Mwanamke aua mtoto wa mwanamke aliyetembea na mume wake

Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Paskazia Andrew Sindano (17) anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata panga kichwani mtoto Kashindye Mgemagiko (03) anayedaiwa kuzaliwa na mama mwingine mwenye mahusiano ya kimapenzi na mmewe.

Akizungumza na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule,tukio hilo limetokea Februari 15,2019 majira ya saa 12 jioni katika kitongoji cha Emalaupena,kijiji cha Misayu kata ya Ubagwe halmashauri ya wilaya ya Ushetu.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa kuwa mama wa mtoto aliyeuawa inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa Paskazia na kupelekea kuzaliwa mtoto huyo”,ameeleza Kamanda Haule.

Haule amesema mbinu iliyotumika ni kumkata panga kichwani nje ya nyumba yake,hata hivyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote

Kamanda Haule amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke malalamiko,kero na migogoro yao hususani ya kimapenzi katika ofisi ya serikali ya kijiji na mabaraza ya wazee ili kuepuka vitendo vya kinyama.

Darmpya
Sina roho ya namna hiyo, siwezi kutoa uhai ea kiumbe kwa sababu ya mapenzi, i winder kama huyo mwanamke ana kizazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afungwe mume wake kwa kuoa mtoto kisha wafungwe wazazi kwa kuozesha mtoto ndipo hukumu irudi kwa mtoto kumuua mtoto mwenzie
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom