Mwanamke anaposema "Mwanaume wake haeleweki" anamaanisha moja kati ya haya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
Ijumaa Kareem!

Moja ya sababu zinazofanya mwanamke amuache mwanaume kimahusiano ni pamoja na "kutoeleweka Kwa Mwanaume". Bila Shaka ulishawahi kusikia Kauli Kama hizi Kwa wanawake, wakisema mwanaume Yule haeleweki, mume wake haeleweki, mchumba wake haeleweki.

Haya ni baadhi ya mambo yanayomaanishwa na wanawake wasemapo Kauli hiyo.

1. Umeshindwa kumfanya ajione yupo peke yake moyoni mwako. Yaani hana uhakika yeye ndio utamuoa.

2. Kipato chako anashindwa kukikadiria. Hajui unafanya shughuli gani hasa inayokuingizia kipato. Hivyo hana uhakika na huduma utakazompa pindi utakapomuoa.
Kumbuka Mwanamke anahitaji Security.
Security yake ya Kwanza ni Kupendwa yeye pekeake. Pili, kuhudumiwa na kutunzwa.

3. Kutoa ahadi lakini unashindwa kuzitimiza.
Wanawake hupenda kukujaribu kwenye ahadi. Huweza kukuuliza; Baby utaninunulia Mkoba Kama ule wa Doreen, ni elfu 60 tuu.
Utajibu, atakuuliza lini, utajibu. Basi atasubiri hiyo siku. Ukishindwa kutimiza ahadi za namna hiyo zaidi ya tatu nne atasema haueleweki.

Kumbuka wanawake huwaelewa wanaume wanaotimiza ahadi hasahasa ahadi ndogondogo kwani kupitia kutimiza ahadi kunamfanya akuamini na azidi kukupenda.

Kwa mwanamke ni Bora usimuahidi kuliko utoe ahadi usitimize kwake analichukulia Kama Deni.

4. Kupoteza kumbukumbu.
Mwanaume anayepoteza kumbukumbu Kwa mwanamke huwa hamuelewi. Wanawake hawawaelewi wanaume wanaopoteza kumbukumbu hasa zile za muhimu kama birthday zao, au Jambo Fulani mliopatana.
Mwanamke anaona mwanaume anayepoteza kumbukumbu Hajali na sio responsible Man.

5. Kutoa Kauli za kumtisha.
Kauli Kama, ondoka kwenu, nitakupa talaka, nitaongeza mke mwingine n.k.
Wanawake huamini maneno zaidi kuliko hata matendo.
Mwanamke hawawaelewi wanaume wanaowatisha kuwa wanasema kweli au wanatabia na kuwatisha tuu.
Kadiri unavyomtisha mwanamke unamtengezea mazingira ya kujihami na kujiandaa Kwa lolote. Tena hata usipomfukuza anaweza kujipanga kuondoka mwenyewe wakati unamhitaji.

Wanawake hawapendi kuishi na mtu wasiyemuelewa. Wanaona usalama wao ni mdogo.

Hata hivyo mwanamke hapendi kumuelewa mwanaume Kwa baadhi ya mambo. Hasa Ratiba zake, maamuzi yake endapo litatokea Jambo la hatari kwenye familia.

Taikon niishie hapa.
 
Ijumaa Kareem!

Moja ya sababu zinazofanya mwanamke amuache mwanaume kimahusiano ni pamoja na "kutoeleweka Kwa Mwanaume". Bila Shaka ulishawahi kusikia Kauli Kama hizi Kwa wanawake, wakisema mwanaume Yule haeleweki, mume wake haeleweki, mchumba wake haeleweki.

Haya ni baadhi ya mambo yanayomaanishwa na wanawake wasemapo Kauli hiyo.
Tatizo wanawake wenyew ndo hawaeleweki mkuu.
Ngoja watakuja kufafanua hilo
 
Wanawake wanaeleweka Mkuu, labda wewe ndio huwaelewi.

Sifa Yao kuu ni Vigeugeu.
Ndio maana watu wanasema hawaeleweki lakini kueleweka kwao ni ugeugeu wao.
Ili uwaelewe inabd umiliki dunia,afya njema ,mizizi,miti shamba,mizimu ,ufundi ,uchambuz wa mpira,uwe umeiona movie iliyozinduliwa jana ,ujue kuogelea ,uwe mcheshi ,uwe na hasira ,.uwe mchapakaz ,uwe mtumiaji wa pesa vizuri, ukikosa nguvu za kiume atakukimbia maana hutoelewekaa ..
Anyway watakuja wajuvi kudadavua zaidi
 
Namba 5 kuna muda huwa naitumia anaponivuruga hasahasa anaponishutumu kwa jambo ambalo sijalifanya na anakazia.

Back
Top Bottom