Mwanamke aua mtoto wa mwanamke aliyetembea na mume wake

miss zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,919
2,000
Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Paskazia Andrew Sindano (17) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata panga kichwani mtoto Kashindye Mgemagiko (03) anayedaiwa kuzaliwa na mama mwingine mwenye mahusiano ya kimapenzi na mmewe.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,tukio hilo limetokea Februari 15,2019 majira ya saa 12 jioni katika kitongoji cha Emalaupena,kijiji cha Misayu kata ya Ubagwe halmashauri ya wilaya ya Ushetu.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa kuwa mama wa mtoto aliyeuawa inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa Paskazia na kupelekea kuzaliwa mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Haule.

Haule amesema mbinu iliyotumika ni kumkata panga kichwani nje ya nyumba yake,hata hivyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote

Kamanda Haule amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke malalamiko,kero na migogoro yao hususani ya kimapenzi katika ofisi ya serikali ya kijiji na mabaraza ya wazee ili kuepuka vitendo vya kinyama.

Darmpya
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,773
2,000
Kuna watu watamhukumu huyo "mwanamke" kutokana na rika lake

Mapendhi jamani duuh shikamooo
 

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
38,927
2,000
Duuh! Badala ya kuhangaika na Mume wake au huyo mwanamke aliyezaa na Mumewe ye anamalizia hasira kwa Malaika asiye hata na hatia.

Sheria ichukue mkondo wake ili apate kujifunza. Na hapo ye akiwa jela ajue ndio kawaachia wenzie Uwanja.
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,799
2,000
So sad .... wait WA mikoani mtaacha lini hayo mapicha picha yeny ya kuuana mbona mmekuwa na roho mbaya kiasi hicho !?

Mimi ningewaona wamaana kidogo laiti kama mngeitumia hiyo roho yenu mbaya Kumfanyizia Jiwe and co .

Kinyume na hapo nazidi kuwa wajinga tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
17,301
2,000
Miaka 17 sherïa iliyotumika kumhuumu Èlìzabeth Michael Lulù itumike na kwa huyu bìnti
 

Mngoni clothes

JF-Expert Member
Sep 24, 2018
203
250
Duuh! Badala ya kuhangaika na Mume wake au huyo mwanamke aliyezaa na Mumewe ye anamalizia hasira kwa Malaika asiye hata na hatia.

Sheria ichukue mkondo wake ili apate kujifunza. Na hapo ye akiwa jela ajue ndio kawaachia wenzie Uwanja.
Tena wataoana kabisa wazae mwingine, Aisee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom