Mwanamke anayekupenda kweli

Mwanamke anayekupenda kweli

Siku hizi hakuna mwanamke wa aina hiyo. Wote ni wa tuma na ya kutolea.
Pole sana kijana kwa maswahibu hayo yanayowakuta 😅!!! Ukitongoza kipesa utawapata wadangaji na hayo ndio madhara yake...
 
Wanawake wako wengi sana,wanawajibika hata kuigiza upendo ili wapate wa kuwakojoza
 
siku nikimpata huyo nitaleta mrejesho ....
so far sijawah kutana na wa aina hiyo
 
Change
Screenshot_20210707-180815.jpg
 
Sio kazi ngumu sana kuelewa mwanamke anaekupenda kiukweli mwanamke anaekupenda kweli hawezi kukuomba wewe kitu chochote bali atachohitaji kutoka kwako sana sana ni muda wako na 'attention' yako kwake.

Hayo mengine kuhusu pesa, outing, shopping na mengineyo unatakiwa kujiongeza wewe kama mwanaume na sio kubweteka na kupendwa, kwa sababu mwanamke wako anahitaji matunzo vilevile.

Anachohitaji mwanamke ni wewe tu na muda wako. Wanawake wameumbwa na moyo 'strong' lakini katika suala la mapenzi na hisia wako 'sensitive' sana. Wanahitaji kupendwa na wanahitaji kuona akijaliwa.

Mwanamke akikupenda kweli kutoka moyoni mwake atahitaji awe na wewe muda mwingi, atakutext mara kwa mara, atakupigia simu every time when she feels she wants to talk to you.

Atakuwa kama mtoto mdogo anayehitaji kupendwa, kukumbatiwa, kubebwa na kutizamwa kwa umakini.

Mpende sana mwanamke wa aina hiyo, muda mwingine aweza kuwa anakufuatilia sana mpaka unajiuliza nina 'date' na shushushu ama nini? Ila unapaswa kutambua kuwa anakupenda kwa dhati na anataka ajihakikishie kuwa yupo peke yake kwako.

Ukipata mwanamke wa aina hiyo tulia, usimuumize wachana na mitambo mingine, utazunguka bucha zote lakini nyama ni ile ile sana sana utamaliza nauli yako na nguvu zako za kuzunguka kila bucha.
Kuna wanawake wengine hawatakiwi kupendwa hata kidogo, hivi mtu na akili yako utamuoa Kajala au mwanaye kweli? Wanawake wengine ni issue sana, wambea na hawana lolote lakini anakuganda ili tu akupate umtunze. Hasaidii chochote katika maisha yako bali kukutia hasara tu, wanawake dizaini hii wako wengi sana hapa Bongo.
 
Back
Top Bottom