ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
asante sana kwa ushauri mzuri kiasi hichi ndo mana nilisema naitaji unishauri kwani mie yashanikuta na kunikumba na yakanisulubisha kiakili, kimawazo, na kimwili pia na hapa sasa naonge nawe nabaki nalia tu sioni msaada wowote juu ya dunia hii nimemwachia Mungu najua ndiye msaada wangu. kwani ndiye kimbilio na ngome imara kwake nakaa salama, nimeamua kumtegemea yeye maisha yangu yote (samahani nimeamua kufunga hapa)
Hakuna ujanja mwinginwe wowote zaidi ya kumshirikisha Mungu then akili zetu za kawaida zifuate baadaye zikiongozwa na Muumba. Wengi wetu huanza kutamani mtu halafu ndiyo huomba msaada kwa Mungu tayari akiwa na taswira akilini make ya mtu aliyemuona mchana sehemu fulani.
Aidha wengine huchagua wenzi kwa kuangalia muonekano wa nje kama vile urembo/utanashati, elimu, uchumi nk. vitu ambavyo huweza kutengenezwa na kuharibika. Ndiyo maana wengi hujikuta wameingia kwenye mahusiano na mtu ambaye si sahihi kwa nguvu ya vitu nilivyovidokeza hapo juu. Laiti kama wangelijua unaweza kuwa na mke/mume ambaye si mrembo/mtanashati kivile lakini wewe mwenyewe ukamfanya awe kama unavyotaka (kila kitu kipo madukani siku hizi).
Kama ni hela mnaweza kuoana mkiwa walala hoi, bila elimu lakini kwa umoj awenu mkajisomesha, mkaanzisha shughuli za ujasiriamali mkaondokana na umaskini mkiwa pamoja. Mara nyingi watu walioanzisha mahusiano kwa staili hii huheshimiana milele maana wakikumbuka walipotoka kila mmoja anamuona mwenzake ni sababu ya mafanikio.
