Mwanamke aliyelipwa kimakosa Sh milioni 151 kama fidia ya ugaidi agoma kurudisha

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mwanamke mmoja wa nchini Kenya amepelekwa mahakamani kutokana na mzozo wa pesa za fidia ambazo zilitolewa kwake kimakosa kutoka Marekani kuwafidia waathiriwa wa shambulio la kigaidi la mwaka 1998.

Mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Mary Ngunyi Muiruri alipokea Dolla 65,683.50 (Tsh milioni 151) kimakosa mnamo Novemba 2020, ambazo zilikusudiwa kumwendea Mary Njoki Muiruri, mwathiriwa wa shambulio hilo.

Mary Ngunyi Muiruri alishtakiwa na shirika lenye makao yake makuu nchini Marekani la Hazina ya Ubalozi wa Marekani uliopewa jukumu la kuwalipa fidia waathirika wa shambulio la kigaidi la 1998.

Mary Ngunyi Muiruri alishtakiwa na shirika hilo kwa kupokea pesa hizo, kuzitumia na kudaiwa kukataa kuzirejesha ambapo kwa sasa Shirika hilo sasa linataka Mahakama Kuu kumshurutisha Ngunyi kurejesha pesa hizo.

Mwakilishi wa shirika hilo, Charles Marr, aliiambia mahakama kwamba mkanganyiko huo ulitokea sababu ya majina ya mwanzo na mwisho ya wanawake hao na hayo yalisababishwa na kampuni ya sheria iliyowasilisha ombi hilo kwa niaba ya wahanga wa shambulio la kigaidi.

“Hitilafu ya kampuni ya mawakili ilitokea kutokana na kufanana kwa karibu kati ya jina la mshtakiwa wa kwanza na mwathiriwa halali. Isipokuwa kwa majina yao ya kati, mshtakiwa wa kwanza na mwathiriwa halali wana majina yanayofanana na yanavyoonekana katika hifadhi data/rekodi za kampuni ya mawakili.

“Kulingana na maelezo yaliyotolewa ninaamini kwa hakika kwamba kampuni ya mawakili ilifanya makosa na makosa ya kweli,” stakabathi za mahakama zilisoma kwa sehemu.

Ubalozi wa Marekani pia ulishirikisha benki iliyotumiwa pesa hizo katika kesi hiyo na hata hivyo, benki hiyo ilisema kuwa Ngunyi amekataa kuridhia ombi hilo la kurejesha pesa hizo.

Zaidi ya hayo, hati za mahakama zilifichua kwamba alitoa pesa hizo kwa kuandika hundi tisa kati ya Novemba 2020 na Januari 2021.

Ngunyi alishikilia kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa pesa hizo na benki iliarifu shirika hilo la Marekani kuwa tayari ametumia pesa nyingi kutoka kwa KSh 7 milioni. Hazina hiyo pia iligundua kuwa Ngunyi alikuwa ametumia pesa nyingi na salio lilikuwa $5,553 (TSh milioni 12.8) kwenye akaunti yake.

Source: kenyans.co.ke
 
Back
Top Bottom