Mwanajeshi auawa kwa ugomvi wa pombe ya kiroba

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Mwanajeshi mmoja nchini Uganda ameuawa na wananchi wenye hasira kali nchini Uganda kwenye shambulizi linalodaiwa kuchochewa na kugombea pombe aina ya waragi.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea katika Wilaya ya Bududa ambapo wananchi hao wenye hasira inasemekana walimvamia mwananjeshi huyo kwa kisasi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, mwanajeshi huyo mwenye miaka 32 aliyetambulika kama Fred Kimanai aliuawa wikendi na watu ambao walikuwa wanaomboleza kifo cha kijana Ivan Mukuma Wamalile.

Gazeti hilo linaripoti kuwa kadhia yote ilianza baada ya wawili hao ambao wote sasa ni marehemu kugombea pombe ya kienyeji aina ya 'kiroba' inayoitwa waragi.

Mwanajeshi huyo inadaiwa alichukua kisu na kumchoma mwenzake ambaye alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali.

Waombolezaji wa msiba wa Mukuma walimalizia hasira zao kwa kulipa kisasi kwa kumshambulia mpaka kifo mwanajeshi huyo ambaye amerejea nchini Uganda siku si nyingi akitokea Somalia ambapo alikuwa alikinda amani.

Msemaji wa polisi wa eneo hilo bwana Robert Tukei, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo mawili na kuwa uchunguzi unaendelea.

"Tumepoteza wau wawili katika mkasa huo, mwanajeshi na raia. Tunachunguza matukio yote mawili," amesema.

Bw Tukei ametoa onyo kali kwa raia kujichukulia hatua mikononi, na kuwa wote watakaobainika kushiriki kwenye mauaji hayo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

"Washukiwa watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya mauaji," amesema Bw Tukei.

Pia amethibitisha kuwa marehemu hao wawili walikuwa na ugomvi uliosababishwa na pombe.

Tukio hilo linatokea siku chache toka Uganda kupia marufuku utengenezwaji na usambazwaji wa pombe za waragi.

Miili ya marehemu hao imehifadiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Baduda ambapo inaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Msemaji wa kikosi cha jeshi ambacho Kimanai alikuwa anahudumu wamethibitisha kifo hicho.

"Tmempoteza mmoja wetu, lakini tayari tumeshatuma kikosi cha kuchunguza tukio hilo. Baada ya hapo tutajua nini cha kufanya kufuatana na ripoti tutakayopata," amesema Kapteni Abert Arinaitwe.

Mwaka jana, askari wa wanyamapori katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Elgon iliyopo kwenye eneo hilo aliuawa na wakazi wa Baduda baada ya askari mwengine kumuua moja ya wakazi wa wilaya hilo.

BBC
 
Back
Top Bottom