Mwanamke epuka kumuambia mwanaume wewe sio type yangu

tamu 3

Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
88
Reaction score
216
WEWE SIO TYPE YANGU

Mwanamke epuka kumuambia mwanaume wewe sio type yangu, wewe sio wa hadhi yangu, wewe huwezi kunimudu, katafute masikini wenzako huko Mimi ni wa viwango vya juu kama huna pesa usijisumbue you can't afford me n.k.....maneno haya yamewagharimu wanawake wengi sana.

Kuna wanawake wamezika hatma zao za mahusiano kwa sababu ya maneno kama haya. Mwanamke unaweza kuyaona ya kawaida ila mwanaume anayachukulia kwa uzito mkubwa sana.

Ni mbaya sana kumuambia mwanaume wewe sio wa hadhi yangu, you can't afford me. Maneno kama haya yamekuwa sababu ya wanawake wengi kujikuta wakiingia katika mahusiano au kuolewa na wanaume wazee ambao kimsingi ni sawa na babu zao.

Wengi wa wanawake wenye haya maneno ya nyodo na dharau ni wale ambao ukitoa ngono hakuna kingine kinachobaki katika mahusiano wanachokichangia.

Wewe kama huvutiwi au humtaki mwanaume fulani wewe mwambie tu "asante lakini samahani kwa sasa nahitaji kuwa peke yangu hadi wakati mwingine" au mwambie tu HAPANA kwa njia nyingine tu ya heshima na hekima kuliko kumpa maneno ya kashfa, dharau na nyodo ambaye yatageuka kuwa kitanzi katika maisha yako yote.
 
Most of them ni hawa watoto wa maskini wanaotoka huko kwao Nanjilinji na kuvamia majiji ya watu, halafu akabahatika kupata mtu wa kumvimbisha hapo town.

Kwahiyo kijana ambaye haujajipata, ukimsemesha huwa wanawaona kama Steve Nyerere kabla ya kujipata sababu ya uchawa.
 
Kuna mmoja alimtamkia mume wake usiku baada ya kuchakatwa kunako siku ya kwanza tangu wafunge ndoa kuwa mume wake si type yake. Jamaa akamuacha on the spot na sasa ana mke mwingine na yule mropokaji anatafuta mume wa kumuoa hajampata bado
 
WEWE SIO TYPE YANGU

Mwanamke epuka kumuambia mwanaume wewe sio type yangu, wewe sio wa hadhi yangu, wewe huwezi kunimudu, katafute masikini wenzako huko Mimi ni wa viwango vya juu kama huna pesa usijisumbue you can't afford me n.k.....maneno haya yamewagharimu wanawake wengi sana.

Kuna wanawake wamezika hatma zao za mahusiano kwa sababu ya maneno kama haya. Mwanamke unaweza kuyaona ya kawaida ila mwanaume anayachukulia kwa uzito mkubwa sana.

Ni mbaya sana kumuambia mwanaume wewe sio wa hadhi yangu, you can't afford me. Maneno kama haya yamekuwa sababu ya wanawake wengi kujikuta wakiingia katika mahusiano au kuolewa na wanaume wazee ambao kimsingi ni sawa na babu zao.

Wengi wa wanawake wenye haya maneno ya nyodo na dharau ni wale ambao ukitoa ngono hakuna kingine kinachobaki katika mahusiano wanachokichangia.

Wewe kama huvutiwi au humtaki mwanaume fulani wewe mwambie tu "asante lakini samahani kwa sasa nahitaji kuwa peke yangu hadi wakati mwingine" au mwambie tu HAPANA kwa njia nyingine tu ya heshima na hekima kuliko kumpa maneno ya kashfa, dharau na nyodo ambaye yatageuka kuwa kitanzi katika maisha yako yote.
Sahihi mkuu,hata sisi wanaume hatupaswi kutamka hivyo ni kukosa Hekima, maana hatujui mbeleni kuna Nini si kipato tuu,hata kusaidiwa kwa namba mbalimbali!
 
Mkuu usichojua wanawake ni watu wa majivuno. Pia mengi wanayosema hawamaanishi

Kuna wanawake wakikasirika humwambia mume mtoto si wako huyu. Hata kama copyright
 
Back
Top Bottom