussness

Member
Nov 29, 2014
46
20
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu, baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa. Je huyu binadamu anastahili msamah? Au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote.
 
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa je huyu binadamu anastahili msamaha au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote
Hii ni red kadi tatu kwa mpigo wala usiangalie nyuma wala kujdaili chap action period!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu, baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa. Je huyu binadamu anastahili msamah? Au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote.

MSAMEHE KWA ALIYOTENDA, TUISHI KWA KUSAMEHEANA NDIYO MAAGIZO YA VITABU VITAKATIFU
 
Akumuulikae mchana, usiku atakuchoma.
673fb6f08b1b15202d39feb2a514aa49.jpg
 
Mlipiga? Au ulimpiga mkuu!


Angalia nafsi yako inakushuhudia nini. Shida siyo kuwekwa sero tatizo kubwa ni kitu gani kiliwapelekea kugombana.

Kuna ndugu yangu alimkata mke wake na msumeno kwenye paja kisa mke wake alikuwa kasafiri kikazi na mme wake alikuwa anaijua safari hiyo.

Mama aliporudi jamaa akaanzisha ugomvi usiyo na kichwa wala miguu, matokeo yake akamkata mkewe na msumeno kwenye paja. Mke akaamua kwenda polisi na jamaa akaswekwa ndani. Mtoto wao ndiye alikuwa shahidi polisi. Jamaa akashauriwa aombe msamaha vinginevyo hali ilikuwa mbaya kwake.

Kama ilivyo kawaida mke akasamehe wakarudi nyumbani. Hivi sasa wanaishi maisha ilimradi tu mawasiliano hayapo kabisa. Mme vituko vimezidi.

Hivyo angalia shida ni nini siyo kuwekwa sero tu.
 
Nina mke tumeishinaye kwa miaka kadhaa juzi kati imetokea kutoelewana kati yetu ugomvi wetu ulikuwa mkubwa kiasi cha kupigana japo hakuna aliyeumia kati yetu, baadaye alikimbia police na kufungua kesi ya shambulio nilikamatwa na kuchukuliwa maelezo na kuwekwa ndani kesho yake kaja na ndugu zangu kama watatu akiomba msamaha na mdhamana nisiende mahakamani baadaye nilidhaminiwa. Je huyu binadamu anastahili msamah? Au nimpotezee maana alikuwa na nafasi ya kushirikisha ndugu kabla ya yote.
Napenda sana wanaume wajinga wanapoumia roho baada ya mtenda kutendewa, unabahati alikutoa, mie usingeniona na ndugu taarifa hakuna kupewa mpaka uzoee kunyea debe. No man shall ever lay a finger on his wife, Period.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kama mlipigana akakupeleka polisi na umeshapata dhamana nadhani ni muda muafaka na wewe kumpeleka police ili ajue ubaya wa case,hiyo sio ya kujiuliza mara mbili utajikuta unaingia ngome bila kutegemea.
 
Story kama hii ya upande mmoja hasa kwenye masuala ya ndoa ni vigumu kushauri kwa kuwa muwamba ngoma daima huvutia kwake.......

Lakini naweza kuhisi ni jinsi gani wewe unavyoiendesha familia yako kibabe hata unashindwa kutafuta suluhu katika masuala madogo kama hayo....hadi mkafikia hatua mkapigana......

Kwa jinsi ninavyoona na ulivyoelezea kwa kuangalia upande ni wazi kuwa mkeo anakupenda sana...na amekuvumilia na mengi.....tukio la yeye kukimbilia polisi kuripoti na katika kutetea usalama wake kwani dunia imeshachafuka na kila leo tunasikia au kuona wanaume wanavyowachinja wake zao kikatili.........

Kwa upendo alionao akashindwa kuvumilia kuona mumewe kipenzi aende jela kwa masuala ya ndani....ndio maana akaona aje azuie ili usipelekwe mahakamani na pengine anakuja kufanya hayo hapo polisi ana majeraha yako........

Kwa upande mwingine wanawake ni viumbe vyenye maudhi na kutia hasira...lakini sisi kama wanamume ndio viongozi wao na kuwaweka sawa ni jukumu letu...
Pia tupaswa kuishi nao kwa akili....huku tukijitahidi kuwa wastahimilivu....kwani siku zote hasira huzaa hasara.....

Kaa chini na mkeo mzitatue tofauti zenu....kila mmoja ajishushe ili mrudishe amani na kujenga familia bora.......

Mafahari wawili daima hawakai zizi moja.....
 
Hiyo sio dalili nzuri kwa huyo mwanamke!huyo hata kukutilia sumu ni rahisi sana.kwa utaalam wangu huyo mwanamama ana wivu sana kuwa muangalifu sana roho isije kuacha mwili.kingine ucmpige tena mwanamke akileta maneno toka nje urudi baadae
 
Kumpiga mwanamke ni risk sana na kitendo cha uwoga wa hali ya juu....
Imagine mkeo anakupikia,anakufulia,anakuzalia,anakupa maku hata kama hana mudi,anakutunzia siri zako kibao na yeye ndie anakua wa mwisho kupata usingizi siku zote lakini hajawahi kukudhuru.
Una bahati kakuweka lokapu,wenzako waliwekewa Sumu,wengine limbwata na wengine waliishia kupigwa na vitu vizito kichwani wakiwa usingizini.
Bado anakupenda na ndio maana kakupeleka selo....na kama haitoshi kaja kukutoa na kukuomba msamaha.
Wenzako kama wewe ambao badala ya kupigana na maisha wakapiga wake zao walipelekwa mochwari.
Na hao wake zao wamebaki mtaani wanaponda raha na midume mingine inayojua kupiga wanawake kwa mahaba na siyo mkong'oto.
Change man na mshukuru mola kakupa MKE BORA na siyo BORA MKE.
Na ndio maana kakukumbusha ulipokosea.
 
kama wewe ulikua na guts za kumpiga mbona yeye asiwe na guts za kukuweka ndani.
the issue here ni kwamba wote mlifanya upumbavu uliosukumwa na hasira.
na alichokifanya kimetoa msamaha direct kwa kile ambacho kilikua kati yenu.
Hebu achana na hilo samehe kisha muhakikishe lililowafanya mkapigana halitokei tena.
 
Mwanamke wa aina hiyo ukisema umpige red card we ndo utaumizwa chakufanya we jifanye mjinga. Mkifika polisi/mahakamani we jifanye unampenda kuliko maelezo ila yeye hakutulia hapo watatambua yeye ndie shida. Mkifika tu home unambadilikia kwa maneno na utasusia mambo yake yote
 
kama bado unampenda usifanye maamuzi magumu ukaja kujutia.
kukupeleka polisi sio kigezo kuwa hakupendi labda alikuwa na hasira/mihemko sana akashindwa kujizuia ndio maana akaenda polisi chakufanya kaeni chini muondoe tofauti zenu sio kuwekeana vinyongo na visasi
 
Moyo wako unasemaje? Ila dalili ya mvua ni mawingu! Kuna siku utaenda jela
 
Back
Top Bottom