Mwanamke apewe Haki kushawishi (Kutongoza)

mwemweremwemwere

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2016
Posts
605
Reaction score
681
Wakuu kwa mila na desturi zetu imezoeleka mwanaume kumfata mwanamke kwa ajili ya kuanzisha mahusiano.

Kwa sasa wanawake wameongezeka sana kwa idadi ikilinganishwa na wanaume. Tumefika pahala kuna wanawake wanalazimika kuparamia waume wa wenzao, hawa tunaowaita michepuko.

Ni wazi sasa tumefika pahala wanaume wameshakuwa bidhaa adimu. Hali hii ikiachwa kuendelea ni wazi vita ijayo ya dunia (WWIII) itakuwa ya kugombea waume.

Kwa sasa japo haijaandikwa au kuelezwa popote ikitokea mwanamke amemshawishi (amemtongoza) mwanamume basi mwanamke huyo hutazamwa kwa jicho tofauti sana na jamii. Atapewa majina yote mabaya unayoyajua wewe. Kwa maneno mengine mwanamke amekatazwa kushawishi (kutongoza)!

Kama suluhisho kwanini wanawake nao wasiruhusiwe kushawishi (kutongoza) wanaume na ikiwezekena waruhusiwe hata kutoa maali kwa familia ya huyo mume ili kuleta usawa na ushindani wa haki.

Wakuu karibuni tujadili bila panic.
 
Apewe haki kwani imechukuliwa na Nani..??
Mbona wanaweza kutongoza!
Au unafikiri mwanamke kutongoza mpaka aje akuambie..?
Mwanamke anaweza kukutongoza kupitia lugha mwili tu.. halafu swala la kutoa mahali ni utamaduni tu na ni makubaliano..

Nina experience ya kutongozwa na mwanamke mmoja kwa barua.. wapili lugha mwili ila anaogopa kusema na mwengine hivyohivyo pia...
Labda ungesema wahaswe wawe wawazi ktk kusema hisia zao juu yetu! Sasa na wakiwa hivyo dah!

Hebu tuweke kikao tuulizane tutakuwa tunakataa kweli au ndo tutaijaza dunia kwa spidi ya awamu ya tano😜😅
 
Nature inakataa.Me hushawishi ke ili akimpata atamlinda,atamlisha na ile sitaki nataka humstimulate me na mwisho wa siku akimpata hujiona mshindi mbele ya me wenzake.
 
Hahahah! Umenikumbusha kipindi nipo shule niliwahi kutongozwa na demu nikamkataa tena nilimuona wa ajabu, alikuwa rafiki wa demu wangu. Baadae nilikuja kujuta nikaapa siji kukataa demu. Nlipomaliza Form 4 kuna demu akajipendekeza sikuchezea tena hii chance ya kimasihara.

Mademu wanaotongoza wapo wengi tu, hapo mwanzo nilikua naona ajabu ila ni kawaida tu maana na wao pia wana hisia.
 

Iwe itakavyokuwa mkuu mwanamke ana majukumu mazito sana katika ndoa huwezi kumuongezea na mengine
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…