Mambo mengine ni kuendekeza ujinga wa mtu. Kwa hiyo kuondoka kwake ndiyo ww utishike? Huyu mwanamke anaonekana ana alergy na wageni. Si akae mpaka mwisho athibitishe kama kweli unatembea naye? Kwa hiyo ndani ya hiyo nyumba mtakuwa hampokei wageni kisa mke ataondoka?? Hii imenisikitisha sana hata kam wivu hii naona imepitiliza.
Inaonekana kwa wakati wote wa ndoa yenu humthamini na kumheshimu mke wako, mara nyingi umekuwa humsikilizi ndiyo maana aliamua kuleta message kwako by action ya kuondoka. Hivyo JIFUNZE kumsikiliza na kumheshimu mke wako, sikiliza hisia zake.
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf
Mama B hiyo mizigo ikisafiri mnaichungaje? na je mnafahamu huwa inakutana na akina nani huko safarini?Ndio maana sisi wengine tuko reluctant kuingia kwenye hii institution ya ndoa kwani imani hamna kabisa. Looks like jamaa ailkuwa na nia nzuri tu ya kumsadia mgeni, jamani huyu mtu kalipoti kituo cha kazi kijijini siwezi kuimagine hali ilivyo huko so alihitaji mwenyeji ambaye ndio huyu kaka Mungu kamtumia. Does this mean tukioa au kuolewa tuache kusupport wale tunaowafahamu simply because ni opposite sex? Kama ndivyo basi kuoa au kuolewa ni bullshit, there is no meaning in it completely. Humu duniani we need each other wandugu kama si leo basi ni kesho.
Fukuza haraka huyo mgeni, nenda katafute mkeo haraka sana!nasisitiza tena haraka sana usilete mchezo na ndoa!
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf
Hapa duniani kila kitu hutokea kwa sababu. Kuwa kwako na raha leo usione kwamba umefika na kusahau shida za wenzako. Huyo kaka alisoma na huyo dada na kwa kuwa wanafahamiana aliomba afikie hapo. Na kwa jibu wa Gervace hajatuambia kuwa huyo mgeni alifika bila taarifa au lah!! Jamani kuweni wavumilivu msianze kuhukumu maisha mnayajua hasa mtu anapoenda kuanza kazi. Na pia mwanamke kwa upande mwingine ataondokaje nyumbani alafu atume message kwenye simu? Kama kweli yeye ni genuine kwa nini asikae chini ajadiliane na mumewe? Asije kuwa alikuwa anatafuta sababu siku nyingi ya kuondoka kwa huyo mumewe na hii ndiyo kaipata. Kingine ni rahisi sana kusema fukuza bila kuangalia madhala ya upande wa pili.
Nimepata mgeni jana wa kike, amelala kwangu na kesho anaondoka kuelekea kituo alipoajiriwa. Tulisoma wote kigoma na kwa sasa ameajiliwa hapa kijijini kwetu kikazi. Hamjui mtu huku tofauti na mimi. Hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi na hata sasa sina mpango nae. Mke wangu kaniandikia meseji fupi 'nakupisha oa'. Ametoweka nyumbani kwa sharti kuwa lazima dada huyu aondoke leo hii. Nimfukuze mgeni au nianze kumsaka wife?. Nishaurini wana jf
Huyo mkeo mpe siku 3 asiporudi nyumbani OA mgeni. Kwishney.