Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,514
- 22,001
Hii ni maalumu kwa ladies wote ambao hamjaolewa.
Ni hivi, hupaswi kabisa kumwamini mwanamume anapokwambia "nakupenda" kabla hajakuoa.
Kwa kawaida mwanaume hutumia neno "nakupenda" akilenga kufanya ngono tu na mwanamke ili kutimiza tamaa yake ya mwili baada ya kuvutiwa na shepu yako tu, kisha hutoweka mazima baada ya lengo kutimiza na kukuacha na maumivu makali.
Wanawake wengi huwa hawaelewi maana ya neno "nakupenda" huwa linamaanisha nini kwa mwanaume!
Katika uchumba wa kawaida, mwanamume anaposema, “Nakupenda,” ni sawa na kukuambia tu kwamba anataka ngono.
Kwa wanawake wengi, huwa hawaoni kitu kama kufanya ngono tu, bali wao hupokea na kuamini juu ya kufanya mapenzi ya kweli na huunganishwa kihisia baada ya kusikia neno "nakupenda" wakitamkiwa na mwanaume.
Mwanamke, unapolala na mwanamume, unashiriki upendo wako - unaachilia mapenzi yako kwa mwanaume huyo. Lakini huyo huyo mwanamume ambaye si mwenzi wako wa maisha anakuona wewe kama kichezeo chake tu cha kumpa furaha yake ya ngono!
Ingawa wanaume na wanawake wote ni viumbe vya kihisia, lakini wanaume wengi huona ngono kabla ya ndoa kawaida tu kama shughuli ya kufurahisha mwili.
Akiisha kukuonja usitarajie simu au SMS baada tu baada ya kushiriki naye ngono kwa usiku mmoja na kuondoka, hatakutafuta hadi hamu yake ya ngono itakapomvaa tena ndipo atakutafuta tena akuchezee.
Isingekuwa kwa ahadi za kimaadili, kidini na kifamilia, wanaume wengi wangelala na kila mwanamke anayemvutia kingono.
Wanawake wengi mnaweza kuridhika na mwanamume mmoja anayejali, anayewajibika na wa kimapenzi, ila kwa wanaume ni ngumu sana kuridhika.
Ingawa wanaume wanapenda wanawake wa tabia, wanaume wanavutiwa zaidi na mwili wa mwanamke kwa muda tu ila kiukweli hakuna upendo wa kudumu. Ndio maana kuna wanaume wengi walio na uraibu wa ponografia, vilabu vya kuvua nguo na picha za wanawake uchi.
Ikiwa hutaki kuendelea kuumizwa na wanaume, sema HAPANA kwa ngono kabla ya ndoa hadi huyo jamaa atakapofanya ahadi rasmi na kufunga ndoa nawe.
Ndoa haihitaji umati kushuhudia - ni agano kati ya watu wawili na Mungu.
Huo umati utakaotaka kuualika kushuhudia ndoa yako hauwezi kuifanya ndoa yako kuwa ya agano lililo rasmi.
NB: wanaume tusicomment chochote tusome tu comments za wanawake, hili ni bandiko linalowahusu wao.
Barikiwa